Akiwa na miaka 18 tu Abigail Chamungwana maarufu Abby Chams anaendelea kuimarika zaidi . Ni msichana ambaye nyota yake inazidi kung'aa . lakini kisichojulikana ni kwamba nyuma ya mafanikio mengi ya msanii huyu ni mahangaiko , pandashuka na changamoto.
Habari za moja kwa moja
Na Dinah Gahamanyi
time_stated_uk
Rwanda: Maafisa wa zamani wa waasi wa FDLR wahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela
Yves Bucyana
BBC Swahili
Mahakama mjini Nyanza imewahukumu Ignace Nkaka (La Forge Fils Bazeye), msemaji wa zamani wa FDLR, na Lt Kanali Jean Pierre Nsekanabo (Abega), afisa wa zamani wa upelelezi, kifungo cha miaka 10 jela.
Mahakama iliwapata na hatia ya kuwa wanachama wa shirika la kigaidi, ingawa wakati wa vikao vya kesi walikiri kuwa katika kundi la waasi bila kujua ni kundi la kigaidi.
Mnamo tarehe 12/2018, wawili hao walikamatwa kwenye mpaka wa Bunagana baina ya Uganda na DR Congo wakitokeana mjini Kampala kwa tuhuma za kushiri mkutano wa kuvuruga usalama wa Rwanda.
Kesi yao imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya miaka miwili.
Walishtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na kuwa katika kundi haramu la kijeshi lenye lengo la kuangusha utawala wa Rwanda ,na kufanya mauaji ya wananchi.
Mahakama haikuwakuta na hatia kwa mashtaka hayo.Jaji amesema kwamba hata ingawa mwendeshamashtaka alisema kwamba walikuwa katika ngazi za juu za FDLR lakini hawakuwa katika nafasi ya kuchukua maamuzi yoyote kuhusu mipango ya kundi hilo ya kuhujumu usalama wa Rwanda.
Kundi la FDLR lilikiri kuhusika na mashambulio kadha wa kadha dhidi ya Rwanda kwanzia mwaka 98 hadi 2012 ambapo watu wengi walipoteza maisha yao,na mali nyingi kuteketezwa.
Awali waasi hao wa zamani wa FDLR waliomba mahakama kuwaachilia huru na kuwarudisha katika maisha ya kawaida kama ilivyotokea kwa waliokuwa wapiganaji wengine wa FDLR waliorejea Rwanda baadhi wakawekwa katika taasisi za serikali pamoja na jeshi la taifa.
Kuhusu hilo,mahakama imesema wao hawakurudi nchini Rwanda kwa hiari yao kama ilivyokuwa kwa wapiganaji wengine.
Jaji wa mahakama amesema wamepunguziwa adhabu na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kutokana na wao kurahisishia vyombo vya sheria katika kesi hiyo pamoja na kutoa taarifa muhimu kwa vyombo vya usalama kuhusu hali ya makundi ya waasi mashariki mwa DR-Congo.
Ignace Nkaka maarufu kama La Forge Fils Bazeye aliyekuwa msemaji wa kundi la FDLR na Luteni Kanali Jean Pierre Nsekanabo maarufu Abega Camara hawakupwepo mahakamani na mawakili wao hukumu hiyo ilipotolewa.Mahakama imesema wana siku 30 za kukata rufaa.
Mahakama yaamuru Zuma arudishwe tena gerezani
Mahakama ya Afrika Kusini imeamua kuwa rais wa zamani Jacob Zuma anapaswa kurejea gerezani, ikisema kuwa msamaha wa kimatibabu aliopewa awali ulikuwa"kinyume cha sheria".
Muda aliokaa nje ya gereza haupaswi kuhesabiwa katika hukumu yake ya miezi 15 ,mahakama ya Pretoria aliamua.
Zuma aliachiliwa huru Septemba 5, kwa hali ya kiafya ambayo haikufichuliwa.
Alikuwa amefungwa gerezani kwa kushindwa kuhudhuria uchunguzi kuhusiana na na ufisadi wakati wa urais wake.
Bw Zuma mwenye umri wa miaka 79 alijisalimisha kwa polisi mwezi Julai, lakini kifungo chake, ambacho hakikutarajiwa kiliibua maandamano na uporaji.
Zaidi ya watu 300, wengi wao wakiwa ni kutoka katika ngome ya Zuma ya jimbo la KwaZulu-Natal , walikufa katika maandamano hayo ya ghasia.
Unaweza pia kusoma:
Kenya yaripoti visa vitatu vya kwanza vya kirusi cha Omicron
Kenya imegundua visa vitatu vya kwanza vya aina mpya ya virusi vya Covid 19 , Omicron vilivyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema visa hivyo viligunduliwa miongoni mwa wasafiri.
Wiki iliyopita, Uganda ilitangaza kuwa imegundua visa vya Omicron kwa wasafiri wanaokuja nchini, maambukizi ya kwanza kuripotiwa Afrika Mashariki.
Visa hivyo viligunduliwa kwa watu waliopimwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe ambao walisafiri kwa ndege kutoka nchi tano tofauti, mamlaka ya matibabu ya Uganda ilisema katika taarifa.
Watano walikuwa wametoka Nigeria, wawili kutoka Afrika Kusini - ambapo aina hiyo iliripotiwa mara ya kwanza - na wawili kutoka Falme za Kiarabu.
Siku ya Jumanne, matokeo ya utafiti uliochapishwa nchini Afrika Kusini yalionyesha shindano mbili za chanjo ya Pfizer ya Covid inatoa karibu asilimia 70 ya kinga dhidi ya kirusi cha Omicron.
Kuibuka kwa aina hiyo ya kirusi kulizua hofu kwamba inaweza kusababisha ugonjwa mbaya, maambukizo zaidi au kukwepa chanjo.
Viashirio vya awali vilionyesha kuwa inaweza kuambukizwa kwa haraka, lakini data ya kuzua matumaini kufikia sasa imependekeza kuwa chanjo bado hutoa kinga dhidi ya Omicron.
Unaweza pia kusoma:
Mchunguaji na mkewe washutumiwa kumbaka msichana wa miaka 16
Kamanda wa polisiwa jimbo la Ogun nchini Nigeria ametangaza kuwa mchungaji wa kanisa kwa jina Peter Taiwo na mke wake, Elizabeth, watafikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashitaka ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 na muimbaji wa kwaya.
Msemaji wa jeshi la polisi Abimbola Oyeyemi, ameiambia BBC idhaa ya Yoruba kwamba wawili hao walihusika katika tukio la ubakaji dhidi ya msichana huyo.
Bw Oyeyemi amesema mchungaji huyo na mke wake tayari wameomba msamaha kwa kile walichomfanyia msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.
Msemaji wa polisi alisema kuwa mke wa mchungaji alimwambia msichana kwamba Mchungaji alimtaka usaidizi.
Mara baada ya msichana kuingia ndani ya nyumba yao, mke wake alifunga mlango na ghafla mchungaji alianza mazungumzo na msichana huyo kabla ya kumbaka.
Bw Oyeyemi alisema kuwa baada ya mchungaji kumbaka msichana, mkewe alipatikana akiwa analia.
"Lakini mchungaji alimwambia msichana asimwambie yeyote kuhusu yaliyomtokea, kwasababu anaweza kufa’’
"Mke wa mchungaji pia alimwambia msichana kuwa amekuwa mwanamke baada ya kushiriki ngono na mchungaji ."
Msemaji wa polisi amesema msichana huyo binafsi alipeleka malalamiko kwa polisi akidai alibakwa na mchungani alimbaka.
Mahakama inatarajia kusikiliza kesi hiyo hivi karibuni, na kutoa uamuzi.
Rais Samia: Niko tayari kusamehe na kuanza ukurasa mpya
Aboubakar Famau
BBC Swahili, Dodoma
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema yuko tayari kusamehe na kuanza ukurasa mpya.
Hayo ameyasema hii leo alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa kisiasa wanaojadili hali ya demokrasia nchini.
Rais Samia ameyasema hayo baada ya kuombwa na mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini Zitto Kabwe kumsamehe mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema Freeman Mbowe ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi na uhujumu uchumi.
“Demokrasia ni kuheshimu sheria, uvunjifu wa sheria unavunja heshima, na serikali inashindwa kukuheshimu. Kusameheyana kupo,” amesema rais Samia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa aina hii kufanyika tangu rais Samia kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli.
Chadema, ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania tayari kimetangaza msimamo wake wa kutohudhuria katika mkutano huo.
Wakati huo huo, Rais Samia, amewataka wadau wanaoshiriki mkutano huo wa siku tatu kujadili namna bora ya kufanya mikutano ya hadhara bila kuvuruga amani na kutukanana.
Kauli hii ya Rais Samia inaonekana kuleta matumaini mapya kwa vyama vya kisiasa baada ya mikutano ya hadhara kupigwa marufuku.
Unaweza pia kusoma:
Rwanda yathibitisha kuwa na visa sita vya aina mpya ya corona- Omicron
Serikali ya Rwanda imethibitisha kuwa visa sita vya aina mpya ya virusi vya corona aina ya Omicron.
Imesema visa hivyo viligundulika katika sampuli zilizokusanywa kutika kwa wasafiri pamoja na watu wengine waliokutana na wasafiri hao, kulingana na taarifa ya wizara ya afya.
Imesisitiza haja ya watu wote wenye umri wa miaka 12 na zaidi kupata chanjo kamili na wale wenye umri wa miaka 18 na zaidi kuangalia uwezekano wa kupata chanjo ya kuboresha chanjo za awali.
Tangazo hilo limetolewa kwenye ukurasa wa Twiiter:
Rwanda imekwishawachanga asilimia 40 ya watu wake na hivi karibuni ilianza kutoa chanjo ya kuimarisha kinga ya chanjo za awali.
Unaweza pia kusoma:
Malta yawa nchi ya kwanza katika Muungano wa EU kuhalalisha bangi
Malta imekuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuhalalisha ukulima na matumizi ya kibinafsi ya bangi.
Watu wazima wataruhusiwa kubeba hadi gramu saba za bangi, na kukuaza mimea isiyozidi minne ya bangi nyumbani
Lakini kuivuta hadharani au mbele ya watoto itakuwa kinyume cha sheria.
Mataifa mengine kadhaa yana mipango sawa ya kufanya hivyo, kama vile Ujerumani, Luxembourg na Uswizi. Nchi kama vile Uholanzi huruhusu matumizi ya bangi katika hali fulani.
Bunge la Malta lilipiga kura ya kuunga mkono mageuzi hayo Jumanne mchana, huku mswada huo ukishinda kwa kura 36 za ndio na 27 za kupinga.
Waziri wa Usawa, Owen Bonnici, alisema hatua hiyo ya "kihistoria" itawazuia watumiaji wadogo wa bangi kukabiliana na mfumo wa haki na "itapunguza ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kuhakikisha kuwa [watumiaji] sasa wanakuwa na njia salama na mahali wanapoweza kupata bangi".
Video content
Bangi: Zijue nchi tano zilizoruhusu uzalishaji wa bangi Afrika
Tanzania na Kenya zinaongoza kwa uvutaji wa bangi Afrika mashariki
Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?
Kutazama ponografia nikiwa mchanga kulinisababishia ndoto mbaya- Billie Eilish
Mwimbaji Billie Eilish ameelezea jinsi alivyoteseka na ndoto mbaya baada ya kuonyeshwa ponografia za "matusi" kuanzia akiwa na umri wa miaka 11.
Akiongea kwenye SiriusXM, kijana huyo wa miaka 19 alisema sasa "amehuzunishwa" kutafakari juu ya kuzitazama video hizo .
Eilish alisema tukio hilo lilimpelekea "kutokataa mambo ambayo hayakuwa mazuri" alipoanza kufanya ngono.
"Ilikuwa ni kwa sababu nilifikiri hilo ndilo nililopaswa kuvutiwa nalo," mshindi huyo wa wa Tuzo ya Grammy alisema.
Eilish, ambaye anakaribia kufikisha miaka 20, ametumia muda mwingi wa maisha yake ya ujana akiangaziwa na umma. Alijitengenezea umaarufu kwa kuvaa mavazi ya mtindo wa baggy na amekuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu muonekano wa mwili kushiriki ngono alipokuwa akikua.
Mada ya ponografia iliibuka katika mahojiano kama inavyorejelewa katika wimbo, Male Fantasy, kwenye albamu yake ya Happier Than Ever.
Alimwambia aliyekuwa akimhoji Howard Stern kwamba sasa anafikiri ponografia "ni aibu" baada ya kutazama maudhui aliyoyaelezea kuwa "ya jeuri" na "matusi" alipokuwa akikua.
Eilish alikosoa hasa jinsi ponografia inavyoweza kuonyesha miili ya wanawake na matukio ya ngono.
Sudan yatuma wanajeshi zaidi mpakani na Ethiopia Vikosi vya jeshi la Sudan
Sudan imetuma vikosi zaidi kwenye mpaka unaozozaniwa na Ethiopia, na kutangaza kuwa wana udhibiti kamili wa eneo hilo huku kukiwa na mvutano na Addis Ababa.
Jeshi lilituma ujumbe wa kuwatuliza wananchi, na kuwaambia "walale fofofo". Sudan ilitangaza tarehe 1 Disemba kwamba wanajeshi wake walikuwa wamesambaratisha makaazi ya Waethiopia na kuyadhibiti baada ya kurushiana risasi na vikosi vya nchi hiyo jirani katika eneo la al-Fashaga.
Ilifuatia ripoti kwamba wanajeshi 21 wa Sudan waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika mapigano na wanajeshi wa Ethiopia katika eneo la Birkat Nourain huko al-Fashaga tarehe 27 Novemba.
Mapigano hayo mapya yalimfanya mtawala wa kijeshi wa Sudan, Luteni Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, kuapa kwamba nchi yake "haitaachia inchi moja" ya eneo lake kwa Ethiopia.
Unaweza pia kusoma:
Rais Samia kukutana viongozi wa upinzani huku Chadema kikigoma kushiriki
Aboubakar Famau
BBC Swahili, Dodoma
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hii leo anatarajiwa kukutana na viongozi wa vyama vya kisiasa nchini Tanzania.Rais Samia atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo wenye lengo la kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa na Baraza la vyama vya siasa.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa aina hii kufanyika tangu rais Samia kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu kufuatia kifo cha rais John Pombe Magufuli.
Chadema, ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania tayari kimetangaza msimamo wake wa kutohudhuria mkutano huo.
Wakati haya yakijiri, kiongozi wa upiinzani wa Tanzania aliyeko uhamishoni Tundu Lissu amepinga ajenda za mkutano baina ya Rais Samia Suluhu na vyama vya kisiasa. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bw Lissu amesema mkutano huo sio wa kujadili hali ya demokrasia:
Unaweza pia kusoma:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatano tarehe 15.12.2021