Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Ujerumani wamewashinda Sweden 2-1 kwa bao la dakika za mwisho (90+5) lililofungwa na Toni Kroos
 2. Sweden walikuwa wametangulia kufunga kupitia Ola Toivonen dakika ya 32
 3. Ubelgiji walishinda 5-2 dhidi ya Tunisia, kwenye mechi ambayo ilishuhudia ufungaji wa mabao mengi kipindi cha kwanza
 4. Lukaku alifunga mabao mawili, na sasa ana jumla ya mabao manne, sawa na Ronaldo
 5. Mechi ya Ubelgiji na TunBao la kwanza lilifungwa na Eden Hazard kupitia penalti dakika ya 6, Lukaku akafunga (16' , 45'+3). Hazard akaongeza lake la pili dakika ya 51. Batshuayi akafunga dakika ya 90.
 6. Tunisia walifungiwa na Bronn dakika ya 18 lakini akaumia na kuondolewa uwanjani kwa machela dakika chache baadaye
 7. Carlos Vela aliwafungia Mexico dhidi ya Korea Kusini kupitia penalti dakika ya 25, Javier Hernandez (Chicharito) naye akafunga kipindi cha pili. Korea Kusini walikomboa moja dakika za mwisho.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Ujerumani wafufua matumaini kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Sweden, Ubelgiji 5-2 Tunisia, Mexico 2-1 Korea Kusini

Toni Kroos akisherehekea kufunga
AFP
Toni Kroos akisherehekea kufunga

Ujerumani wamefufua matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya muondoano Kombe la Dunia Urusi baada ya kuwashinda Sweden 2-1 kupitia bao la dakika za mwisho lililofungwa na Toni Kroos.

Sweden walitangulia kufunga dakika ya 32 kupitia Ola Toivonen lakini Marco Reus akawasawazishia Ujerumani dakika ya 48.

Ubelgiji awali waliwalaza Tunisia 5-2.

Katika mechi hiyo ya Ujerumani, Jerome Boateng alioneshwa kadi ya pili ya manjano ya kufukuzwa uwanjani.

Ujerumani hata hivyo watasubiri hadi siku ya mwisho kufahamu iwapo watafika hatua ya 16 bora, kwani wana alama sawa sasa na Sweden.

Sweden watacheza na Mexico siku ya mwisho nao Ujerumani wacheze na Korea Kusini.

Kwa sasa, mambo yako hivi kwenye kundi:

Kundi
BBC

Pata taswira halisi ya mambo yalivyo makundi mbalimbali hapa:

Kombe la dunia la FIFA 2018 - Mpangilio na matokeo

Awali, Ubelgiji walishinda 5-2 dhidi ya Tunisia, ambapo Lukaku na Hazard walifunga mabao mawili kila mmoja.

Soma zaidi hapa: Belgium 5-2 Tunisia: Lukaku awafikia Cristiano Ronaldo na Diego Maradona

Mechi yamalizika: Ujerumani 2-1 Sweden

Habari za hivi pundeUjerumani wafunga!

Toni Kroos awafungia Ujerumani bado ambalo huenda likawa la kuwashindia mechi.

Amelifunga dakika ya 90+5

Fursa ya mwisho?

Ujerumani wamepata frikiki karibu na eneo la hatari. Watafunga?

Ujerumani wagongwa mwamba wa goli

Dakika tano za ziada

Ujerumani washambulia kwa ukali, lakini wapi

Kipa wa Sweden ameokoa mpira wa kichwa wa Mario Gomez. Sweden wamefanikiwa kuzima mashambulio ya Ujerumani.

Neuer awaokoa Ujerumani mara mbili

Boateng apewa kadi nyekundu

Dakika ya 82

Jerome Boateng amepewa kadi ya pili ya manjano na kulazimika kuondoka uwanjani. Amekuwa muhimu sana safu ya ulinzi ya Ujerumani.

Kadi ya kwanza ya manjano yatolewa

Albin Ekdal amepewa kadi ya njano kwa kucheza visivyo

Muller akaribia kufunga kwa kichwa

Muller amekaribia kufunga kwa kichwa, lakini mpira wake ukatikisa wavu kutoka nje.

Habari za hivi pundeUjerumani wasawazisha kupitia Marco Reus

Ujerumani 1-1 Sweden (Dakika ya 48)

Marco Reus amewasawazishia Ujerumani ambao wamerejea kwa kishindo, wakishambulia vikali sawa na walivyoanza mechi.

Kipindi cha pili kimeanza

Mario Gomez ameingia nafasi ya Julian Draxler

Ni wakati wa mapumziko sasa

Kipindi cha kwanza kimemalizika. Unafikiri Joachim Low na wachezaji wake wanasema nini?

Neuer awaepusha Ujerumani aibu

Ujerumani 0-1 Sweden

Manuel Neuer amefanya kazi ya ziada kuzuia Sweden kufunga bao la pili kupitia frikiki.

Ujerumani hatarini!

Ujerumani walishindwa mechi yao ya kwanza 1-0 na Mexico. Kwa sasa, Mexico wana alama sita baada ya kuwashinda Korea Kusini 2-1 mapema leo.

Sweden waliwashinda Korea Kusini mechi ya kwanza.

Sweden wakishinda leo watakuwa na alama sita sawa na Mexico.

Mara ya mwisho Ujerumani kuyaaga mashindano ya Kombe la Dunia bila kufika hatua ya muondoano ilikuwa ni mwaka 1938.

Habari za hivi pundeBaoooo! Ujerumani 0-1 Sweden

Germany 0-1 Sweden (Dakika ya 32)

Ola Toivonen awafungia Sweden baada ya makosa safu ya ulinzi ya Ujerumani. Manuel Neuer alikuwa ameshatoka kwenye lango kwenda kudaka mpira.

Sweden zaidi wanategemea kujibu mashambulizi, ingawa wameimarika kadiri mechi ilivyosonga.

Sweden wataka penalti

Sweden wamejibu shambulio tena, lakini Marcus Berg akakabwa na Jerome Boateng kutoka nyuma. Wametaka penalti lakini mwamuzi amekataa hilo.

Manuel Neuer alikuwa tayari ametokea na akauzuia mpira.

Ujerumani wameanza kwa mashambulizi

Dakika ya 10

Ujerumani wameanza mechi kwa kukita kambi eneo la hatari la Sweden, wamepata nafasi kadha nzuri za kufunga lakini bahati yao haijasimama.

Sweden wamepata nafasi moja kupitia kujibu mashambulizi lakini zaidi wanaonekana kuangazia kujilinda.

Ujerumani
Reuters

Mechi imeanza: Ujerumani v Sweden

Ujerumani wataathiriwa na 'laana ya mabingwa watetezi' na kushindwa kufuzu kwa hatua ya muondoano?

Ujerumani v Sweden

Mabingwa watetezi Ujerumani wanakutana na Sweden Kombe la Dunia, mechi ambayo itaanza saa tatu saa za Afrika Mashariki.

Wachezaji watakaoanza mechi wametangazwa, badiliko kuu kwa Ujerumani ikiwa ni kuondolewa kwa Mesut Ozil safu ya kati na badala yake kuwekwa Marco Reus.

Ujerumani walishindwa 1-0 na Mexico mechi yao ya kwanza.

Ujerumani
BBC Sport
Sweden
BBC Sport

Mechi yamalizika Korea Kusini 1-2 Mexico

Korea Kusini 1-2 Mexico

Korea Mexico
BBC

Habari za hivi pundeKorea Kusini wajipatia bao!

Korea Kusini 1-2 Mexico (Dakika ya 90+2)

Son Heung-min amewapatia Korea Kusini bao muda wa kuongezwa.

Habari za hivi pundeChicharito awafungia Mexico la pili

Korea Kusini 0-2 Mexico (Dakika ya 65)

Javier Hernandez maarufu kama Chicharito amewafungia Mexico bao la pili.

Alifunga bao pia siku kama ya leo pia Kombe la Dunia 2014.

Ni wakati wa mapumziko: Korea Kusini 0-1 Mexico

Ni wakati wa mapumziko sasa, Korea Kusini wameimarika kiasi tangu walipofungwa lakini bado hawajafanikiwa kufunga.

Son Heung-min anavuma sana, ambapo anasaidiana na Lee Yong.

Habari za hivi pundeMexico wafunga kupitia penalti

Korea Kusini 0-1 Mexico (Dakika ya 25)

Carlos Vela amewafungia Mexico Penalti.

Andres Guardado alikuwa ameshambulia na alipoupiga mpira beki wa Korea Kusini anayechezea FC Tokyo Jang Hyun-soo akafika kumkaba kwa kuteleza lakini akaunawa mpira.

Ndiyo penalti ya 14 kupigwa katika michuano ya sasa.

Sababu ya wachezaji wa Korea Kusini kupiga saluti

Korea Kusini 0-0 Mexico (Dakika ya 20)

Wachezaji watatu wa timu ya taifa ya Korea Kusini wamepiga saluti wimbo wa taifa ulipokuwa unaimbwa kabla ya mechi hii kuanza.

Mabeki Hong Chul, Kim Min-woo na kiungo wa kati Ju Se-jong wamelazimika kufanya hivyo kwa sababu bado wanalitumikia jeshi.

Ni sheria nchini humo kwamba mchezaji yeyote ni lazima awe analitumikia jeshi la taifa hilo kwa lazima kabla ya kutimiza miaka 28, isipokuwa tu akifanikiwa akichezea timu hiyo.

Korea Kusini bado hawajashinda mechi hata moja katika mechi saba walizocheza karibuni zaidi Kombe la Dunia.

Wametoka sare mechi mbili na kushindwa tano. Wameshindwa mechi tatu walizocheza karibuni zaidi.

Aidha, wameshinda kuzuia kufungwa katika mechi 12 kati ya 13 walizocheza karibuni Kombe la Dunia.

Wamefungwa kila mechi kati ya mechi saba walizocheza karibuni zaidi.

Walishindwa 1-0 na Sweden mechi yao ya kwanza michuano ya sasa ya Urusi. Mexico waliwashinda Ujerumani 1-0 mechi ya kwanza.

Mashabiki wa Mexico kwa kujipamba, wacha tu...

Mashabiki wa Mexico wamejitokeza wakiwa wamejipamba kwa kila aina.

Hebu jionee mwenyewe:

Shabiki
Getty Images
Shabiki
Getty Images
Shabiki
Getty Images

Korea Kusini v Mexico, mechi imeanza

Mechi kati ya Korea Kusini na Mexico - waliowashangaza mabingwa watetezi Ujerumani, imeanza mjini Rostov-on-Don.

Karibu robo tatu ya mashabiki wamevalia jezi za Mexico.

Mexico
BBC Sport
Korea Kusini
BBC Sport

Mechi yamalizika: Belgium 5-2 Tunisia

Mpira sasa umekwisha. Ubelgiji 5-2 Tunisia.

Habari za hivi pundeTunisia wakomboa moja

Tunisia wameonesha bado hawajaishiwa na risasi, wamekomboa bao moja dakika za mwisho.

Habari za hivi pundeHatimaye! Batshuayi afunga

Ubelgiji 5-1 Tunisia (Dakika ya 90)

Hata kabla hatujamaliza, Batshuayi amefunga bao lake la kwanza Kombe la Dunia. Sasa mambo ni 5-1.

Batshuayi bahati bado haijasimama

Ubelgiji 4-1 Tunisia (Dakika ya 90)

Michy Batshuayi ameendelea kupata nafasi nzuri za kufunga, wakati mmoja ameugonga mwamba wa goli mpira ukarudi ndani ya uwanja, alipojaribu mara ya pili ukapinduliwa na mpinzani na kutoka nje.

Bahati yake bado haijasimama.

Mfungaji bora wa mabao atakuwa nani?

Romelu Lukaku wa Ubelgiji na Cristiano Ronaldo wa Ureno kwa sasa wanashikilia nafasi ya kufunga mabao mengi Kombe la Dunia michuano ya sasa, wote wana mabao manne.

Denis Cherryshev wa urusi na Diego Costa wa Uhispania kila mmoja ana mabao matatu sasa.

Lionel Messi anaongoza kwa kushambulia doli zaidi, mara 12.

Lakini mabao ya kujifunga bado ndiyo mengi, matano kufikia sasa.

Soma zaidi: Anayeongoza ufungaji wa mabao Kombe la Dunia

Batshuayi akaribia kufunga, lakini bado

Michy Batshuayi amembwaga kipa na kuelekeza mpira kwenye lango, lakini kuna mchezaji wa Tunisia alikuwa amekimbia langoni na akazuia mpira kutumbukia ndani.

Michy
AFP

Mambo yalivyo Kundi G kufikia sasa

Ubelgiji 4-1 Tunisia (Dakika ya 75)

Tunisia na Ubelgiji bado watasubiri matokeo mechi kati ya England na Panama kubaini iwapo wamesonga hatua ya 16 kwa Belgium na kwa Tunisia kama wameyaaga mashindano.

Kundi lao mambo yako hivi:

Jedwali
BBC Sport

Habari za hivi pundeBatshuayi apewa nafasi, Hazard aondolewa

Roberto Martinez amemtoa nahodha Eden Hazard na nafasi yake akamuingiza Michy Batshuayi. Hii ina maana Hazard hatapata nafasi ya kufunga hat-trick sawa na Lukaku.

Kikosi cha Ubelgiji hakikubadilishwa

Ubelgiji walianza na wachezaji wale wale walioanza mechi dhidi ya Panama ambayo walishinda 3-0 mechi yao ya kwanza Kundi G. Vincent Kompany ambaye amekuwa akiuguza jeraha hakujumuishwa kwenye kikosi.

Belgium
BBC Sport

Habari za hivi pundeLukaku nje, Fellaini ndani

Ubelgiji 4-1 Tunisia

Romelu Lukaku amepoteza nafasi ya kujipatia hat-trick. Ameondolewa uwanjani na nafasi yake ameingia Marouane Fellaini.

Mabao ni Eden Hazard na Romelu Lukaku

 • Ubelgiji wanaongoza 4-1 dhidi ya Tunisia, kwenye mechi ambayo imeshuhudia ufungaji wa mabao mengi kipindi cha kwanza
 • Lukaku amefunga mabao mawili, na sasa ana jumla ya mabao manne, sawa na Ronaldo
 • Bao la kwanza lilifungwa na Eden Hazard kupitia penalti dakika ya 6, Lukaku akafunga (16' , 45'+3). Hazard ameongeza lake la pili dakika ya 51
 • Tunisia walifungiwa na Bronn dakika ya 18 lakini akaumia na kuondolewa uwanjani kwa machela dakika chache baadaye
Hazard
AFP
Lukaku
AFP