Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Brazil imekwishatua hatua ya mchujo lakini inahitaji sare au ushindi dhidi ya Serbia kujihakikishia nafasi yao.
  2. Uswizi inahitaji ushindi kufuzu, lakini pia droo itatosha iwapo Serbia itatoka sare au kupoteza dhidi ya Brazil.
  3. Serbia huenda ikafuzu iwapo itatoka sare na Brazil nayo Uswizi ilazwe na Costa Rica kwa mabao mawili au Zaidi.
  4. Costa Rica tayari imeliaga Kombe la Dunia baada ya kupoteza mechi zake zote.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Siku ya Senegal na Afrika

Mechi za Kundi H:

Mhimili wa Afrika Kombe la Dunia Senegal, imebakisha tu Colombia kurejesha tabasamu kwa nyuso za wapenzi wa soka barani.

Hii ni baada ya wawakilishi wengine kuondolewa Kombe hilo.

Colombia imezua fujo kundi H kwa kuinyorosha Poland 3-0 kufuatia kurejea kwa James Rodriguez.

Japan na Senegal wana alama 4 kila mmoja nayo Colombia ikiwa ni ya tatu na lama 3.

Wawili hao watakwatuana uga wa Samara Arena, Samara.

Ngoma nyingine Kundi H itapigwa kati ya Japan na Poland uwanja wa Volgograd Arena, Volgograd.

Hazard V Harry Kane Alhamisi.

Mechi za Kundi G:

Uingereza V Ubelgiji: Kaliningrad.

Ni mchuano usiokuwa na umuhimu mbali na kuwania ubabe kwani kila mmoja ametia kapuni alama sita.

Uingereza na Ubelgiji tayari wamefuzu kwa hatua ya mchujo baada ya kuzipa funza Tunisia na Panama.

............................................................

Panama V Tunisia Mordovia Arena, Saransk

Kinyume na wanachama wenzao wa Kundi, wawili hawa watakuwa wacheza wakifahamu ni rahisi kwao kufika uwanja wa ndege kuliko hatua ya mchujo.

Panama inadaiwa mabao 8 Kombe la Dunia nayo Tunisia inadaiwa mabao manne.

Brazil V Mexico: Uswizi V Sweden wiki Ijayo

Mechi za hatua ya muondoano.

Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil watakuwa wenyeji wa Mexico Samara Arena, Samara Jumatatu tarehe 2/7/2018.

Hii ni baada ya Brazil kudondoka hadi hatua ya mchujo kwa kumaliza wa kwanza Kundi E na alama 7.

Kwa upande wake Mexico ilinyakua nafasi ya pili Kundi F baada ya Ujerumani kulemewa na Korea Kusini 2-0.

Siku itakayofuata ya Jumanne 3/7/2018, Uswizi itakuwa mgeni wa Sweden iliyotwaa nafasi ya kwanza Kundi F, ugani Krestovsky, Saint Petersburg,.

Uswizi ilijikakamua na kutoka sare 2-2 dhidi ya Costa Rica ugani Nizhny Novgorod.

Licha ya kujaribu kuipiku Uswizi nafasi ya pili, Serbia imelazimika kujituliza na nafasi ya tatu Kundi E.

Nyota wa Uswizi aliyetia kimiani goli la kwanza dhidi ya Costa Rica, Blerim Dzemaili ndiye mchezaji bora wa mechi hiyo .

Dzemaili alifungua hesabu (dakika ya 31) lakini Waston akaisawazishia Costa Rica (dakika ya 56).

Uswizi ilikaribia kusajili ushindi wa pili Urusi baada ya nguvu mpya Drmic kufunga zikiwa zimesalia dakika chache mechi kumalizaika (dakika ya 88). Ndoto hizo zilikatizwa baadaye.

Licha ya kuwa na mchezo mzuri mechini, mdakaji wa Uswizi Sommer alijifunga mwenyewe baada ya Penalti ya Ruiz (dakika ya 93).

Wawili kati ya timu hizi nne wataliaga kombe hili na kujiunga na timu 12 ambazo kwa sasa zimegeuka watazamaji baada ya kutemwa hatua ya makundi.

Kundi E
BBC Sport
Kundi E

Uswizi ndani ya 16 za mwiso

Kipute kimekamilika: Uswizi 2-2 Costa Rica

Serbia nje ya Kombe la Dunia

Mechi imekamilika: Serbia 0-2 Brazil.

Brazil wamemaliza wa kwanza Kundi E.

  • Paulinho na goli la kwanza (Dakika ya 36)
  • Thiago Silva kwa kichwa goli la pili (Dakika ya68)

Costa Rica wapachika penalti: Bryan Ruiz!

93' Uswizi 2-2 Costa Rica

Dakika za Drmic Starehe Uswizi

90+ Uswizi 2-1 Costa Rica

Josip Drmic aliingia dakika chache zilizopita na kuchukua nafasi ya Mario Gavranovic........

Kumbe wachezaji wa akiba wa Uswizi ni mabao ya akiba pia?

Drmic dawa ya Costa Rica

87' Uswizi 2-1 Costa Rica

Unakumbuka bao la Rojo dhidi ya Nigeria? ......ni pacha lake!

Neymar ajaribu kuina...bila mafanikio.

87' Serbia 0-2 Brazil

Costa Rica kutoka Urusi na bao

86' Uswizi 1-1 Costa Rica

Joel Campbell amewatatiza mabeki wa Uswizi, lakini timu hiyo huenda isipate ushindi.

Campbell aliupinda krosi kufuatia kona na Kendall Waston akaipa Costa Rica bao la kusawazisha dakika ya 56.

Bao hilo ni la kihistoria kwa Costa Rica kwani, ni bao lao la kwanza 2018.

Mwisho walifunga dhidi ya Ugiriki hatua ya mchujo Kombe la Dunia 2014.

Kendall Waston
Getty Images
Kendall Waston

Coutinho nje Renato August ndani

81' Serbia 0-2 Brazil

Ni mabadiliko Brazil.

Brazil watoa onyo: 2018 sio 2014.

80' Serbia 0-2 Brazil

Mabingwa hao mara 5 Kombe la Dunia walidhalilishwa wakiwa wenyeji wa Kombe hilo 7-1 na Ujerumani...(Kwa sasa wameenda nyumbani) mnamo 2014.

Kwa sasa ndio viongozi wa Kundi E wakiwa na alama 7.

Brazil
Getty Images
Brazil

Kosa si sare, ni mastaa?

74' Serbia 0-2 Brazil, Uswizi 1-1 Costa Rica

Iwapo bado unakumbuka, Ujerumani na Mexico wakicheza mechi zao za awali dhidi ya Korea Kusini na Sweden, walikuwa wamevaa sare za kufanana. Wawili wote waliishia kulazwa mechi zao!

Uswizi na Serbia leo wamevaa sare za kufanana.

Lakini kufikia sasa, wekundu wa Serbia tu ndio wako nyuma kwa magoli 2.

Uswizi na Costa Rica wanakabana sare 1-1 hadi sasa.

Brazil ya 2018...Brazil Bora au Bora Brazil?

71' Serbia 0-2 Brazil

Brazil ni maarufu kwa mpira wenye burudani lakini mechi hizi tatu za sasa Kombe la Dunia zimetoa taswira tofauti kuhusu Samba Boys.

Kazi ya Neymar ya kupiga mbizi anapoguswa na kusaka frikiki na mabeki waliochoka ni baadhi ya udhaifu unaozungumziwa.

Cioutinho ndie ameng'aa katika Kombe la Dunia 2018.

Amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja muhimu mechi hii.

Neymar
Reuters
Neymar

Brazil mbele tena!

69' Serbia 0-2 Brazil

Beki Thiago Silva ameacha majukumu ya kuzuia magoli na kuchukua majukumu ya kuyafunga. Ameipa Brazil bao dakika ya 68.

Bao hilo limezika matumaini ya Serbia.

Thiago Silva amzuia Mitrovic

61' Serbia 0-1 Brazil

Mitrovic aliachilia kichwa lakini Silva ameondoa mpira.

Paulinho...jiwe lililokataliwa na Tottenham, bora Brazil.

55' Serbia 0-1 Brazil

Mfungaji Paulinho ametia kimiani bao lake la 8 Brazil mechi yake ya 18 akiichezea timu hiyo ya taifa.

Paulinho
Getty Images
Paulinho

Tabasamu Costa Rica!

56' Uswizi 1-1Costa Rica

Watson amefunga kufuatia mpira wa kupinda wa Kona!

Nemanja Matic nje pia

54' Serbia 0-1 Brazil

Kiungo wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic amecheza mechi yake ya mwisho Urusi iwapo timu yake itachujwa.

Lakini wakifuzu kwa hatua ijayo ya mchujo, hatoshiriki kwani atakuwa anatumikia adhabu ya kupokea kadi ya njano.

Costa Rica waimarika lakini kuchelewa

48' Uswizi 1-0 Costa Rica

Baada ya kutapatapa dhidi ya Brazil na Serbia mechi zake za awali Kundi E, Los Ticos wamerejea na fomu nzuri dhidi ya Uswizi licha ya kufunga virago tayari.

Usiijaribu Uswizi

46' Uswizi 1-0 Costa Rica

Uswizi imeshinda mechi zake sita kati ya saba Kombe la Dunia ilizomaliza kipindi cha kwanza ikiongoza.

Ni Uhispania tu imetia rekodi yao safi dosari 2-1 mnamo 1966.

Uswizi
Getty Images
Uswizi

Neymar pia abebwa

Kipindi cha Kwanza: Serbia 0-1 Brazil, Uswizi 1-0 Costa Rica

Mastaa walibebeshwa matumaini ya timu, lakini, baada ya majukumu kuwa mazito, wamegeuka wa kubebwa walipokwama!

Baada ya Messi kubebwa na Marcos Rojo begani walipoponyoka dhidi ya Nigeria, imekuwa ni zamu ya Neymar kubebwa baada ya Paulinho kukatiza ukame Samba Boys!

Neymar abebwa
Getty Images
Neymar akibebwa

Nani ata -E-ndelea au ata-E-lekea nyumbani Kundi E?

Muda wa mapumziko: Serbia 0-1 Brazil, Uswizi 1-0 Costa Rica

  • Farasi ni watatu Kundi E kwani Costa Rica tayari imeliaga Kombe la Dunia baada ya kupoteza mechi zake za kwanza.
  • Brazil imekwishatua hatua ya mchujo lakini inahitaji sare au ushindi dhidi ya Serbia kujihakikishia nafasi hatua ya mchujo.
  • Ushindi muhimu Uswizi,lakini pia droo ni sawa iwapo Serbia itatoka sare au kupoteza dhidi ya Brazil.
  • Serbia pia ina nafasi ya kufuzu iwapo itatoka sare na Brazil nayo Uswizi ilazwe na Costa Rica kwa mabao mawili au Zaidi.

Uswizi sako kwa bako na Brazil Kundi E

Kipindi cha Kwanza: Serbia 0-1 Brazil, Uswizi 1-0 Costa Rica

.....Msimamo baada ya mabao.......

Kundi E
BBC Sport
Kundi E

Stephan Lichtsteiner nje ya mchuano ujao

44' Uswizi 1-0 Costa Rica

Nahodha wa Uswizi na beki mpya wa Arsenal Stephan Lichtsteiner hatoshiriki mchuano ujao wa hatua ya muondoano iwapo watafuzu baada ya kusajiliwa kitabu cha refa kwa kupokea kadi ya njano.

Kombe la Dunia lamalizika kwa Marcelo

39' Serbia 0-1 Brazil

Beki wa Brazil Marcelo ameumia dakika ya 12 na jinsi alivyotoka, linaashiria kuwa ni jeraha nzito.

Marcelo
re
Marcelo

Samba boys wapachika moja kupitia Paulinho!

36' Serbia 0-1 Brazil

Uswizi yawakomesha Costa Rica

33' Uswizi 1-0 Costa Rica

Blerim Džemaili ameachilia shuti safi dakika ya 31 nusra ararue wavu.

Ni alama 3 kwa Uswizi.

Taharuki Uswizi na Costa Rica

25' Uswizi 0-0 Costa Rica

Hawajafungana kufikia sasa.

Lakini....Kipa wa Uswizi Yann Sommer ndiye aliyepigishwa mazoezi kufikia sasa. Shuti za Costa Rica zimemkwamisha.

Matokeo
BBC Sport
Matokeo

Amerika ya Kusini kupunguzana?

Serbia V Brazil, Uswizi V Costa Rica

Brazil....itachuana na mwenzake kutoka Amerika ya Kusini,

Mexico......hatua ya muondoano!

Uswizi watakwatuana na Sweden.....

Lakini ni iwapo..........

Matokeo yatabaki kuwa hivi......

Neymar aitikia wito wa Tite

18' Serbia 0-0 Brazil

Mchezo wa Brazil unaonekana kwenda kulingana na miondoko ya Neymar.

Ndio ushauri wa Tite kwa nyota huyu wa PSG?

Neymar na Tite
Reuters
Neymar na Tite

Serbia Yamakinika

16' Serbia 0-0 Brazil

Serbia wamerejea kwenye mechi. Awali Brazil iliwatawala, kwa kuwazidi kwenye umiliki wa mpira.

Neymar amepokea mpira na sasa Serbia ndio wa kusaka mpira Brazil wakisakata.

Kasoro ya Costa Rica Umri?

14' Uswizi 0-0 Costa Rica

Wachezaji 10 kikosi cha Costa Rica wamezidi Miaka 30.

Costa Rica
EPA
Costa Rica

Marcelo nje, Filipe Luis aingia Brazil

11' Serbia 0-0 Brazil

Marcelo amejeruhiwa na kuondoka mechini mapema!

Msimamo Kundi E

Serbia V Brazil, Uswizi V Costa Rica

Kundi E
BBC Sport
Kundi E

Wanaofaa kucheza kwa tahadhari

04' Serbia 0-0 Brazil

Wachezaji wafuatao wanastahili kujiepusha na kadi ya njano la sivyo, huenda wakakosa kushiriki hatua ya muondoano!

Brazil: Neymar, Philippe Coutinho na Casemiro.

Serbia: Aleksandar Mitrovic, Sergej Milinkovic-Savic na Nemanja Matic...

Uswizi V Costa Rica

01' Uswizi 0-0 Costa Rica

Kipute kimeanza ugani Nizhny Novgorod!

Serbia V Brazil

00' Serbia V Brazil

Mechi imeanza Otkrytie Arena.

Costa Rica kibarua kwa Uswizi

Serbia V Brazil, Uswizi V Costa Rica

Kiungo Bryan Ruiz wa Sporting Lisbon anacheza ,echi yake ya 111 kwa timu ya taifa.

Ingawa wametemwa kutoka Kombe hilo, wanacheza kwa faraja!

Kikosi kamili Costa Rica: 1 Keylor Navas (c) 2 Nhlanhla Zwane 3 Giancarlo Gonzalez 19 Kendall Waston 16 Cristian Gamboa 5 Celso Borges 20 David Guzman 8 Bryan Oviedo 9 Daniel Colindres 10 Bryan Ruiz 12 Joel Campbell.

Costa Rica
BBC Sport
Costa Rica

Hakuna wasiwasi Uswizi

Serbia V Brazil, Uswizi V Costa Rica

Xhaka na Shaqiri kikosini licha ya kuonywa na FIFA.

Ingawa 2014 waliponea nchini Brazil, ambapo waliponyoka kutoka Kundi lao, 2018 wana matumaini wataitesa Costa Rica.

Ni kazi ugani Nizhny Novgorod..maarufu uga wa huzuni!

Kikosi cha Uswizi: Yann Sommer 2 Stephan Lichtsteiner (c) 22 Fabian Schär 5 Manuel Akanji 13 Ricardo Rodríguez 11 Valon Behrami 10 Granit Xhaka 23 Xherdan Shaqiri 15 Blerim Dzemaili 7 Breel Embolo 18 Mario Gavranovic

Shaqiri
Getty Images
Shaqiri