Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

  1. Edison Cavani ameifungia Uruguay mabao mawili, Pepe ndiye mfungaji wa bao la Ureno
  2. Ni mchuano wa kwanza kati ya pande hizi mbili Kombe la Dunia
  3. Tangu 1986, Uruguay haijavuka hatua ya mchujo mara tatu kati ya vipindi vinne. Imefaulu 2010 pekee na kufeli 1986, 1990 and 2014.
  4. Cristiano Ronaldo hajafunga hatua ya mchujo sawa na Lionel Messi

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Kina nani uwanjani jumapili 1/7/2018?

Mechi za mchujo, raundi ya pili Urusi 2018

Mechi ya Kwanza:

Mwenyeji Urusi atakuwa nyumbani dhidi ya Mabingwa wa Dunia 2010 Uhispania.

Kipute kitagaragazwa uwanja wa Luzhniki, Moscow.

Mechi ya Pili:

Macho ya Watanzania na waafrika yatakuwa ugani Nizhny Novgorod wakati kijana wa 'Tanga' Yussuf Poulsen mwenye asili ya Tanzania, atakuwa anapiga kikosi cha Denmark dhidi ya Croatia.

Anatarajiwa kurejea baada ya kutumikia adhabu ya mechi moja nje kutokana na kadi mbili za njano alizokusanya Urusi.

Uwanja huo sio geni kwa Luka Modric na Croatia kwani mji Nizhny Novgorod ndio mji ulioandaa mechi ambayo Croatia iliidunisha Argentina 3 mtungi mbele ya Maradona mechi ya makundi.

.............

Ni hayo tu kwa leo, hadi Jumapili...

Lakini gumzo zaidi ni Kurasa zetu Facebook na Twitter.

Tunatoa shukrani za dhati kwa kushiriki nasi Kombe la Dunia mtandaoni.

Alamsiki!

Mjadala wa ni nani bora kati ya Messi na Ronaldo benchi kwa sasa.

Argentina na Ureno wameliaga Kombe la Dunia.

Ukurasa mpya umefunguliwa kwa mashabiki wa soka duniani kuhusu ubora wa wachezaji maarufu wa soka.

Ingawa kila mwamba ngoma, ngozi huivutia kwake, ukweli ni kuwa, wachezaji wapya wametumia vyema jukwaa lililopatikana Kombe la Dunia Urusi 2018.

Baada ya kutawala vinywa vya wengi ndani ya zaidi ya kipindi cha miaka 10, kuondoka kwa Argentina na Ureno Urusi hatua za mchujo, imewanyima Messi na Ronaldo muda zaidi wa kujadiliwa.

Kurunzi za soka sasa zimeelekezwa kwa Neymar wa Brazil, Paul Pogba, Kylian Mbappe na Antoine Griezmann wa Ufaransa, Edison Cavani na Luis Suarez wa Uruguay, Harry Kane wa Uingereza na Romelu Lukaku wa Ubelgiji.

Orodha ni ndefu, lakini yote yataamuliwa kulingana na mchango wa wachezaji hawa kwa ufanisi wa timu zao.

Ronaldo
Reuters
Ronaldo
Mbappe ampa pole Messi
AFP
Mbappe ampa pole Messi

Ronaldo nje ya hesabu za kiatu cha dhahabu

Mfungaji bora Kombe la Dunia 2018.

Kuondoka kwa Ureno imekuwa pigo la kipekee kwa Ronaldo, aliyejitahidi kuzidisha mabao yake Urusi kwani ni wazi sasa wenzake watampiku kwenye uwaniaji wa tuzo ya mfungaji bora.

Ronaldo, alianza vyema baada ya kuondoka na mpira wa mechi dhidi ya Uhispania alipofunga hat-trick mechi yake ya kwanza.

Kipa wa Iran Ali Beiranvand pia alimnyima kwa kushika penalti yake walipokutana.

Kwa sasa mbio ni kati ya Lukaku, Harry Kane, Cavani na Mbappe na wengine.

Diego Costa wa Uhispania na Cheryshev wa Urusi watapata fursa ya kufunga mabao wawili hao watakapokwaruzana siku ya Jumapili katika uwanja wa Luzhniki, Moscow.

Orodha ya wafungaji Urusi 2018
BBC Sport
Orodha ya wafungaji Urusi 2018

Ufaransa kukwatuana na Uruguay

Robo fainali Urusi 2018

Baada ya Ulaya kuiondoa Amerika ya kusini, itakuwa ni zamu ya kulipiza kisasi kati ya Ufaransa, mwakilishi wa Ulaya na Uruguay inayotoka Amerika ya kusini Uwanja wa Nizhny Novgorod, Nizhny Novgorod Ijumaa tarehe 6/7/2018.

Aidha, Mbappe na Cavani, waliowatoa mahasimu wao, nao watakutana huku kila mmoja akilenga kujiongezea idadi ya mabao.

Kombe la Dunia kuwa bila Messi na Ronaldo

Argentina na Ureno watemwa nje ya Kombe la Dunia.

Kombe la Dunia 2018 limekuwa bila huruma kwa mastaa wawili wa soka waliotawala kizazi chao, Lionel Messi wa Argentina na Cristiano Ronaldo wa Ureno baada ya wawili hao kung'olewa ngarambe hizo hatua ya muondoano.

Uruguay yatua Robo fainali, Ronaldo na Ureno nje!

Mechi imekamilika: Uruguay 2-1 Ureno

Kona ya mwisho Ureno, Uruguay wakataa

94' Uruguay 2-1 Ureno

Uruguay dakika tu kutua robo fainali

93' Uruguay 2-1 Ureno

Ureno haijakata tamaa, lakini ushindi si jambo la Utani Uruguay

Ni Dakika 4 za ziada

90' Uruguay 2-1 Ureno

Ureno wanagonga ila hakuna njia ngome ya Uruguay

89' Uruguay 2-1 Ureno

Bernado Silva na Quaresma wanajaribu kuwavuta na kuwatawanya wapinzani, lakini walinzi makini wa Uruguay hawaruhusu.

Manuel Fernandes apiga lakini buuuuu

87' Uruguay 2-1 Ureno

Nguvu mpya amejaribu bahati nje ya sanduku, lakini mkwaju wake umewaudhi wenzake pamoja na kocha wake Fernando Santos.

Uruguay ngumu

86' Uruguay 2-1 Ureno

Saa zinakwenda ugani Fisht

81' Uruguay 2-1 Ureno

Ureno imebaki na chini ya dakika kumi kusawazisha na kusalia Urusi.

Ronaldo
Reuters
Ronaldo

Mbappe ampiku Messi, Cavani kumvuka Cristiano?

75' Uruguay 2-1 Ureno

Jumamosi la maajabu, Mbappe na Cavani wamejipa magoli mawili mechi za mchujo.

Imekuwa ni Ukame kwa Messi awali, sasa Cristiano Ronaldo aonekana kukwama.

Cavani ametoka kwa sasa na kumpisha Stuani.

Ureno imemtambulisha mshambulizi Andre Silva kuchukua nafasi ya Guedes.

Cavani
Reuters
Cavani akisherekea goli lake la pili dhidi ya Ureno

Cavani kazini abandika la pili langoni

64' Uruguay 2-1 Ureno

Ameukunja na kuuficha mkwaju wake uliomuaga kipa Patricio na kutulia wavuni.

Kibarua kwa Ureno kwa mara nyingine mechini!

Cavani bila kukawia aipa Uruguay bao la pili

62' Uruguay 2-1 Ureno

Kona nyingine kwa Ureno

60' Uruguay 1-1 Ureno

Ureno imekita kambi lango la Uruguay.

Mbinu mpya za Ureno zaokoa Ureno na Ronaldo

57' Uruguay 1-1 Ureno

Ureno imeanza kubadili mbinu dhidi ya Uruguay.

Imepunguza mipira ya juu, na kupiga pasi za kutafutana kwenye eneo la goli la Uruguay.

Tayari kona iliyotokana na njia hizo mpya za kuwahadaa mabeki wa Uruguay imewapa bao la kusawazisha.

Ronaldo
Getty Images
Ronaldo

Ureno wapata lao!

55' Uruguay 1-1 Ureno

Beki Pepe amekomboa kupitia kichwa!

Kona kwa Ureno, Uruguay wazuia

51' Uruguay 1-0 Ureno

Tabarez matumaini ya Uruguay

46' Uruguay 1-0 Ureno

Oscar Tabarez ndiye mkufunzi pekee aliyewahi kubeba Kombe la Dunia na Uruguay tangu 1970.

Alikuwa kocha wao pia Kombe la Dunia 1990. Lakini tangu alipowaaga,wameshiriki Kombe la Dunia mara moja kati ya nafasi nne.

Tangu alipoajiriwa tena 2006, Uruguay imeshiriki Kombe la Dunia mara 3 mfululizo.

Oscar Tabarez
EPA
Oscar Tabarez

Siri ya Uruguay: Kikosi kinacholenga kutua Fainali Urusi

Kipindi cha kipili: Uruguay 1-0 Ureno

Hawa ndio tegemeo la nchi nzima kuwafikisha fainali Urusi 2018.

Uwanjani Uruguay: Muslera, Caceres, Gimenez, Godin, Laxalt, Nandez, Torreira, Vecino, Bentancur, Suarez, Cavani.

Kwenye benchi: Campana, Varela, Sanchez, Rodriguez, De Arrascaeta, Stuani, Gaston Silva, Maxi Pereira, Gomez, Coates, Urreta, Martin Silva.

Uruguay
BBC Sport
Uruguay

Mwisho wa kipindi cha kwanza

45' Uruguay 1-0 Ureno

Ni Kibarua kwa Cristiano Ronaldo na Ureno kufufua matumaini yao kwenye Kombe la Dunia 2018 kipindi kinachofuata cha pili.

Diego Godin na mabeki wabanifu wa Urguay

43' Uruguay 1-0 Ureno

Mkifunga, ni sifa kwa wafungaji, na msipofungwa, iwe shukrani kwa mabeki!

Uruguay haijafungwa hata goli moja kufikia sasa Kombe la Dunia 2018.

Imeruhusu tu shuti sita dhidi yake hadi sasa.

Isipofungwa bao na Ureno, itafikia rekodi ya Brazil kwa kuwa timu ya Amerika ya Kusini isiyofungwa bao mechi zake 4 za kwanza tangu 1986.

Mlinzi na nahodha wa timu hiyo Diego Godin amewekeza uzoefu wake kikosini na kuwa mkuu wa walinzi wa Uruguay wasioruhusu bao dhidi yao.

Diego Godin
Ge
Diego Godin

Siku ya mbingwa kulishwa upanga?

39' Uruguay 1-0 Ureno

Lionel Messi kwa sasa ni mtazamaji wa Kombe la Dunia akiwa nyumbani.

Je, Cristiano Ronaldo atajiunga naye?

Ureno inadaiwa bao kufuatia kichwa cha Cavani.

Ronaldo hapati raha Uruguay

33' Uruguay 1-0 Ureno

Walinzi wa Uruguay wamkaba Ronaldo. Ana kwa ana naye!

Wakiongozwa na kiungo anayesakwa na Arsenal, Lucas Torreira, mabeki wa Uruguay wanamzuia nyota huyo kuzidisha mabao yake Urusi.

Ronaldo
Getty Images
Ronaldo dhidi ya Uruguay

Frikiki eneo la 'Ronaldo' kwa Ureno

31' Uruguay 1-0 Ureno

Ureno njiani nje ya Urusi. Nani ataiokoa? Fahamu kikosi

26' Uruguay 1-0 Ureno

Safu ya Ureno: Rui Patricio, Ricardo Pereira, Pepe, Fonte, Guerreiro, Bernardo Silva, William Carvalho, Adrien Silva, Joao Mario, Goncalo Guedes, Ronaldo.

Wachezaji wa Akiba: Lopes, Bruno Alves, Fernandes, Joao Moutinho, Andre Silva, Dias, Bruno Fernandes, Gelson Martins, Mario Rui, Quaresma, Cedric, Beto.

Ureno
BBC Sport
Ureno

Cavani aiweka Uruguay kifua mbele.

21' Uruguay 1-0 Ureno

Bao la Edison Cavani dakika ya 7 linakaribia kumuondoa Ronaldo Kombe la Dunia.

Edison Cavani
Getty Images
Edison Cavani