Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Nigeria wamewashinda Iceland 2-0, mabao yao wakifungiwa na Ahmed Musa.
  2. Brazil wamewalaza Costa Rica 2-0, mabao yakifungwa na Countinho na Neymar.
  3. Uswizi wamewachapa Serbia 2-1
  4. Imewahi kupoteza dhidi ya Costa Rica, mechi ya kirafiki Machi 1960.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Siku ya Xherdan Shaqiri, Sherehe za Nigeria na Neymar!

Serbia 1-2 Uswizi

Mkombozi wa Uswizi Xherdan Shaqiri.....Wa Nigeria....Ahmed Musa....na Wa Samba boys ni Neymar!

Ingawa klabu yake ya Stoke City imelishwa upanga, haijamzuia Xherdan Shaqiri kunawiri Russia 2018.

Mbona ukose kuwa nasi kesho?

KUNDI G: Belgium V Tunisia: uga wa Spartak: Moscow

KUNDI F: Jamhuri ya Korea V Mexico: Rostov Arena - Rostov-On-Don

KUNDI F: Ujerumani V Sweden: Uwanja wa Fisht

....Kutoka meza ya BBC Kombe la Dunia, shukran kwa kuwa nasi leo.

Tunawatakia wikendi njema.......!

Xherdan Shaqiri
Reuters
Xherdan Shaqiri
Nigeria
BBC Sport
Musa na Ihe-anacho
Neymar
Rex Features
Neymar

Ushindi Uswizi!

Mechi imekamilika: Serbia 1-2 Uswizi

Ni alama 3 muhimu kwa Uswizi...na tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa Xherdan Shaqiri!

...........Mabao

  • Granit Xhaka dakika ya 53
  • Xherdan Shaqiri dakika ya 90+
  • Serbia ilitangulia dakika ya 5 kupitia Aleksandar Mitrovic

Lakini kazi ipo Uswizi.......

Uswizi watafuzu iwapo wataandikisha ushindi dhidi ya Costa Rica.

Serbia nayo itafuzu hatua ya muondoano ikiilaza Brazil.

Kundi E Kufikia sasa..............

Brazil alama 4.

Uswizi alama 4

Serbia alama 3.

Costa Rica alama 0

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Dakika 4 zimeongezwa.

93' Serbia 1-2 Uswizi

Goooooli! Uswizi wapata bao!

Serbia 1-2 Uswizi

Shaqiri aifungia Uswizi.

Uswizi wamepanda hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 4.

Kona kwa Serbia.

86' Serbia 1-1 Uswizi

Xhistoria!

84' Serbia 1-1 Uswizi

Granit Xhaka ni mchezaji wa tatu wa Uswizi kufunga goli zaidi ya Kombe moja la Dunia.

Wengine ni: Jacques Fatton na Andre Abegglen.

Mabadiliko Serbia

82' Serbia 1-1 Uswizi

Mbinu za kusaka bao la ushindi zaongezeka Serbia.

Radonjic ameingia nafasi yake Milivojevic.

Ni Soka au Miereka?

74' Serbia 1-1 Uswizi

Aleksandar Mitrovic amechezewa visivyo na Fabian Schar pamoja na nahodha Stephen Lichtsteiner!

....Lakini Serbia haipati penalti!

Mabadiliko Uswizi: Breel Embolo ameingia nafasi yake Blerim Dzemaili,

Mitrovic
EPA
Mitrovic amwuliza refa Felix Brych

Xhaka hatarini kwa alivyosherekea?

69' Serbia 1-1 Uswizi

Kuna madai kuwa Granit Xhaka alifanya ishara kutumia mikono yake kuashiria hisia za kisiasa!

.....tutajua zaidi baada ya mechi..!

Xhaka
Getty Images
Xhaka

Xhaka awaka!

62' Serbia 1-1 Uswizi

Kiungo huyo wa Arsenal ameachilia shuti kutoka yadi 25 na kupata bao lake la kwanza Kombe la Dunia.

Bao hilo limehuisha matumaini ya Uswizi Kombe la Dunia.

Xhaka
Getty Images
Xhaka

Uswizi watoka nyuma mechi ya pili!

Serbia 1-1 Uswizi

Granit Xhaka ameifungia Uswizi dakika ya 53.

Kwa mara ya pili Kombe hili, Uswizi wamepata bao la kusawazisha licha ya kuwa wa kwanza kufungwa.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Uswizi wasawazisha

53' Serbia 1-1 Uswizi

Boom Xhaka Xhaka!

Alhamdulillah: Ahmed Musa!

Nigeria 2-0 Iceland

.....Mfungaji Musa amekata kimya......tazama alichoandika!

View more on twitter

Nini inafuata Nigeria?

Nigeria 2-0 Iceland

Imekuwa faraja kukuletea mechi ya Nigeria V Iceland.....

Kumbuka...

Ahmed Musa anahitaji mabao matatu kuwa mfungaji bora wa Afrika Kombe la Dunia.

  • Asamoah Gyan(Ghana): Mabao 6.
  • Roger Milla (Cameroon): Mabao 5.

Tupe hisia zako kwenye Facebook na Twitter.

Usisahau...........Jumanne ijayo itakuwa ni ya kuvutia.....

Nigeria itakwaruzana na Argentina

na....

Iceland itaonana na Croatia.

Hata hivyo...Usibanduke

Zidi kuwa nasi mechi yetu ya mwisho leo, Serbia ikiiongoza Uswizi hadi sasa!

Shukran kwako pia kwa kuwa nasi kwenye michuano yote....

Nigeria
Reuters
Wachezaji wa Nigeria wakisherekea

Serbia - Njano

Kipindi cha Kwanza: Serbia 1-0 Uswizi

Kufikia sasa wachezaji watatu wa Serbia wamelishwa kadi kwenye mechi ya Kundi E.

Matic amwumiza Lichtsteiner: Kadi ya Njano

Milinkovic-Savic amkwaruza Schar: Kadi ya Njano

Luka Milivojevic: Kadi ya Njano

Kwa nini kiatu cha Shaqiri kimezua mjadala?

47' Serbia 1-0 Uswizi

Mshambulizi wa Uswizi Shaqiri amechapisha bendera ya Kosovo kwenye kiatu chake.

Eneo hilo la Kosovo limekuwa na mvutano kwa muda lakini, Mashirikisho ya soka, FIFA and UEFA yameitambua Kuwa huru Mei 2016. Serbia haijafurahia uamuzi huo.

Xhaka na Shaqiri wametaka kuliwakilisha Kosovo, lakini FIFA imekataa.

Usishangae mchuano huo ukikumbwa na hisia nyingi na hasira.

Shaqiri
Getty Images
Shaqiri

Acheza kwa shauku Shaqiri

Serbia 1-0 Uswizi

Xherdan Shaqiri na mwenzake Steven Zuber wawasumbua mabeki wa Serbia.

Shaqiri
EPA
Shaqiri

Serbia bado mbele

25' Serbia 1-0 Uswizi

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Dimba la mabao...2018

23' Uswizi 0-1 Serbia

Kombe la Dunia Russia 2018 limeshuhudia goli kila mechi.....

Hii inamaanisha........

Kwa mara ya kwanza sawa na Uswizi 1954, bao limefungwa kila mechi Kome la Dunia mwaka huu.

Wakati huo, mechi 26 zilishuhudia goli......

Ushindi wa pili Serbia wanukia?

16' Uswizi 0-1 Serbia

Bonge la pasi kutoka Dusan Tadic ...kichwa cha Aleksandar Mitrovic..hadi kwenye lango

Mitrovic
Getty Images
Mitrovic

GOLI: Mitrovic aiweka Serbia mbele

11' Uswizi 0-1 Serbia

Aleksandar Mitrović amefunga goli dakika ya 5.

Kipindi cha Kwanza

Uswizi 0-0 Serbia

Moja kwa moja kutoka Uwanja wa Kaliningrad, Kaliningrad.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Kikosi cha Switzerland

Serbia 0-0 Switzerland

Uswizi wamedumisha timu iliyotoka sare dhidi ya Brazil.

Wachezaji wa Arsenal Granit Xhaka na Stephan Lichtsteiner waanza mechi.

Uswizi.

Sommer, Lichtsteiner, Schar, Akanji, Rodriguez, Behrami, Xhaka, Shaqiri, Dzemaili, Zuber, Seferovic.

Wachezaji wa akiba.

Mvogo, Moubandje, Elvedi, Lang, Embolo, Freuler, Fernandes, Zakaria, Gavranovic, Drmic, Djourou, Burki.

Switzerland
BBC Sport
Uswizi

Kikosi cha Serbia

Serbia 0-0 Switzerland

Kocha Mladen Krstajic amefanya ukarabati kwenye kikosi kilichoshinda dhidi ya Costa Rica.

Winga Adem Ljajic amempisha Filip Kostic.

Beki wa zamani wa Chelsea Branislav Ivanovic anashiriki mechi yake ya 105 timu ya taifa.

Safu ya Serbia:

Stojkovic, Ivanovic, Milenkovic, Tosic, Kolarov, Matic, Milivojevic, Tadic, Milinkovic-Savic, Kostic, Mitrovic.

Benchi:

Rajkovic, Rukavina, Spajic, Zivkovic, Prijovic, Veljkovic, Rodic, Grujic, Radonjic, Jovic, Ljajic, Dmitrovic.

Serbia
BBC Sport
Serbia

Serbia v Switzerland

Serbia 0-0 Switzerland

Tunaingia mechi ya mwisho siku ya Ijumaa...............

Ahmed Musa: Nigeria yasema Alhamdulilah

Nigeria 2-0 Iceland

Kutoka Daresalam hadi Durban, Lagos hadi Luanda ushindi wa Nigeria wazidi kushangiliwa.

Francis Uzoho
Getty Images
Kipa Francis Uzoho akisherekea

Nigeria 2-0 Iceland

Nigeria 2-0 Iceland

22/6/2018

Siku ya Ijumaa isiyowahi kusahaulika.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo
View more on twitter

Beki aliyeibadilisha Nigeria

Nigeria 2-0 Iceland

Beki Kenneth Omeruo wa Chelsea ameleta mabadiliko kwenye ngome ya Nigeria.

Super Eagles wamemaliza mechi bila kufungwa.

Musa azima ndoto za Iceland.

Mechi imekamilika: Nigeria 2-0 Iceland

Ulaya mboga kwa Nigeria

94' Nigeria 2-0 Iceland

Ni ushindi 6 kwenye mechi 6 dhidi ya timu kutoka bara Ulaya katika Kombe la Dunia

Iwobi ameingia

93' Nigeria 2-0 Iceland

Kiungo wa Arsenal Alex Iwobi amepata dakika za kushiriki mechi, nafasi ya Oghenekaro Etebo.

Njooni tusherekee: Nigeria

90' Nigeria 2-0 Iceland

Mabao ya Ahmed yanaonekana kuzidisha nafasi ya Nigeria kufuzu kwa hatua ya muondoano.

Nigeria inahitaji pointi moja tu dhidi ya mchuano wao ujao dhii ya Argentina.

Ahmed Musa
AFP
Ahmed Musa

Hatari Iceland....

88' Nigeria 2-0 Iceland

Kipa Francis Odinaka Uzoho apangua!

Mabadiliko Nigeria

86' Nigeria 2-0 Iceland

Mshambulizi Ighalo ameingia nafasi ya mwenzake Iheanacho!

Penalti tena...Iceland wapoteza

83' Nigeria 2-0 Iceland

Gylfi Sigurdsson amepaisha penalti waliopewa!

Mikwaju 12 imetolewa, 6 kwa matumizi ya VAR kwenye Dimba hili.

Penalti kwa Iceland

Nigeria 2-0 Iceland

Mtambo wa VAR umetumika kufanya uamuzi huo.

Musa tena

80' Nigeria 2-0 Iceland

Ahmed Musa amemuacha kipa wa Iceland akiwa sakafuni na kuiongezea Nigeria bao la pili.

Bao hilo limeizamisha Iceland.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Musaaa......la pili kwa Nigeria

Nigeria 2-0 Iceland

Ahmed Musa aweka rekodi

68' Nigeria 1-0 Iceland

Mabadiliko Iceland

66' Nigeria 1-0 Iceland

Kiungo wa Iceland Ragnar Sigurdsson ametolewa baada ya kuzidiwa na maumivu.

Nafasi yake imechukuliwa na Sverrir Ingason.

Ragnar Sigurdsson
Getty Images
Ragnar Sigurdsson