Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Msimamo: Kundi B

  Baada ya juhudi za timu zote, hivi ndivyo Kundi B ilivyo.

  Kombe la dunia
  Image caption: Msimamo Kundi B
 2. Ratiba Kombe la Dunia: Siku ya Alhamisi

  Mechi ya Kundi C: Denmark V Australia

  Mechi ya Kundi C: Ufaransa V Peru

  Mechi ya Kundi D: Argentina V Croatia

 3. De Gea aponea

  Kwa mara ya kwanza kombe hili, De Gea amemaliza mechi bila kufungwa bao.

  Alishtumiwa kwa kosa lake dhidi ya Ureno baada ya kutozuia bao la Ronaldo.

  De Gea
  Image caption: De Gea
 4. Siku ya uhaba wa magoli...na majonzi

  Siku zinapokwenda, Kombe nalo linaonekana kuwa ngumu zaidi.

  Mechi zote zilizochezwa siku ya Jumatano, zimeshuhudia goli moja kila mechi.

  • Uhispania imefunga Iran 1-0.
  • Uruguay imeilaza Saudi Arabia 1-0.
  • Portugal ilishinda Morocco 1-0.

  Licha ya kuwa goli moja, mabao hayo yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa kila timu.

  Baada ya ushindi dhidi ya Morocco na Iran, Uhispania na Portugal wanashikilia nafasi ya kwanza kundi B.

  Kila mmoja ana alama 4.

  Ushindi wa awali wa Uruguay umeipa tiketi ya kushiriki hatua ijayo ya timu 16 bora.

  Saudi Arabia na Morocco wameanza kufunga safari kuelekea mataifa yao.

 5. Vahid Amiri - aliyemdhalilisha Pique

  Mchezaji wa Iran aliyeupitisha mpira katikati ya miguu ya Pique. Imekuwa mojawapo ya burudani Kombe hili.

  Vahid Amiri
  Image caption: Vahid Amiri
 6. Matokeo: Iran 0-1 Uhispania

  Matokeo
  Image caption: Matokeo
 7. Dakika 4 zimeongezwa

  Iran 0-1 Uhispania

 8. 90 zimekamilika. Iran 0-1 Uhispania

  Tunaingia muda wa ziada....

 9. Bao walilozuia Iran

  Liwe liwalo, haliwi goli

  Iran
  Image caption: Iran langoni
 10. Dakika za Iran.....

  Iran imefunga magoli yake matatu ya mwisho Kombe la dunia ndani ya dakika 15 za mwisho.

 11. Vahid Amiri alishwa kadi ya njano

  Mchezaji wa Iran asajiliwa kwenye kitabu cha refa..

 12. Mkwaju unazuiwa.

  Mpira umerejea ngome ya Uhispania

 13. Frikiki kwa Uhispania

 14. Kwa nini bao la Iran lilikataliwa...VAR imetumika

  Mchezaji Saeid Ezatolahi wa Iran amepatikana ameotoa.

  Bao la kuotewa haliruhusiwi!

  Zimesalia chini ya dakika 20 mechi kumalizika.

  Uhispania inazidi kuongoza.

  Iran
  Image caption: Iran ilivyootea
 15. Miili kwenye mstari

  Wachezaji wa Iran wanafanya kila wawezalo kuzuia bao la pili.

 16. Diego Goal-sta

  Diego Costa amefunga goli lake la tatu Russia, kutoka kombora lake la tatu tu!

  Ni Ronaldo tu anamzidi kwenye orodha ya wafungji bora Kombe la dunia mwaka huu.

  Diego Costa
  Image caption: Diego Costa
 17. Bao linaonekana kuwa na utata...tusubiri

 18. Iran imesawazisha...bao limekataliwa

 19. Unakubaliana na ubashiri huu?

  Uhispania tayari imepata goli la kwanza.

  Iran 0-1 Uhispania.

  Uhispania
  Image caption: Shabiki wa Uhispania
 20. Benchi ya Uhispania:

  • 4 Nacho
  • 7 Saúl
  • 8 Koke
  • 9 Rodrigo
  • 10 Thiago Alcántara
  • 12 Odriozola
  • 13 Arrizabalaga
  • 14 Azpilicueta
  • 16 Monreal
  • 17 Iago Aspas
  • 20 Asensio
  • 23 Reina