Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Korea Kusini walichapwa 1-0 na Sweden katika mechi ya Kundi F
 2. Mexico wanaongoza kundi hilo baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Ujerumani 1-0 Jumapili
 3. Tunisia walichapwa 2-1 na England
 4. Misri, Morocco na Nigeria wote walishindwa mechi zao za kwanza. Senegal watacheza kesho.
 5. Ubelgiji waliwachapa Panama 3-0

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Msimamo Kundi G baada ya mechi za kwanza

Ingawa Uingereza na Ubelgiji wakona alama 3 kila mmoja, Ubelgiji ndio wanaongoza Kundi G, baada ya kuitesa Panama 3-0.

Mabao ya Harry Kane limeipaisha Uingereza hadi nafasi ya pili.

Ni mara ya kwanza mchezaji wa Uingereza kufunga mabao mawili katika mechi mmoja. Mwingine ni Gary Lineker aliyefunga dhidi ya Cameroon 1990.

Tunisia ni ya tatu kundi hilo baada ya kulazwa dakika za mwisho kwenye mchuano uliomalizika.

Washiriki wa Kombe la dunia kwa mara yao ya kwanza, Panama, wanasalia nafasi ya nne kwenye jedwali hilo.

Mechi za Kundi G zitaendelea Jumamosi tarehe 23/6/2018 wakati Ubelgiji itachuana na Tunisia.

Uingereza itakua mwenyeji dhidi ya Panama Jumapili tarehe 24/6/2018.

Wachezaji wa Uingereza
Rex Features
Wachezaji wa Uingereza wakisherekea

Captain Kane bora kuliko Wayne Rooney?

Harry Kane ana mabao mengi kwenye Kombe la dunia kuliko Wayne Rooney.

Amefunga mabao mawili dhidi ya Tunisia.

Harry Kane
Rex Features
Harry Kane akitia bao kimiani

Kane akatiza ukame wa miaka 12! Tunisia 1-2 Uingereza.

Ukame wa Uingereza wa kutopata ushindi mechi ya kwanza Kombe la dunia mika 12 umekwisha!

Goli hilo lilikuwa lake la pili kufuatia kona.

View more on twitter

Harry Kane aiweka mbele Uingereza

Kane tena! Tunisia 1-2 Uingereza

Mabadiliko ya mwisho Tunisia

Awali kipa Mouez Hassen alimpisha mwenzake Farouk Ben Mustapha

Baadaye Naïm Sliti akatolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Ben Amor.

Nahodha Wahbi Khazri ameondolewa na Saber Khalifa ameingia

Ashley Young afyatua frikiki juu!

Uingereza inaendelea kusubiri bao lake la pili na la ushindi.

Loftus-Cheek amechukua nafasi ya Dele Alli.

Rashford asumbua

Ameingia dakika chache zilizopita, lakini nyota huyo wa Manchester United anaonekana kuitesa Tunisia.

Rashford
Getty Images
Rashford

Mabadiliko ya kwanza Tunisia

Naïm Sliti ametolewa na nafasi yake imechukuliwa na Ben Amor.

Sterling amepumzishwa.

Alionekana kuwa staa wa Uingereza kabla ya Kombe la dunia, lakini atasubiri mchuano ujao kuona bao lake.

Sterling
Reuters
Sterling

Sterling nje Rashford Ndani

Uingereza wamefanya mabadiliko yao ya kwanza.

Tunisia hawapitiki: Bado Tunisia 1-1 Uingereza

Nahodha wao ni mfungaji lakini hata hivyo, mabeki wa Tunisia wakiongozwa na Syam Ben Youssef wamewazima washambulizi wa Uingereza.

Ni wawakilishi wa kwanza wa Afrika waliofunga bao kwenye kombe la dunia mwaka huu.

Tusubiri. Ni mchuano wao wa kwanza tu!

Ashley Young na Syam Ben Youssef
Reuters
Ashley Young na Syam Ben Youssef

Dakika 60 za kwanza zimekatika. Tunisia 1-1 Uingereza

Wapi VAR?

Uingereza wauliza kwa nini teknolojia haikutumika kuona iwapo wangefaa kupewa penalti.

Harry Kane
Rex Features
Harry Kane sakafuni

Henderson hodari

Nyota wa Liverpool Jordan Henderson anaonekana kutawala eneo la kati katika mchuano huu.

Jordan Henderson
Getty Images
Jordan Henderson

Tunisia waafrika wa kwanza kuwafunga Uingereza tangu 1990

Ni mpinzani mmoja tu kutoka Afrika amewahi kufunga goli dhidi ya Uingereza.

Kabla ya mechi ya leo, Roger Milla wa Cameroon ndiye aliweza kuweka historia wakati Uingereza ilipofungwa bao na timu kutoka Afrika.

Uingereza imecheza dhidi ya timu ya Afrika kombe la dunia mara 6.

Mchuano huo ulipigwa 1990 na ulimalizika kwa ushindi upande wa Uingereza 3-2.

Bahati haijasimama Uingereza

Wamerejea kipindi cha pili wakijitahidi kusaka goli la ushindi.

View more on twitter

Awamu ya pili: Tunisia 1-1 Uingereza

Tunisia 1-1 England

Kipindi cha pili

Kipindi cha kwanza: Tunisia 1-1 Uingereza

Mechi imeingia mapumzikoni.

stones
Reuters
Stones wa Uingereza
Ferjani Sassi Tunisia
Getty Images
Ferjani Sassi wa Tunia

Tunisia 1-1 England

Kipindi cha kwanza cha mechi chakamilika

Penalti ya kwanza tangu 1998.

Tangu kombe la dunia 1998 - bao la Ferjani Sassi ndio mkwaju wa kwanza kufungwa dhidi ya Uingereza katika muda wa kawaida.

World Cup since June 1998

Mara ya mwisho walifungwa na mchezaji wa Argentina Gabriel Batistuta mnamo Juni 1998.

Wachezaji wa Uingereza wanalalamika kuwa penalti hiyo haikustahili kutolewa.

Kipindi cha kwanza kinaelekea kumalizika na matumaini ya Tunisia yamerejea!

Uingereza
Reuters
Wachezaji wa Uingereza

Lingard akaribia kuipa goli Uingereza

Jesse Lingard amekosa nafasi ya kuipa Uingereza goli la pili na la uongozi.

Uingereza wamepewa kona.

Lingard
Reuters
Lingard

Penalti si Penalti?

Mjadala wa iwapo mkwaju huo ulistahili kupewa umezuka.

Tunisia imesawazisha baada ya kupata bao kupitia penalti.

Kyle Walker
Reuters
Kyle Walker

Refa wa Mchuano Tunisia V Uingereza

Refa kutoka Colombia Wilmar Roldan ndiye mwamuzi wa mchuano huu.

Tunisia 1-1 Uingereza

Ferjani Sassi ameirejesha Tunisia mechini kwa kufunga penalti.

Pickford amepiga mbizi bila mafanikio.

Kyle Walker amesababisha mkwaju huo baada ya kumuangusha Ben Youssef .

Penalti kwa Tunisia

Harry aweka Historia!

Harry Kane ameweka historia kwa kufunga goli lake la kwanza Kombe la dunia akishiriki Kombe hilo kwa mara ya kwanza!

Alan Shearer aliifungia Uingereza mechi yake ya kwanza Kombe la Dunia, dhidi ya Tunisia 1998.

Wote wamefunga mabao yao ya kwanza dhidi ya mpinzani sawa - Tunisia.

Kona kwa Tunisia

Harry Kane matumaini ya Uingereza?

Kipa Mouez Hassen alijaribu kuondoa hatari lakini Harry Kane hakuzubaa.

Goli lake limeipa Uingereza uongozi - na alama tatu kufikia sasa.

Nyota huyo wa Tottenham ametajwa kuwa tegemeo la Three lions.

Anatosha?

Harry Kane
Getty Images
Harry Kane

Elewa kuhusu Tunisia

 • Wanashiriki mara ya kwanza tangu 2006. Hawajavuka hatua ya makundi.
 • Hawajashinda mechi zao 11 za mwisho Kombe la Dunia tangu kuilaza Mexico 1978.
 • Kilikuwa kipute cha kwanza kushindwa na mwakilishi kutoka Afrika.
 • Wemamaliza mechi za kufuzu kombe la dunia bila kupoteza mechi.
 • Ni timu ya Africa inayoorodheshwa vyema katika orodha ya mataifa ya FIFA.
 • Ni Nambari 21 jedwali ya FIFA.

Tunisia na matatizo ya kuzuia goli

Mechi tayari ni 1-0 kwa Uingereza.

Goli la Harry Kane linamaanisha kuwa Tunisia wamekosa kufungwa goli mara moja tu - sare ya 0-0 dhidi ya Ujerumani Magharibi 1978.

Kane aipa Uingereza uongozi! Tunisia 0-1 Uingereza.

Mambo muhimu kuhusu Uingereza

 • Hawajawahi kufungwa na mpinzani kutoka Afrika katika dimba la dunia (Ushindi 3,Sare 3).
 • Wameongoza kundi lao mara tano - tangu kombe la dunia 2006.
 • Imefungwa tu magoli matatu kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia.
 • Kikosi kizima cha Uingereza kinacheza ligi ya Uingereza – Timu pekee.
 • Inashiriki kombe la dunia mara sita mfululizo.
 • Imevuka Zaidi ya robo fainali mara moja tu – 1990. Imeshinda 1966.
 • Hawajafunga zaidi ya goli moja katika mechi zake 9 zilizopita kombe la dunia.

Tunisia taabani

Uingereza yaanza kuilemea Tunisia lakini ni kona.

Ngoma imeanza. Tunisia 0-0 Uingereza