Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Muhtasari

 1. Uingereza imeondoa nuksi ya kutemwa kwa njia ya matuta na kutua robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 2006.
 2. Eric Dier amefunga mkwaju wa ushindi punde tu Kipa Jordan Pickford alipozuia penalti ya Colombia iliyochapwa na Carlos Bacca.
 3. Waliofunga Uingereza: Kieran Trippier, Harry Kane, Marcus Rashford na Eric Dier.
 4. Mateus Uribe ameupigisha mkwaju wake kwenye mwamba wa goli kabla ya mkwaju wa Carlos Bacca kushikwa.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

Mechi za Robo fainali.

Kombe linaingia mapumziko Jumatano na Alhamisi!

Siku ya Ijumaa:

Uruguay v Ufaransa: Uwanja wa Nizhny Novgorod

Brazil v Ubelgiji: Kazan Arena, Kazan

...............

Siku ya Jumamosi:

Urusi v Croatia: Uga wa Olimpiki wa Fisht

Sweden v Uingereza: Samara Arena, Samara

Pickford apangua penalti ya Bacca kuiweka Uingereza robo fainali

UINGEREZA KUCHEZA DHIDI YA SWEDEN JUMAMOSI

Baada ya kungoja zaidi ya dakika 120, hatimaye, timu ya mwisho kufuzu robo fainali Urusi 2018, imefahamika.

Hii ni baada ya Eric Dier kufunga mkwaju wa mwisho punde tu Kipa Jordan Pickford alipozuia mkwaju wa Colombia uliochapwa na Carlos Bacca.

Uingereza imeondoa nuksi ya kutemwa kwa njia ya matuta na kutua robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 2006.

Wakati huo huo, Uingereza imeshinda mechi ya Kombe la Dunia kwa njia ya penalti kwa mara ya kwanza (3-4).

Awali mfungaji bora wa magoli, Harry Kane alitikisa wavu kwa mara ya sita Kombe hili kuiweka three lions kifua mbele dakika ya (57) lakini uongozi huo ulikatizwa kupitia kichwa cha beki Yerry Mina dakika ya (90+3).

Awamu ya mikwaju ya hatua kumi na mbili ilipofika, timu zote zilifunga penalti mbili za kwanza.

Ndoto za Uingereza zilionekana kuzama pale kipa wa Arsenal David Ospina alipopangua mkwaju wa Jordan Henderson uliokuwa wa tatu upande wa Uingereza.

Uingereza ilirudi kwenye Kombe baada ya Mateus Uribe kuupigisha mkwaju wake kwenye mwamba wa goli.

Kieran Trippier wa Tottenham alifufua matumanii ya Uingereza kwa kutandika penalti yake hadi kutulia kimiani.

Wachezaji Eric Dier na Jordan Pickford walitimiza majukumu yao ya kufnga na kuzuia na kuihakikishia Uingereza nafasi kati ya timu 8 zilizosalia Urusi.

Waliofunga Uingereza:

 • Kieran Trippier
 • Harry Kane
 • Marcus Rashford
 • Eric Dier

Waliofunga Colombia.

 • Juan Cuadrado
 • Falcao
 • Luis Muriel

Uingereza itatoana jasho na Sweden ugani Samara, Jumamosi 7/7/2018.

Furaha Uingereza
BBC Sport
Furaha Uingereza

Uingereza V Sweden robo fainali Kombe la Dunia 2018

COLOMBIA 3-4 UINGEREZA

ERIC DIER ..........Aiweka Uingereza Robo fainali

Carlos Bacca wa Colombia apoteza penalti yake!

COLOMBIA 3-3 UINGEREZA

Kieran Trippier ametinga mkwaju wake

COLOMBIA 3-3 UINGEREZA

MATUMAINI YA UINGEREZA IMEREJEA!

Mateus Uribe aharibu mkwaju wake

COLOMBIA 3-2 UINGEREZA

Jordan Henderson amepoteza penalti yake!

COLOMBIA 3-2 UINGEREZA

Luis Muriel kupiga, amefunga

COLOMBIA 3-2 UINGEREZA

Marcus Rashford amefunga penalti ya pili Uingereza

COLOMBIA 2-2 UINGEREZA

Juan Cuadrado amefunga Penalti ya pili Colombia

COLOMBIA 2-1 UINGEREZA

Zamu ya Kaka Kane mbele ya Ospina: Kane amefunga

Uingereza imefunga penalti yake.

Falcao amefunga

Colombia imepata penalti ya kwanza

Falcao dhidi ya Jordan Pickford

Colombia kuanza kupiga.

Urusi na Croatia wametinga robo fainali kupitia mikwaju.

Muda wa mikwaju: Colombia V Uingereza

Colombia kutangulia kupiga mikwaju.

Muda wa mikwaju

Nani atapiga penalti za Uingereza?

Ni kipindi cha mikwaju ya penalti.

Tuliwauliza mashabiki awali.....matokeo ni......

Dele Alli hayumo uwanjani kwa sasa!

Wapigaji wa mikwaju Uingereza
BBC Sport
Wapigaji wa mikwaju Uingereza

Ni Dakika 1 zaidi.

121' Colombia 1-1 Uingereza

Pande zote zimezuia mchezo hadi kuingia kipindi cha penalti.

Sekunde zimesalia uwanjani Spartak.

119' Colombia 1-1 Uingereza

Kieran Trippier ainua, waondolewa!

119' Colombia 1-1 Uingereza

Kwa nini Uingereza inaomba mechi isiingie Penalti?

117' Colombia 1-1 Uingereza

Imecheza mikwaju 3 ya penalti Kombela Dunia, na kupoteza zote!

Colombia V Uingereza: Mechi ya mwisho Uga wa Spartak, Moscow

116' Colombia 1-1 Uingereza

Kiwango cha Mashabiki:: 43,298 na Imezunduliwa: 2014.

Uwanja huu ulifahamika kama Otkritie Arena kabla ya kuitwa Saprtak kwa ajili ya kombe la dunia.

uko Kaskazini Magharibi mwa Moscow na ni uwanja rasmi wa klabu ya Sparak Moscow.

Iliandaa mechi ya kwanza Septemba 5 2014, ambapo Spartak ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Red Star Belgrade.

Rangi za nje za uwanja zinaweza kubadilishwa kulingana na sare za timu zinazochuana.

Colombia wamzindua beki mpya, Zapata

115' Colombia 1-1 Uingereza

Santiago Arias amempisha.

Eric Dier apoteza kichwa wazi!

114' Colombia 1-1 Uingereza

Barrios atoa, kona Uingereza. Roho mdomoni

114' Colombia 1-1 Uingereza

Timu zinaruhusiwa mchezaji mmoja zaidi ndani ya kipindi hiki

113' Colombia 1-1 Uingereza

Kyle Walker amempisha Rashford.

Rose akaribia kuitoa Colombia, kabla ya kombora lake kuchomoka hadi nje

112' Colombia 1-1 Uingereza

Colombia au Uingereza?

108' Colombia 1-1 Uingereza

Colombia imetua robo fainali mwaka wa 2014 pekee.

Uingereza imeshinda mechi mbili za mchujo pekee tangu 1990.

Dier hajadumu kwenye mechi

107' Colombia 1-1 Uingereza

Eric Dier amekamilisha asilimia 28% ya pasi zake tangu alipoingia kwenye mechi.

Dier
EPA
Dier

Vaaaaaaardy...lakini ameotea.

105' Colombia 1-1 Uingereza

Kipindi cha pili muda wa nyongeza

105' Colombia 1-1 Uingereza

Kombe la makinika hadi kipenga cha mwisho kiite!

Takwimu za haraka

Mabao 31 yamepachikwa nyavuni ndani ya dakika 10 za mwisho zikiwemo za ziada Kufikia sasa.

Muda wa mapumziko: Ndani ya kipindi cha ziada

Dakika 15 zimebaki: Colombia 1-1 Uingereza

Mojica aharibu miondoko ya Colombia: Dakika 1 zaidi kuchezwa

105' Colombia 1-1 Uingereza

Falcao...Yadi moja mbali kutoka lango: Onyo Uingereza

103' Colombia 1-1 Uingereza

Johan Mojica aangushwa, mkwaju wa Colombia.

103' Colombia 1-1 Uingereza

Ashley Young nje, Danny Rose ameingia

101' Colombia 1-1 Uingereza

Mabadiliko kikosi cha Uingereza sehemu ya kushoto au wingi ya Ashley Young ya Kushoto.

Miiiiiiiiiiiinnnnaaaaa....lakini hamna kitu!

101' Colombia 1-1 Uingereza

Hatari: Kona nyingine Colombia

100' Colombia 1-1 Uingereza