Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Ubelgiji kuwania nafasi ya 3 Kombe la Dunia 2018.

  Itachuana na atakayepoteza kati ya Croatia na Uingereza Jumatano

 2. Mtaka yote, hu-Henry yote!

  Mfaransa aliyekuwa naibu meneja wa Ubelgiji

  Taifa lake 'alipozaliwa' limetua fainali.

  Waajiri wake ' Ubelgiji' wametemwa nje!

  Thierry Henry
  Image caption: Thierry Henry
 3. Griezmann: Gari la Usafiri Ufaransa

  Amechangia mabao 5 muhimu Ufaransa

  Sio kwa pasi, au kwa goli, kila hatua ya Ufaransa, ina mchango wa Griezmann.

  Achia mbali Mbappe, nyota huyo, hukiuka kimo chake na kubadili mchezo.

  Mengi zaidi ni Jumapili ijayo mjini Moscow kwenye fainali wakati atazidi kuonyesha kwa nini amekabidhiwa majukumu ya kuibeba Ufaransa!

  Griezmann
  Image caption: Griezmann
 4. UFARANSA KUCHEZA FAINALI JUMAPILI

  INAMSUBIRI MSHINDI KATI YA CROATIA NA UINGEREZA

  Bao la beki Samuel Umtiti (dakika ya 51) imetosha kuifikisha Ufaransa fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya tatu (1998, 2006 na 2018).

  Majonzi Ubelgiji
  Image caption: Majonzi Ubelgiji
 5. Mechi imekamilikia: Ufaransa 1- 0 Ubelgiji

  Ufaransa imefika fainali Urusi

 6. Thibaut Courtois akwama na Ubelgiji, Kona Ufaransa

  96' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 7. Mbio za Lukaku kuishia nusu fainali?

  Lukaku
  Image caption: Lukaku
 8. Jan Vertonghen amgota Mbappe

  94' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 9. Thibaut Courtois amkataza Griezmann

  92' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 10. Mbappe awaudhi Wabelgiji, apokea kadi ya njano

  92' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 11. Hata Hazard haamini, lakini 6 dakika zimeongezwa!

  91' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Mabadiliko Ubelgiji: Michy Batshuayi ameingia

  Hazard
  Image caption: Hazard
 12. Ufaransa dakika chache pekee kutua fainali

  89' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 13. Lukakuuuuuuuuuuuuu, amekosa pasi maridadi kutoka De Bruyne!

  88' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

 14. Kante kadi ya Njano kwa kumtuliza Hazard

  87' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Ufaransa hatarini. Frikiki Ubelgiji.

 15. Blaise Matuidi apumzishwa. Corentin Tolisso aingia

  86' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Matuidi
  Image caption: Matuidi
 16. Ufaransa kufungwa sio kazi kazi rahisi?

  84' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Isipokuwa mikwaju ya penalti,

  Ufaransa haijawahi kufungwa mechi 13 za mwisho za mchujo ilizocheza.

  Imeshiriki mechi: 13

  Imeshinda mechi: 10

  Imetoka sare mechi: 2

  Imefungwa mechi: 1

  Ufaransa
  Image caption: Ufaransa
 17. Steven Nzonzi aingia kuziba ufa Ufaransa

  83' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Giroud amempisha kiungo huyu.

 18. Axel Witsel afyatua bonge la kiki, Lloris apangua.

  81' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Wakati huo huo, Hazard na Matuidi wanapokea matibabu baada ya kugongana.

 19. Yannick Carrasco ajaza pengo la Fellaini

  80' Ufaransa 1-0 Ubelgiji

  Dakika 10 za mwisho Ubelgiji kufufua matumaini ya kutua fainali.