Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Wawakilishi wa Afrika Senegal na Misri wataingia uwanjani leo kwenye mechi za kundi H na Kundi A, kombe la dunia.
 2. Wapinzani wa Misri Urusi, wanaingia mechini kwa majivuno baada ya kuisambaratisha Saudi Arabia 5-0.
 3. Mchezaji wa Croatia akataa kuingia uwanjani kama nguvu mpya Kombe la Dunia
 4. Diego Maradona amuonya kocha 'kutorudi' Argentina iwapo wataondolewa Kombe la dunia
 5. Mwanafunzi anayefanana sana na Pogba atumiwa kumuigiza Uingereza

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Mechi za Jumatano 20/6/2018.

Siku ya Jumanne imeanza kwa mechi za kwanza za Kundi H na kumalizika kwa mechi za Kundi A.

Ratiba ya mechi siku ya Jumatano ni kama ifuatayo.

Itakuwa ni siku ya Ronaldo, Diego Costa, au Suarez?

KUNDI B:

Portugal V Morocco: Luzhniki Stadium, Moscow

KUNDI B:Iran V Spain:Kazan Arena, Kazan

KUNDI A:

Uruguay V Saudi Arabia: Rostov Arena, Rostov-on-Don

Cristiano Ronaldo
Getty Images
Cristiano Ronaldo

Nani atafuzu kutoka Kundi A?

Baada ya kuilaza Misri 3-1, Russia imekaribia kuingia hatua ya timu 16 za mwisho.

Ushindi wa Uruguay dhidi ya Saudi Arabia kesho inamaanisha Misri itaelekea nyumbani.

Wenyeji Russia na Uruguay watafuzu kwa hatua ya timu 16 za mwisho.

Hata iwapo Saudi Arabia itashinda, magoli ya Russia yanatosha kuiwezesha kufuzu.

Hali itasalia hivi hadi tu pale mambo yatakapobadilika mechi za mwisho za kundi hili.

Tazama jedwali kamili hapa.

Kundi A
BBC Sport
Kundi A

Mechi imekamilika: Russia 3-1 Misri

Machozi kwa Misri, furaha kwa Russia.

Ramadan Sobhi....

Chipukizi huyu ameubadili mchezo? Alistahili kuanza mechi?

Ramadan Sobhi
Rex Features
Ramadan Sobhi

Misri kuelekea Misri?

Baada ya kuiadhibu Saudi Arabia 5-0, sasa Russia imeidhalilisha Misri 3-1.

Misri imecheza Mechi 2, alama 0, goli 1.

Inamaanisha Misri watakuwa wawakilishi wa kwanza kufunga safari kuelekea nyumbani?

Wamesalia na mechi moja dhidi ya Saudi Arabia.

Muda wa kawaida unakaribia kumalizika. Kipindi cha pili kina katika pole pole.

Russia
Getty Images
Wachezaji wa Russia

Mohamed Salah aweka historia: Haitoshi kunusuru Misri

Mohamed Salah ni mchezaji wa tatu kuifungia Misri bao kombe la dunia.

Wengine ni:

 • Abdelrahman Fawzi (1934)
 • Magdy Abed El Ghani (1990)
Mohamed Salah
Getty Images
Mohamed Salah

Magoli kulingana na muda: Russia 3-1 Misri.

Magoli yalifungwa kulingana na muda:

 • Mchezaji wa Misri, Fathi alijifunga dakika ya (47) 1-0
 • Cheryshev akaongeza uongozi wa Russia dakika ya (59) 2-0
 • Dzyuba akafunga goli la tatu la Russia dakika ya (61) 3-0
 • Mohamed Salah akaifungia Misri penalti dakika ya (73) 3-1

Ronaldo wa Russia - Denis Cheryshev

Denis Cheryshev ana magoli sawa na Cristiano Ronaldo kombe la dunia.

Hajawahi kuifungia timu ya taifa goli kabla ya kombe la dunia.

Denis Cheryshev
Getty Images
Denis Cheryshev

Misri warejea Mechini! Mo Salah amefunga.

Russia 3-1 Misri

Misri wapewa Penalti.

Mo Salah ameangushwa ndani ya sanduku.

Russia yaisambaratisha Misri: 3-0

Artem Dzyuba amefunga bao la tatu la Russia dakika ya 62 na kuzidisha uongozi wa wenyeji hao wa Kombe la dunia.

Awali Denis Cheryshev alifunga goli la pili la Russia kwenye mechi na lake la tatu kombe la dunia.

Magoli hayo yamevunja nyoyo za mashabiki wa Misri.

Artem Dzyuba
Getty Images
Artem Dzyuba akifunga

Russia 3-0 Misri

Goli: Russia 2-0 Misri

Matumaini yote kwa Mo Salah

Misri inahitaji kufunga goli.

La sivyo, italazimika kuitegemea Saudi Arabia kufunga Uruguay.

View more on twitter

Goli la kujifunga laumiza tena Afrika.

Nahodha wa Misri Ahmed Fathi amejifunga na kufikisha magoli ya kujifunga kutoka timu za Afrika hadi 2.

Awali mchezaji Aziz Bouhaddouz wa Morocco alijifunga dhidi ya Iran mechi ya kwanza.

Kwa sasa Russia inaongoza kupitia goli hilo la kujifunga.

Russia 1-0 Misri: Misri wamejifunga!

Kipindi cha pili kimeanza: Russia 0-0 Misri

Nani ameshambulia zaidi?

Russia imelenga goli la Misri mara nane na kufanikiwa na mkwaju mmoja wa beki Sergei Ignashevich.

Misri imeandikisha majaribio matano kwenye goli la Russia.

Kipa wa Misri Mohamed El-Shenawy ndiye mchezaji wa Misri mwenye mchango mkubwa mechini.

Kipa Mkongwe wa Misri mwenye umri wa miaka 45 Essam El Hadary atalazimika kusubiri hadi mechi ijayo kabla ya kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kushiriki Kombe la dunia.

Matumaini ya Misri yamesalia kwenye kipindi hiki cha pili kuona iwapo watapata alama muhimu za kuwadumisha kwenye dimba la dunia mwaka huu.

Kundi la ut-A-ni?

Je, unafahamu orodha za timu za Kundi A kwenye jedwali ya FIFA kwa timu za taifa?

 • Russia 70
 • Saudi Arabia 67
 • Misri 45
 • Uruguay 14

Kufikia sasa Russia inaongoza kundi hilo, ikifuatwa na Uruguay baada ya kushinda mechi zao za kwanza.

Nje ya Kombe la dunia......Arsenal yamsaini kipa wa Ujerumani

Klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen imetoa tangazo rasmi juu ya uhamisho wa kipa huyo.

View more on twitter

Kipindi cha Kwanza: Russia 0-0 Misri

Kona kwa Russia

Salah acheza kwa tahadhari?

Jeraha la kitambo la bega linalaumiwa kuwa chanzo cha kimya cha Mo Salah.

Ama ni beki wa Russia Yuri Zhirkov amemkomesha?

Mo Salah
Getty Images
Mo Salah na Yuri Zhirkov

Liverpool yafurahia kurejea kwa Mo Salah

Mechi yake ya mwisho kucheza, aliiwakilisha Liverpool - fainali ya Champions League.

Alijeruhiwa na Sergio Ramos na kukaribia kukosa Kombe la dunia.

View more on twitter

Yuko wapi Denis Cheryshev?

Mshambulizi huyu wa Russia anawania tuzo ya mfungaji bora kombe la dunia 2018.

Kufikia sasa amefunga mabao 2 - dhidi ya Saudi Arabia.

Cristiano Ronaldo anaongoza jedwali hilo akiwa na mabao 3.

Denis Cheryshev
Getty Images
Denis Cheryshev wa Russia

Russia: Misri si Saudi Arabia

Wenyeji Russia waliidunisha Saudi Arabia kwenye mechi ya ufunguzi kwa kuifunga 5-0.

Lakini inaonekana Russia wameshuhudia upungufu wa mawazo dhidi ya Misri.

Ahmed Hegazi anaonekana kuwanyamazisha wafungaji wa Russia.

Mchuano unakaribia dakika 30 za kwanza, lakini Misri wanatoshana na Russia - licha ya kuwa ugenini.

Bado mapema?

Russia
Reuters
Wang'ang'ania mpira

Kipindi cha kwanza: Russia 0-0 Misri

Kipindi cha kwanza kipute cha mzunguko wa pili kundi A ugani St. Petersburg.

Wenyeji Russia na wawakilishi wa Afrika Misri hawajafungana.

Russia
BBC Sport
Russia V Misri

Messi wa Misri Mo Salah kuwa kama Messi wa Argentina?

Mchuano umekatika dakika 10 lakini bado Mo Salah hajawa tishio kwa Russia.

Kushiriki kwake mechini ulionekana kuwa utaisaidia Misri kuinyuka Russia.

Huenda bado ni mapema kubashiri?

Mohamed Salah
Reuters
Mohamed Salah

Mo Salah suluhisho?

Mshambulizi wa Misri, Mo Salah ameanza mechi licha ya kukosa mchuano wa kwanza wa Misri.

Misri ilifungwa 1-0 na Uruguay mechi yake ya kwanza.

Mo Salah
Getty Images
Mo Salah

Russia 0-0 Misri

Timu zote ndizo hizi.

Russia
BBC Sport
Kikosi cha Russia
Misri
BBC Sport
Kikosi cha Misri

Baada ya Senegal, sasa ndoto za Afrika zasalia na Misri

Wenyeji Russia wanachuana na Misri.

Sherehe zasheheni Senegal

Baada ya ushindi, sasa ni sherehe kila kona ya Afrika.

View more on twitter

Sifa kwa Senegal.

Ushindi wa kwanza wa Afrika Kombe la dunia 2018....

Alama 3 za kwanza kwa timu ya Afrika Kombe la dunia 2018....

Timu pekee ya Afrika kutofungwa mechi za makundi kombe la dunia....

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Mechi imekamilika! Poland 1-2 Senegal!

Senegal yashikilia uongozi.

Poland hawaamini!

Dakika 4 zimeongezwa lakini Senegal bado inaongoza.

Poland 1-2 Senegal!

Poland
EPA
Mchezaji wa Poland

Poland wamepata bao. Poland 1-2 Senegal.

Robert Lewandowski amelemewa....

Kwa wengine ni mkali, lakini mabeki wa Senegal wamemzima Robert Lewandowski.

Robert Lewandowski
Getty Images
Robert Lewandowski

Demba Ba ashiriki sherehe za Senegal

Mfungaji wa zamani wa Chelsea na Senegal, Demba Ba..........

View more on twitter

Poland na Senegal wafanya mabadiliko.

Mabadiliko kwa Poland: Arkadiusz Milik amempisha Dawid Kownacki.

Senegal imemuondoa mfungaji Mbaye Niang na nafasi yake kuchukuliwa na Moussa Konate.