Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Denmark imefuzu robo fainali 1998 tu licha ya mwaka huu kuwa mara yake ya nne baada ya 1986, 1998 na 2002.
 2. Croatia na Denmark hawajapoteza mechi Urusi hadi sasa.
 3. Croatia imeshinda mechi zake zote Kundi G na kumaliza wa Kwanza.
 4. Tulikosea wapi Afrika Kombe la Dunia 2018?

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Raha iliyoje: Rakitic na Croatia robo fainali

Wameifunga Denmark 3-2 hatua ya mchujo.

Croatia imejawa na furaha baada ya kuvuka hatua ya mchujo, hatua pekee iliyowakwaza katika juhudi zao zote za kufanya vyema Kombe la Dunia.

Mnamo 1998, pindi walipovuka hatua hiyo, walimaliza nafasi ya tatu Kombe la Dunia na kusajili matokeo yao bora zaidi Kombe la Dunia.

Kutofanikiwa mechi za mchujo tangu kipindi hicho, imewanyima ufanisi.

Lakini bahati yao imerejea Urusi kwani mkwaju wa Ivan Rakitic, kiungo mahiri wa Barcelona, ulimchanganya kipa Kasper Schmeichel na kuwaliza wapenzi wa Denmark akiwemo babake mdakaji huyo Peter Schmeichel.

Ngoma hiyo ingekamilika mapema baada ya Croatia kupata penalti dakika za mwisho muda wa ziada. Luka Modric alichelea kuwatema Denmark nje ya Urusi.

Baada ya Urusi kuitoa Uhispania, na Croatia kuishinda Denmark, imekuwa mara ya pili mechi za Kombe la Dunia kumalizika ndani ya siku moja kwa mikwaju tangu Juni 21 1986 (Ufaransa V Brazil, Mexico v Ujerumani).

Croatia sasa itachuana na wenyeji Urusi uga wa Olimpiki wa Fisht, Sochi Jumamosi ijayo (7/7/2018).

Rakitic
Reuters
Rakitic

Croatia kukwatuana na wenyeji Urusi robo fainali!

Nani alipoteza, nani alipachika?

 1. Christian Eriksen (Denmark) aliharibu mkwaju wake.
 2. Milan Badelj (Croatia) akakawia kutumia nafasi hiyo, wake pia ukanyakwa.
 3. Simon Kjaer (Denmark) afuta kosa la Eriksen (bao).
 4. Andrej Kramaric aifungia (Croatia)
 5. Matumaini ya Denmark yarejea: Michael Krohn-Dehli (Denmark) hadi wavuni!
 6. Bao! Luka Modric (Croatia) amerekibisha kosa lake la awali.
 7. Puuu...Lasse Schöne (Denmark) akatapatapa na kutupa penalti yake.
 8. Buuuu....Josip Pivaric (Croatia) naye akamzawidi kipa.
 9. Aiiiiiiiiiii......Nicolai Jørgensen (Denmark) amepoteza.
 10. Ivan Rakitic (Croatia) akafunga kazi..Croatia Robo fainali!

Imekamilika 3-2: Ni Croatia V Urusi Robo fainali!

Ivan Rakitic ameipa Croatia ushindi kwa kufunga mkwaju wa mwisho.

N. JØRGENSEN apoteza!

Kasper Schmeichel amfurahisha babake.

2-2 kufikia sasa

Subasic amnyima Schone

Denmark imepoteza penalti ya pili

2-2 Modric amefunga.

Kramaric aifungia Coatia

Simon Kjaer aifungia Denmark

Ni Denmark 1-0 Coatia

Kasper Schmeichel aiokoa Denmark!

Badelj amenoa

Eriksen amepoteza!

Denmark na kibarua!

Mkwaju wake umegonga mhimili wa goli!

Denmark wa kwanza Kupiga.

Mpigaji ni Christian Eriksen.

............anaelekea kwenye doa la kipute......Danijel Subasic langoni

Luka Modric atainusuru Croatia?

Penalti 5 kila Upande sasa.

Croatia imesalia uwanjani kutokana na udhaifu wa Modric kwenye kitovu cha Penalti.

Kasper Schmeichel atakutana tena na kiungo huyu wa Real Madrid.

Luka Modric
EPA
Luka Modric

Kama baba, kama mwana

Ni Penalti sasa: Croatia 1-1 Denmark

Kasper Schmeichel amempiku babake Peter kwa rekodi za kutofungwa mechi Kombe la Dunia.

Kipa huyo wa Denmark (amezuia mechi 2 kati ya 3) kumliko babake Peter (alifanikisha 1 kati ya mechi 5).

Ustadi wake unahitajika sasa na taifa lake, ni matuta matano kwa kila upande!

Kasper na Peter
Getty Images
Kasper na Peter

Modric amekosa!

Kipa Kasper ameondoa!

Majukumu kwa Modric

Penalti kwa Croatia.

Modric
Reuters
Modric

Ni Penalti dhidi ya Denmark!

114' Croatia 1-1 Denmark

Kikosi cha kiki za Penalti?

110' Croatia 1-1 Denmark

Wakufunzi wanaonekana kuwekeza kwenye mikwaju!

Mabadiliko Croatia: Milan badelj amempumzisha Mario Mandzukic.

Denmark: Pione Sisto ameingia nafasi yake Martin Braithwaite.

Penalti zikipigwa............nani bora?

106' Croatia 1-1 Denmark

Penalti zimeanza kunukia mechi hii ya hatua ya mchujo........

Croatia haijawahi kushiriki mikwaju ya penalti mechi za Kombe la Dunia.

Lakini, katika Kombe la mataifa bora Ulaya 2008, iliondolewa na Uturuki baada ya Luka Modric, Ivan Rakitic na Mladen Petric kutofunga. Ni Dario Srna pekee aliwafungia!

Kwa Denmark, wamejaribu bahati mara mbili.

Nusu fainali Kombe la mataifa bingwa Ulaya 1984 dhidi ya Uhispania. Walifungwa 5-4. Preben Elkjaer pekee alipoteza.

Walibahatika mara ya pili walipoilaza Uholanzi 5-4 1992.

Dakika 1 zaidi kuchezwa

106' Croatia 1-1 Denmark

Denmark wapigiwa upatu

105' Croatia 1-1 Denmark

Kila mmoja anaitakia ushindi, lakini kwa nini?

Mashabiki wa Denmark
Getty Images
Mashabiki wa Denmark

Kasper aokoa tena!

104' Croatia 1-1 Denmark

Mshindi kujulikana kwa mikwaju?

99' Croatia 1-1 Denmark

Mara ya mwisho mechi za Kombe la Dunia zilizochezwa siku moja ziliamuliwa kwa penalti ilikuwa tarehe 21 Juni 1986.

Knudsen kurusha, mpira wa Croatia sasa

96' Croatia 1-1 Denmark

Kona Denmark, Croatia wakataa

95' Croatia 1-1 Denmark

Denmark kambini ngome ya Croatia

93' Croatia 1-1 Denmark

Jonas Knudsen jezi nambari 5 amekabidhiwa majukumu ya kuchanja mipira ya kurushwa.

Juma-Penalti?

Muda wa ziada kupigwa: Croatia 1-1 Denmark

Dalili ya mvua mawingu.......

Jumamosi hatukushuhudia mikwajiu kati ya Ufaransa na Argentina, Uruguay V Ureno...lakini Jumapili hii......

Urusi iliing'oa Uhispania kwa matuta. Pande hizo zilitoka sare 1-1 muda wa kawaida pamoja na ule wa ziada.

Kufikia sasa, Croatia na Denmark wanakabana 1-1.

....Na wachezaji 9 kila upande wamecheza dakika 93.

Tutashuhudia penalti tena?

Tusubiri ndani ya dakika hizi 30!

Croatia V Denmark
Getty Images
Croatia V Denmark

Hatari Denmark lakini nje!

93' Croatia 1-1 Denmark

Mechi imekamilika, ni dakika 30 za ziada!

Mabadiliko Croatia

90' Croatia 1-1 Denmark

Croatia imefanya mabadiliko Josip Pivaric amepokea majukumu ya Ivan Strinic aliyejeruhiwa.

Dakika 3 zimeongezwa.

Mateo Kovacic nafuu kwa Croatia

88' Croatia 1-1 Denmark

Mateo Kovacic amerejea licha ya wasiwasi kuhusu kiwango cha maumivu kwenye bega lake.

Mateo Kovacic
EPA
Mateo Kovacic

Mchezaji wa Croatia Mateo Kovacic aumia begani

85' Croatia 1-1 Denmark

Hajamaliza dakika 10 uwanjani, lakini anaonekana kuzidiwa na uchungu.

Unakumbuka yaliyomkuta Mo Salah dhidi ya Real Madrid?

Dakika 10 za kufa kupona Nizhny!

81' Croatia 1-1 Denmark

Pande hizi zimejiandaa kwa dakika 30 za ziada?

Tutafika penalti? Mabadiliko ni kama ifuatayo mechini kwa pande zote.

Croatia:

Mateo Kovacic ameingia nafasi yake Marcelo Brozovic.

Denmark:

Nicolai Jørgensen nguvu mpya pengo la Andreas Cornelius.

Andreas Christensen amempisha Lasse Schöne.

Yurary hatari

77' Croatia 1-1 Denmark

Yussuf Yurary Poulsen wa Denmark amemtengeneza mwenzake Nicolai Jorgensen lakini matokeo ni shuti dhaifu hadi viganja vya Danijel Subasic!

Mabadiliko Croatia

70' Croatia 1-1 Denamrk

Kiungo wa Real Madrid Kovacic amechukua nafasi ya Brozovic.

Denmark dawa ni Davor Suker

69' Croatia 1-1 Denmark

Croatia na Denmark wanaonekana kutoshana nguvu 1-1 hadi sasa.

Lakini mara yao ya mwisho kukutana shindano la kimataifa, Croatia ilishinda 3-0 kwenye hatua za makundi Kombe la Euro 1996.

Davor Suker aliwafunga mabao (2) na Zvonimir Boban (akatandika 1).

Davor Suker
Getty Images
Davor Suker

Injini Eriksen

61' Croatia 1-1 Denmark

Kiungo wa Tottenham Christian Eriksen ndiye mchezaji aliyekimbia zaidi hatua ya mchujo. Amekimbia kilomita 36.

Na anaonekana kuwapokonya Rakitic na Modric utawala wa eneo la katikati uwanjani.

Christian Eriksen
Reuters
Christian Eriksen

Mandzukic amekabwa

59' Croatia 1-1 Denmark

Huduma za mfungaji Mario Mandzukic wa Croatia zinahitajika na wenzake lakini mabeki wa Denmark Jorgensen na Kjaer.

Nestor Pitana apokea sifa

56' Croatia 1-1 Denmark

Refa wa mechi kati ya Croatia na Denmark Nestor Pitana kutoka Argentina ameanza kumiminiwa sifa na mashabiki pamoja na wachanganuzi kutokana na maamuzi yake mechini.

Hajatoa hata kadi moja mpaka sasa!

Refa Nestor Pitana
Getty Images
Refa Nestor Pitana

Ni Kipindi cha Pili

45' Croatia 1-1 Denmark

Kama sio Kasper..............!

Kipa wa Denmark Kasper awanyima Croatia.

Kasper Schmeichel amemzima Ivan Rakitic, akamkataza Ivan Perisic na kuwadumisha Denmark kwenye Kombe.

Kipa huyu ndiye nyota wa timu kufikia sasa.

Kasper Schmeichel
Reuters
Kasper Schmeichel