Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Ufaransa na Argentina wanakutana kwa mara ya 12. Argentina imefunga Ufaransa mechi 6: Ufaransa imeshinda mbli.
  2. Argentina ndio timu ya mwisho kutoka Amerika ya Kusini kuipiga Ufaransa. 1930 (1-0) and 1978 (2-1).
  3. Ufaransa imepoteza dhidi ya Argentina vipindi viwili walipokutana Kombe la Dunia.
  4. Ufransa imefuzu hatua ya robo fainali kila mara iliposhiriki hatua ya mchujo. (1986, 1998, 2006, 2014).
  5. Lionel Messi,licha ya kuwa mchezaji wa mwisho wa Argentina kufunga dhidi ya Ufaransa, bado anasubiri bao lake la kwanza hatua za mchujo

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Cavani akarabia kumtoa Ronaldo

18' Uruguay 1-0 Ureno

Edison Cavani alifunga bao dakika ya 7.

Uruguay imepigwa jeki na bao hilo.

Edison Cavani
Getty Images
Edison Cavani

Ufaransa watua Robo fainali!

Mechi imekamilika: Ufaransa 4-3 Argentina

Ufaransa imetua robo fainali ya Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo na kubadili historia kufuatia ushindi kwenye mchuano wa kuvutia uwanjani Kazan dhidi ya Argentina.

Argentina, iliyokuwa na baadhi ya wachezaji bora duniani, Lionel Messi na Diego Maradona ugani Kazan, mmoja akicheza mwingine akiwashangilia, wameliaga Kombe la Dunia Urusi 2018.

Mabao ya haraka ya Kijana chipukizi Kylian Mbappe kipindi cha pili yameipa Les Bleus tiketi ya robo fainali Urusi 2018.

Ufaransa inamsubiri mshindi kati ya Uruguay na Ureno watakaokwatuana baadaye.

Ufaransa iliingia mechini vyema kwa kuchukua uongozi baada ya mlinzi Marcos Rojo kumuangusha Mbappe.

Griezmann alitandika Penalti hiyo na kujaa kimiani (dakika ya 13).

Hata hivyo, dakika chache kabla ya kipindi cha pili, Angel Di Maria aliisawazishia Argentina kwa shuti la ajabu kutoka yadi 30 na kumaliza kipindi cha pili kwa sare 1-1.

Punde tu pande hizo ziliporejea kutoka mapumziko, beki Gabriel Mercado aliinyakulia Argentina uongozi (Dakika ya 48) baada ya kuulekeza mkwaju wa Messi langoni.

Sherehe za Albiceleste zilikatizwa baadaye kwani uzembe wa ngome yake ilimruhusu beki Benjamin Pavard, aliyekuwa akishiriki mechi yake ya tisa kwa timu ya taifa, kuisawazishia Ufaransa. Pavard alifunga Dakika ya 58.

Ngoma ilionekana kumalizika sare kabla ya nyota wa PSG Mbappe kuidunisha Argentina kwa mabao ya haraka dakika za (64) na (68) na kuwainua mashabiki wa Ufaransa kutoka viti vyao.

Lionel Messi alijaribu kupunguza madeni ya Argentina kufuatia mabao hayo lakini mbio zake kwenye sanduku ziliandamwa na shuti lake dhaifu hadi kwa viganja vya mdakaji wa Ufaransa Lloris.

Argentina bao la tatu

Hata hivyo dakika chache baadaye Messi hakuchelea kumlisha Aguero naye nguvu huyo mpya, Kun Aguero alipiga kichwa safi dakika ya 92 na kukaribia kufufua matumaini ya Argentina.

Muda haukuwa na huruma kwa Argentina na kipute kilikamilika ushindi ukienda kwa Ufaransa.

Aguero airudisha Argentina mechini....lakini bado bao moja

90+ Ufaransa 4-3 Argentina

Deni ni bao moja tu sasa kwa Argentina!

Dakika 4 tu, zitaitosha Argentina?

90+ Ufaransa 4-2 Argentina

Mbappe ampiku Messi?

90' Ufaransa 4-2 Argentina

Kulingana nawe nani bora?

Mbappe ameigeuza Argentina kuwa kitoweo chake na kuwafunga magoli mawili wakati mchezaji bora wa dunia zamani Lionel Messi akisalia na mihangaiko!

Mbappe amepumzishwa kwa sasa baada ya kuwa chipukizi wa kwanza kufunga magoli mawili Kombe la Dunia tangu Pele dhidi ya Sweden 1958.

Mbappe
EPA
Mbappe
Messi
EPA
Messi

Frikiki kwa Argentina

87' Ufaransa 4-2 Argentina

Messi...Messi...Messi...hadi kwa mikono ya Lloris.

85' Ufaransa 4-2 Argentina

Amejaribu njia zote lakini juhudi zake zimeishia viganja vya Kipa wa Ufaransa Lloris.

Griezmann apumzishwa

83' Ufaransa 4-2 Argentina

Ni muda wa kudumisha uongozi Ufaransa.

Nabil Fekir ameingia nafasi ya Griezmann.

Pogba awaogopesha

80' Ufaransa 4-2 Argentina

Kiungo mshambulizi wa Manchester United amewatawala viungo wa Argentina mechini. Kwa nguvu na kwa maarifa!

Pogba
EPA
Pogba

Mkwaju wa ikabu Ufaransa, Griezmann aachilia

77' Ufaransa 4-2 Argentina

Ni zamu ya Argentina sasa kutekeleza uvamizi.

Mbappe apepea

75' Ufaransa 4-2 Argentina

Va va vooooom!

Magoli mawili kwa Mbappe ndani ya dakika 4!

Kylian Mbappe amedhihirisha ni kwa nini amenyakua nafasi kikosi cha kwanza Ufaransa licha ya umri wake mdogo (miaka 19).

Mbappe
EPA
Mbappe

Hatari lango la Argentina, lakini Mbappe aharibu

74' Ufaransa 4-2 Argentina

Argentina wastaajabu!

72' Ufaransa 4-2 Argentina

Zimesalia dakika 20 ugani Kazan na Argentina wanadaiwa mabao mawili.

Kylian Mbappe amewaadhibu kwa kufunga mabao mawili ya haraka chini ya dakika 4.

Jorge Sampaoli amewashikilia Dybala na Higuain au tuseme mabao kwenye benchi.

Sampaoli
Reuters
Sampaoli

Argentina taabani! La nne Ufaransa

69' Ufaransa 4-2 Argentina

Messi akatazwa njia, apata frikiki

65' Ufaransa 3-2 Argentina

Ni mkwaju wa ikabu kwa Argentina. Sergio Aguero naye ameingia.

Mbapppppppppppeeeeeeeeee awapa tena Ufaransa

63' Ufaransa 3-2 Argentina

Di Maria adai Penalti lakini bila mafanikio

60' Ufaransa 2-2 Argentina

Ni mpira wa kipa Hugo Lloris.

Ufaransa pia wapata!

59' Ufaransa 2-2 Argentina

Beki Benjamin Pavard ameachilia kombora lililojaa kimiani dakika ya 58!

Ni sare 2-2 ugani Kazan.

Nyufa Argentina robo fainali

55' Ufaransa 1-2 Argentina

Argentina itakuwa bila huduma za viungo mahiri Ever Banega na Javier Mascherano baada ya wawili hao kupokea kazi zao za pili Kombe la Dunia mwaka huu.

Ufaransa guu moja nje ya Kombe

53' Ufaransa 1-2 Argentina

Argentina imechukua uongozi mechini kwa mara ya kwanza na kufikia sasa ndio itakayoshiriki robo fainali.

Mkwaju wa Lionel Messi umeelekezwa wavuni na mwenzake Gabriel Iván Mercado.

Hata hivyo ni habari mbaya kwa Argentina kwani kiungo Ever Banega atakosa mchuano ujao kwa kunyakua kadi ya njano.

Goli la Di Maria lazua mjadala

Kipindi cha pili kuanza: Ufaransa 1-1 Argentina

Mkwaju wa Angel Di Maria nje ya sanduku ndio bao la kwanza kufungwa nje ya eneo hatari dhidi ya Ufaransa tangu 1986 ilipokuwa ikichuana na USSR.

Ni goli la kwanza kufungwa kutoka shuti la mbali nchini Urusi.

View more on twitter

Kipindi cha kwanza kimekamilika Kazan Arena.

Muda wa mapumziko: Ufaransa 1-1 Argentina

Kiungo Ever Banega alimuandalia Angel di Maria pasi maridadi. Di Maria, anayepiga na klabu ya PSG ligi ya Ufaransa, akaundaa mpira kabla ya kufyatua kutoka yadi 30 dakika ya 41.

Ni bao lililofufua matumaini ya Argentina Kombe la Dunia 2018 baada ya penalti ya Antoine Griezmann kuiweka Ufaransa kifua mbele dakika ya 13.

Angel Di Maria
Getty Images
Angel Di Maria akisherekea bao lake

Dakika mbili zaidi kuchezwa Kazan.

45' Ufaransa 1-1 Argentina

Di Maria abandika, amuacha Lloris taabani!

42' Ufaransa 1-1 Argentina

Winga wa Argentina Angel Di Maria amewarudisha mechini kwa kuachilia kiki nzito kama nanga hadi kwenye wavu!

Di Mariiiiiiiiaaaaaaaaaaaaaaaa!

41' Ufaransa 1-1 Argentina

Krosssiiiiiiiiiiiiiiii lakini nje

40' Ufaransa 1-0 Argentina

Ilikuwa ni hatari karibu na lango la Argentina, lakini Giroud hakuuwahi mpira.

Mpira ni wa Argentina. Wanapiga Pasi za karibu na za kutafutana.

Usumbufu wa Ufaransa

37' Ufaransa 1-0 Argentina

Jorge Sampaoli na Argentina wanatatizwa na Kasi ya chipukizi Kylian Mbappe na ukakamavu wa Antoine Griezmann. Usisahau Ousmane Dembele bado yuko kwenye benchi. Kazi ipo!

Di Maria......Di Maria ....Umepoteza dira Di Maria?

33' Ufaransa 1-0 Argentina

Mchango wake mkubwa bado hujaonekana mechini. Ancheza kwa uoga. Pindi apatapo mpira hurudi nyuma.

Di Maria
Reuters
Di Maria

Messi anacheza wapi?

30' Ufaransa 1-0 Argentina

Lionel Messi anaonekana akigusa wingi ya kulia na kule mbele. Huenda ndizo mbinu zao mechini.

Ufaransa waipigisha jaramba Argentina

28' Ufaransa 1-0 Argentina

Pogba na Kante watawala lakini Argentina wakataa. Argentina wanasaka bao la kusawazisha kwa juhudi zao zote.

Messi si muelekezi wangu: Kocha wa Argentina

26' Ufaransa 1-0 Argentina

Meneja wa Messi timu ya taifa Jorge Sampaoli amejitetea kuwa ndiye wa kupanga kikosi na sio Lionel Messi kama inavyodaiwa.

Sampaoli amekosolewa baada ya kanda ya video kusambaa akionekana kusaka ushauri wa Messi kabla ya kumshirikisha Sergio Aguero mechi iliyotangulia.

Walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria.

"Lilikuwa tu gumzo la kawaida na mchezaji wangu." alisema Sampaoli

Mbappe aambiwa Pambana

24' Ufaransa 1-0 Argentina

Refa Alireza Faghani amwambia Straika wa Ufaransa Mbappe acheze baada ya chipukizi huyo kulalamika kuchezewa visivyo.

Ni mpira wa Argentina sasa.

23' Ufaransa 1-0 Argentina

Argentina wanatengeneza na kusakata kule katikati.

Kona kwa Argentina lakini juu

22' Ufaransa 1-0 Argentina

Frikiki hatari lakini Pogba apiga juu

21' Ufaransa 1-0 Argentina

Rojo gharama

20 'Ufaransa 1-0 Argentina

Antoine Griezmann alimbwaga kipa wa Argentina Franco Armani na kuipa Ufaransa uongozi wa 1-0. Hii ni baada ya Rojo kusababisha penalti kwa kumtega Mbappe.

Rojo asababisha penalti
Reuters
Rojo asababisha penalti

Griezmann kuitoa Argentina?

12' Ufaransa 1-0 Argentina

Ndio siku Antoine Griezmann na Ufaransa wataitema Argentina?

Ufaransa kifua mbele Kazan Arena kufikia sasa!

Awali Marcos Rojo alimtega Kylian Mbappe na kuzalisha penalti.

Antoine Griezmann
EPA
Antoine Griezmann

Griezmann: Ufaransa hadi kapuni!

12' Ufaransa 1-0 Argentina

Griezmann Kupiga mkwaju

11' Ufaransa 0-0 Argentina

Penalti kwa Mbappe!

10' Ufaransa 0-0 Argentina