Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Poland wamepoteza mechi saba kati ya mechi zao tisa Kombe la Dunia.
 2. Tangu kuifunga Portugal 1-0, 1986, Poland haijwahi tena kuzuia goli dhidi yake.
 3. Lewandowski ndiye nyota wa Poland: Amefunga mabao 21 kwenye mechi 16 timu ya taifa.
 4. Colombia imewahi kufungwa mechi mbili mfululizo Kombe la Dunia mara moja peke
 5. Haijawahi kukosa bao kwenye mechi 19 Kombe la Dunia
 6. Juan Quintero ni mchezaji wa Kwanza wa Colombia kufunga bao makala mawili

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Colombia wapunguza pupa ya Poland, Onyo kwa Senegal!

Poland 0-3 Colombia

Poland ilianza mchuano kwa kasi na pupa. Pasi baada ya nyingine, mkwaju baada ya mwingine.

Hata hivyo ngome ya Colombia ikiongozwa na beki wa Barcelona Yerry Mina iliwazima.

Baada ya dakika 90, Poland walionyesha hisia za kuvunjika kwa moyo na matumaini.

Ukuta wa Colombia, Yerry Mina alidhihirisha ujumuishaji wake kikosini alipoipa Colombia uongozi kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Hata mbinu za mkufunzi wa Poland Adam Nawalka kuwabadili mabeki hazikufua dafu.

Mfungaji Radamel Falcao alipata muda wa kuweka historia alipojipa bao lake la kwanza Kombe la Dunia baada ya kuwa nje ya Dimba la Brazil miaka 4 iliyopita.

Falcao alifunga bao dakika ya 70.

Winga na Beki mshambulizi Juan Cuadrado aliongeza mabao ya Colombia maarufu Los Cafeteros dakika ya 75 na kuwaamsha maelfu ya mashabiki wa Colombia uwanjani Kazan.

Kurejea kwa nyota James Rodriguez iliipiga jeki Colombia kwani alichangia pasi mbili muhimu zilizozalisha mabao.

Kipa David Ospina pia alikuwa kiungo wa kutegemewa kwa Colombia kutokana na uzuiaji wake wa mikwaju.

Fomu yake mechini huenda ikafufua kumbukumbu za kipa wa zamani wa timu hiyo Rene Higuita aliyekuwa uwanjani kushuhudia ngarambe hiyo.

Macho ya mamilioni ya wapenda soka sasa yataelekezwa uwanja wa Samara Alhamisi Ijayo.

Simba wa Teranga Senegal watakuwa wanakwatuana na Colombia Katika mchuano wa kukata na Shoka kundi H.

Awali Senegal ilipoteza nafasi ya kupata ushindi baada ya kuiruhusu Japan kusawazisha mara mbili.

Michuano hiyo siku ya Alhamisi tarehe 28 Juni itaamua hatma ya watakosalia na watakafikisha salamu nyumbani.

...........imekuwa siku njema nanyi Kombe la Dunia...........Ungana nasi Kesho!

Gumzo zaidi, Kurasa zetu za Facebook na Twitter!

Wachezaji wa Poland
Reuters
Wachezaji wa Poland

Poland nje, Kundi (H) yashika moto.

Mechi imekamilika: Poland 0-3 Colombia

Colombia yaamka, yaipa kazi Poland

90' Poland 0-3 Colombia

..........Muamerika Kusini amekasirika Kazan na kuisambaratisha Poland.

Dakika 5 zaidi kuchezwa!

Matokeo
BBC Sport
Mechi kufikia sasa

Leno na Cech chungeni: Ospina

87' Poland 0-3 Colombia

Kipa wa Arsenal na Colombia David Ospina amekuwa uti wa mgongo wa Colombia usiku huu............

Pengine anatetea nafasi yake kwa wanabunduki wa Arsenal?

Ospina
AFP
Ospina

Falcao na Cuadrado: Waliachiliwa na Chelsea, waikomboa Colombia

83' Poland 0-3 Colombia

Radamel Falcao na Juan Cuadrado, walitemwa na Chelsea .......lakini Usiku huu wameifaa

.................COLOMBIA.......................

Juan Cuadrado
Getty Images
Juan Cuadrado,

Nimefika: Falcao

Poland 0-3 Colombia

Amerejea baada ya kukosa Kombe la Dunia Brazil 2014 kupitia jeraha.

Amefunga bao lake la kwanza Kombe la Dunia.

Baada ya kupokea pasi kutoka Quintero, Falcao alimdhalilisha Szczesny na kuzidisha uongozi wa Colombia.

Falcao
Getty Images
Falcao

Cuadrado na Colombia waikunguta Poland: 3-0!

75' Poland 0-3 Colombia

Colombia Mbili Mbele

74' Poland 0-2 Colombia

 • Falcao amezidisha uongozi wa Colombia (Dakika ya 70)
 • Yerry Mina alifunga bao la Kwanza (Dakika ya 40)
Colombia
BBC Sport
Matokeo hadi sasa

Colombiiiiiiiaaaaaaaaaaaaaaaaaaa 2!

70' Poland 0-2 Colombia

Radamel Falcao na bao la Pili la Colombia.

Zimesalia dakika 20 mechi kumalizika.

Messi asherekea

Poland 0-1 Colombia

.........siku ya kuzaliwa

View more on twitter

Poland wamleta 'Turbo'

65 'Poland 0-1 Colombia

Huenda Kocha ameona udhaifu wa kikosi chake ni ukosefu wa kasi.......

Dawid Kownacki amempisha Kamil Grosicki maarufu 'Turbo' kuleta marekebisho!

OOOOOOOOOOOOOOSpinaaaaaaaaaa

60' Poland 0-1 Colombia

Kipa Ospina ameiokoa Colombia na kudumisha uongozi wake mechini!

Amemnyima Robert Lewandowski!

Tuko nanyi Colombia!

58' Poland 0-1 Colombia

......................ndizo kauli zinazotoka Kazan Arena!

Colombia imesalia na dakika 30 kufufua matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mchujo.

Colombia
Getty Images
Shabiki wa Colombia

James Rodriguez

54' Poland 0-1 Colombia

James Rodriguez ana umuhimu kiasi gani kikosini?

View more on twitter

Lewandoski amelemewa?

49' Poland 0-1 Colombia

Mbali na cheo chake cha Unahodha, kinachoonyeshwa kupitia alichovishwa mkononi, Robert Lewandoski anadaiwa kuotoonekana akiitumikia Poland.

Robert Lewandoski
Getty Images
Robert Lewandoski

Poland

45' Poland 0-1 Colombia

........Kipindi cha pili kimeng'oa nanga!

Kuna uhaba wa mabao Poland, lakini sio ukosefu wa wafungaji.

Huduma za wafungaji shupavu wa Poland Jakub Błaszczykowski, Kamil Grosicki na Arkadiusz Milik iwapo zitahitajika, wataingia uwanjani.

Wanasubiri kuitwa kutoka benchi.

Mina arudisha matumaini ya mashabiki wa Colombia

Kipindi cha pili Kuanza: Poland 0-1 Colombia

Waliingia kwenye mchuano baada ya kupoteza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Japan 1-2.

Lakini sasa wanashikilia nafasi ya 3 kundi H, wakionekana kukaribia kuwatimua Poland kutoka Kombe la Dunia 2018.

Aidha, Yerry Mina aliyejumuishwa kikosini leo, amewaamsha mamilioni wa Colombia na maelfu ugani Kazan kupitia bao lake.

Iwapo hali itabaki kuwa hivi, basi kazi kwa Senegal....au Kipute cha Kukata na shoka kutarajiwa.

Yerry Mina
Getty Images
Yerry Mina
Colombia
Getty Images
Mashabiki wa Colombia

Bao la Colombia: Ushirikiano bora

Kipindi cha Kwanza: Poland 0-1 Colombia

Ingawa bao la mchezaji kutoka eneo lililo mbali husifika, bao la Colombia limedhihirisha umoja ni nguvu.

..............ilianzaje?

James Rodriguez pasi fupi kwa Juan Cuadrado, naye akausindikiza mpira hadi Juan Quintero.

Nyota huyo wa Porto Juan Quintero, akawaduwaza mabeki wa Poland kabla ya kumuunganishia Rodriguez.

Rodriguez akachanja krosi safi kwenye sanduku na kumpata Yerry Mina.

Mina akaachilia kichwa kutoka yadi 6 na kumuacha kipa wa Poland Wojciech Szczesny akipaa angani!

Colombia Kifua mbele

45' Poland 0-1 Colombia

Mchuano unakaribia muda wa mapumziko: Bao la Yerry Mina tofauti ya timu hizi.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Colombia: Aguilar ajeruhiwa.

42' Poland 0-0 Colombia

Kiungo wa Colombia Abel Aguilar amejeruhiwa.

Ameondolewa na kumpisha Mateus Uribe wa timu ya Club America.

Aguilar
Getty Images
Aguilar

Bao: 1-0: Mina aifungia Colombia

41' Poland 0-1 Colombia

Beki Yerry Mina, kichwa kama guu - dakika ya 40!

Colombia imechukua uongozi.

Adam Nawałka: Beki wa Zamani, mwalimu wa sasa Poland

31' Poland 0-0 Colombia

Huenda ukamuona akiwapa mabeki wake, Piszczek na Pazdan ushauri.

Kocha wa Poland: Adam Nawałka mwenyewe ni mmoja wa mabeki tajika kwenye historia ya soka Poland.

Alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliong'aa Kombe la Dunia 1978.

Rodriguez: Roho ya Colombia

29' Poland 0-0 Colombia

Rodriguez
Reuters
Rodriguez

Dukuduku dakika 20 za Kwanza

24' Poland 0-0 Colombia

 • Falcao na Cuadrado wamepoteza fursa nzuri ya Kufunga.
 • Wachezaji wa Colombia wanamsaka mfungaji James Rodriguez kwa pasi bora.
 • Piotr Zielinski wa Poland ameachilia kombora lililozuiwa na beki wa Barcelona Yerry Mina.
 • Awali Robert Lewandowski alimkaribisha Yerry Mina mechini kwa kumkanyaga vidole.
 • Poland walipata kona tano mechini, mbili mfululizo: la pili baada ya beki wa Colombia Johan Mojica kuondoa.
 • Dawid Kownacki anayeshiriki mechi yake ya kwanza kwa Poland, anaandaa krosi za maana.

Rene Higuita

13' Poland 0-0 Colombia

Kipa wa zamani wa Colombia mwenye madaha na madoido, Rene Higuita ni mmoja wa mashabiki uwanjani Kazan Arena, kuishabikia Colombia.

Ataleta bahati kwa Colombia?

Rene Higuita
Getty Images
Rene Higuita

Poland V Colombia

06' Poland 0-0 Colombia

Mchuano umeanza huku pande zote zikijituma kusaka bao.

WOte walipoteza mechi zao za kwanza.

Poland V Colombia: Kikosi cha Colombia

Poland 0-0 Colombia

Nyota James Rodriguez kuanza ni mojawapo ya mabadiliko manne ya Colombia.

Beki wa Barcelona Yerry Mina, Viungo Wilmar Barrious na Abel Aguilar waanza pia.

Oscar Murillo, Jefferson Lerma, Carlos Sanchez na Jose Izquierdo walishwa upanga!

Kikosi Kamili cha Colombia:

Ospina, Arias, Mina, Sanchez, Mojica, Aguilar, Barrios, Cuadrado, Rodriguez, Quintero, Falcao.

Colombia
BBC Sport
Colombia

Poland na Colombia: Kikosi cha Poland

Poland 0-0 Colombia

Vikosi uwanjani, lakini wa kuanza ni kina nani?

Ni mabadiliko kwenye ngome ya Poland:

Jan Bednarek na Bartosz Bereszynski kuanza na kuchukua nafasi za Thiago Cionek, na kiungo Jakub Blaszczkowski.

Dawid Kownacki amechukua nafasi ya Arkadiusz Milik.

Watakaoanza Poland: Szczesny, Bereszynski, Piszczek, Bedranek, Pazdan, Rybus, Krychowiak, Goralski, Zielinski, Kownacki, Lewandowski.

Poland
BBC Sport
Poland

Poland V Colombia : Uwanja wa Kazan Arena, Kazan

Poland 0-0 Colombia

Ukubwa: Mashabiki 44,779*

Ulizinduliwa: 2013: Unapatikana Maili 510 kutoka jiji la Moscow.

Uwanja huu ulichorwa na wahandisi waliounda michoro ya viwanja vya;

Emirates inayotumika na klabu ya Arsenal na New Wembley ya Uingereza.

Ingawa ni ndogo Zaidi ya viwanja hivyo, mvuto ni wa hali ya juu.

Ulikamilishwa Julai 2013 kutumika kuandaa mashindano ya kimataifa ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Baaaye uwlianza kutumika na klabu ya Rubin Kazan.

Kazan uliandaa mashindano ya kimataifa ya Maji mwaka wa 2015.

Kundi -H- Hatari? Haitabiriki? Haifahamiki?

Mechi ya Kundi H: Japan 2-2 Senegal

Kwanza, atakayefungwa leo kati ya Poland na Colombia, ataanza safari kuelekea nyumbani.

Lakini.....Iwapo watatoka sare......na

Kila mmoja ashinde mechi yake itakayofuata dhidi ya Japan na Senegal;

Tutakuwa na timu 4 zenye alama 4 kila mmoja.

Kumaanisha;

Kundi hili litaamuliwa kupitia: Tofauti ya magoli (au magoli yaliyofungwa na timu au fair play).

Licha ya yote:

Japan na Senegal wanahitaji alama 1 tu katika michuano yao ijayo kushiriki awamu ya muondoano.

Ratiba ya mechi za Kundi H: Alhamisi 28 JUNI:

Japan V Poland: Volgograd Arena, Volgograd

Senegal V Colombia: Samara Arena, Samara

Kundi H
BBC Sport
Kundi H

Wikendi ya Wague: Mfungaji wa Afrika mwenye Umri mdogo

Mchuano umemalizika: Japan 2-2 Senegal.

Si siku njema kwa Senegal kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Japan...........

Lakini ....................Itakuwa ni wikendi isiyosahaulika kwa Moussa Wague.

Nyota huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 19, ndiye mchezaji wa Afrika mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga goli Kombe la Dunia..............

Alikaribia kuipa Senegal ushindi, lakini kipute hicho kilimalizika sare ya 2-2.

Moussa Wague
Getty Images
Moussa Wague

Simba wa Senegal wakosa kuikwaruza Japan

Matokeo: Japan 2-2 Senegal

 • Sadio Mane alitangulia kuifungia Senegal ( Dakika ya 11)
 • Takashi Inui akaisawazishia Japan (Dakika ya 34)
 • Moussa Wague alionekana kuipa Senegal ushindi (Dakika ya 71)
 • Keisuke Honda akainyima Senegal kwa kufunga goli la kusawazisha (Dakika ya 78)
Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Honda aandikwa kitabu cha historia

92' Japan 2-2 Senegal

Keisuke Honda amejiunga na wachezaji waliofunga bao na kuchangia kuipa timu yao bao kwenye Kombe la Dunia.

Tangu 1966, ni Wachezaji sita tu wamewahi kufanikisha hili.

 1. Keisuke Honda
 2. David Beckham
 3. Asamoah Gyan
 4. Grzegorz Lato
 5. Arjen Robben
 6. Rudi Voller.

Honda amfunga Simba

87' Japan 2-2 Senegal

Nguvu mpya wa Japan, Keisuke Honda

Honda
Getty Images
Honda

Goli la Japan kwa maelezo

84' Japan 2-2 Senegal

Kipa wa Senegal Khadim Ndiaye, huenda ameiharibia Senegal ushindi muhimu!

Kosa lake ??

Alitoka akijaribu kuupangua mpira......lakini hakuuwahi......

Mkwaju ulikwenda kwake Inui, mfungaji wa goli la kwanza, aliyeurejesha mpira eneo hatari.

Okazaki akamzuia kipa Khadim Ndiaye kuunyaka...na pasi ukamfikia Honda......

Ambaye .............

hakuchelea kutikisa wavu......na......Kusawazishia Japan

Japan wawaadhibu Senegal!

79' Japan 2-2 Senegal

Wague aipa Senegal uongozi!

74' Japan 1-2 Senegal

Moussa Wague mchezaji chipukizi mwenye umri wa miaka 19 ameifungia Senegal.

Bao limefungwa dakika ya 71.

Huenda bao hilo likaipa Senegal alama 3 muhimu, na tiketi hadi hatua ya timu 16 za mwisho.

Sene-gggggggggooooooooooooooooollllllllllll

Japan 1-2 Senegal

Senegal wafanya mabadiliko.

68' Japan 1-1 Senegal

Kouyate ameingia nafasi ya N'Diaye

Jaaappppppaaaaan........Lakini kwenye mwamba wa goli

65' Japan 1-1 Senegal