Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Ubelgiji yadumisha hadhi yake dhidi ya Japan

  Wamefuzu kucheza robo fainali dhidi ya Brazil.

  Kila mmoja amewamiminia sifa wachezaji wa sasa wa kikosi cha Ubelgiji huku wakitabiriwa kuponyoka na Kombe la Dunia 2018.

  Japan ilikaribia kuzamisha ndoto na matumaini ya wachezaji hawa, lakini mwisho wa mchezo, Ubelgiji imedhihirisha kwa nini jina lao linawaacha wapinzani wake bila usingizi.

  Ubelgiji imekuwa timu ya kwanza kutoka nyuma mabao mawili au zaidi na kushinda mechi hatua za mchujo tangu Ureno kuifunga Jamhuri ya Korea 5-3 ngoma ya robo fainali 1966.

  Hii ni baada ya Ubelgiji kuwafikia na kuwafunga Japan licha ya kuachwa nyuma kwa mabao 2-0.

  Red Devils walisawazisha na kuondoka na ushindi wa 3-2 dakika za kukunja jamvi na kuwaacha wengi vunywa wazi.

  Wakati huo huo, Ubelgiji imedumisha rekodi yake ya kutolazwa kwa kusakata mechi 23 bila kufungwa. (Imeshinda mechi 18 na kutoka sare mechi 5). Mara ya mwisho ilipoteza (0-2) dhidi ya Uhispania mnamo Septemba 2016.

  Kabla ya kutemwa, timu nyingine yenye rekodi ndefu ya kutopoteza mechi ilikuwa Uhispania (Imecheza mechi 23 bila kufungwa).

  Je, ni nani atakatiza mbio za wachezaji hawa?

  Kibarua chao cha kwanza ni dhidi ya Brazil Ijumaa wiki hii, wakati watakuwa na fursa nyingine kuwafunga mdomo wakosoaji wake!

  Ubelgiji
  Image caption: Ubelgiji
 2. Kombe la Dakika za lala salama?

  Rekodi ya mabao ya lala salama kuvunjwa Urusi 2018?

  Goli la ushindi la Ubelgiji baada ya dakika 90 ni la 9 kufungwa Urusi 2018 ndani ya dakika hizo.

  Kumbuka, hatujafika hatua za robo fainali!

  Wakati huo huo, ni Magoli 10 tu kwa jumla yalifungwa ndani ya dakika hizo katika Kombe la Dunia (1998, 2002, 2006, 2010 na 2014)!

 3. Waliotua Robo Fainali Urusi kufikia sasa!

  Mechi kuchezwa Ijumaa na Jumamosi wiki hii.

  Ni kina nani wanajitetea kucheza nusu fainali?

  1. Ufaransa
  2. Brazil
  3. Urusi
  4. Croatia
  5. Uruguay
  6. Ubelgiji
 4. Walioliaga Kombe la Dunia mpaka sasa!

  Timu mbili zaidi kutemwa Jumanne.

  Walioondoka:

  1. Argentina
  2. Ureno
  3. Uhispania
  4. Denmark
  5. Mexico
  6. Japan
 5. Xhaka na Shaqiri V Sweden, Harry Kane V Rodriguez Jumanne

  Mechi za hatua ya mchujo Kombe la Dunia!

  Ni nafasi mbili tu zimesalia kwenye ndege ya robo fainali Urusi kufikia sasa.

  Licha ya juhudi zao hatua ya makundi, timu sita tayari zimekwenda nyumbani hadi sasa huku wa mwisho kuondoka akiwa ni Japan.

  Wakati huo huo, timu sita zinajiandaa kucheza robo fainali.

  Siku ya Jumanne, Sweden itagaragazana na Uswizi Krestovsky, mjini Saint Petersburg.

  Mechi ya mwisho siku hiyo itakuwa ni kati ya Colombia na Uingereza uwanja wa Otkrytie Arena, Moscow.

 6. Mbappe, Neymar, Suarez, Hazard ndani ya siku moja!

  Mechi za robo fainali: Uruguay V Ufaransa, Brazil V Ubelgiji

  Ijumaa ijayo itakuwa ni ya kufana kutokana na ratiba ya mechi za Kombe la Dunia.

  Kitakachovutia zaidi ni kuwa mastaa wa kizazi hiki, watakuwa wanawania umaarufu ndani ya siku hiyo kwa kuoneshana ubabe.

  Luis Suarez wa Uruguay na Kylian Mbappe wa Ufaransa watakwatuana uwanja wa Nizhny Novgorod ulioko Nizhny Novgorod katika mechi ya kwanza.

  Suarez, nyota wa Barcelona, amesajili mabao mawili hadi sasa naye Mbappe akiifungia Ufaransa mabao matatu yakiwemo yaliyomtoa Messi kwenye Kombe hili.

  Hapo baadaye Neymar wa Brazil anayepiga PSG na Eden Hazard wa Ubelgiji na Chelsea watatoana jasho ugani Kazan.

  Hata hivyo macho yote kwenye kikosi cha Ubelgiji yatakuwa kwa mshambulizi wa Manchester United Romelu Lukaku anayeshikilia nafasi ya pili orodha ya wafungaji Kombe la Dunia hadi sasa.

  Yote Tisa: Kumi, mastaa wawili watakaofanya vyema ndio watakaokutana nusu fainali na kurefusha muda wa kutawala vyombo vya habari na vinywa vya watangazaji na mashabiki!

 7. Waleteni Brazil!

  Matokeo: Ubelgiji 3-2 Japan

  Mabao ya wachezaji wa akiba wa Ubelgiji Marouane Fellaini Nacer Chadli walioingia dakika ya 65 yamegeuza mchuano wa kukata na shoka ugani Roistov Arena na kuifikisha Ubelgiji robo fainali.

  Red Devils watacheza robo fainali kwa mara ya tatu kwenye historia yao baada ya kufuzu 1986 na 2014.

  Ubelgiji ilihangaishwa mapema kupitia magoli ya Haraguchi dakika ya (48) na Inui kunako dakika ya (52) lakini mabadiliko ya kocha Roberto Martinez yalipindua mchezo.

  Beki Vertonghen alirekebisha kosa lake lililoipa Japan goli la kwanza kwa kupiga kichwa cha maajabu kilichowakanganya wote dakika ya (69).

  Dakika tano baadaye, nguvu mpya Fellaini alifuta uongozi wa Japan na kudumusiha Ubelgiji Urusi.

  Kunako dakika ya 94, Kona ya Japan iligeuka kasoro kwao kwani punde tu ilipopigwa, iligeuka kuwa hasara kwao licha ya kukusanyika kwa lango la Japan.

  Thomas Meunier wa Ubelgiji alichomoka na mpira na kuanza safari iliyoishia pasi kwa Lukaku aliyempisha mwenzake Nacer Chadli kufunga kazi dhidi ya Japan!

  Kwa sasa ni mechi kati ya Neymar na Eden Hazard ugani Kazan siku ya Ijumaa wiki hii.

  Roberto Martinez
  Image caption: Roberto Martinez
 8. Nacer Chadli, bila kuchelewa, aiweka Ubelgiji Robo fainali!

  Mechi Imekamilika: Ubelgiji 3-2 Japan

 9. Lukkkkkkaaaaaakkkkkuuuuuu! Ubelgiji robo fainali!

  93' Ubelgiji 3-2 Japan

 10. Kompany aonywa kwa kumwumiza Yuto Nagatomo

  92' Ubelgiji 2-2 Japan

  Frikiki kwa Japan kupitia Honda!

 11. Kipindi kinazama polepole Rostov Arena

  91' Ubelgiji 2-2 Japan

  Ubelgiji imefika robo fainali 1986 na 2014 pekee!

  Japan haijawahi kufuzu katika historia yake!

 12. Kagawa anagawa lakini......

  90' Ubelgiji 2-2 Japan

  Kagawa
  Image caption: Kagawa
 13. Ni muda wa Marouane Fellaini

  88' Ubelgiji 2-2 Japan

  Aligonga vichwa vya habari kwa kusaini mkataba wa kusalia Manchester United hadi 2020, lakini usiku huu, wahariri wanaandika taarifa tofauti kutokana na bao lake lililoiwezesha Ubelgiji kusalia kwenye Kombe la Dunia kufikia sasa!

  Marouane Fellaini
  Image caption: Marouane Fellaini
 14. Kawashima .......... kawashinda

  85' Ubelgiji 2-2 Japan

  Kipa wa Japan Eiji Kawashima amepangua mipira yote iliyoelekezwa lango la Japan.

 15. Keisuke Honda aingia kuisafirisha Japan

  83' Ubelgiji 2-2 Japan

 16. Ni Roho mdomoni Rostov Arena

  77' Ubelgiji 2-2 Japan

  Kila timu inasaka ushindi, uvamizi baada ya mwingine!

 17. Inui alainisha nyasi kutumia mabeki wa Ubelgiji, Hadi kona....

  75' Ubelgiji 2-2 Japan

 18. Hazard amemtengeneza nguvu mpya Fellaini....2-2

  74' Ubelgiji 2-2 Japan

  ...naye Fellaini ametumia kimo chake kunufaisha Ubelgiji!

 19. FFFFFFFFFFFFEEEEEEEEEELLLLLLAAAAAAINI!

  Ubelgiji 2-2 Japan

 20. Wachezaji wa Ubelgiji wanataka Penalti, lakini ni Kona

  73' Ubelgiji 1-2 Japan