Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Croatia yailiza England tena tangu 1990

  Matokeo: Croatia 2-1 England

  Mlinzi John Stones haamini
  Image caption: Mlinzi John Stones haamini

  Croatia imetoka goli moja nyuma na kuchupa hadi fainali ya Kombe la Dunia baada ya kupata mabao mawili kwenye kipindi cha pili katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

  Ndoto za England kufika fainali tangu 1966 zilipata uhai kupitia Kiera Trippier aliyeipa timu yake uongozi dakika ya (5).

  Trippier aliupinda mpira ulioishia kutulia kimiani kupitia mkwaju wa ikabu.

  Pande hizi ziliingia awamu ya mapumziko England ikidumisha goli lake.

  Hata hivyo, Croatia ilirejea kutoka mapumziko na nguvu zaidi na juhudi zao zilizaa matunda pale Ivan Perisic alipoisawazishia dakika ya (68).

  Uzoefu wa mastaa wa timu hiyo wakiwemo Luka Modric, 32, Ivan Rakitic, 30, Ivan Perisic, 29, na mfungaji Mario Mandzukic, 32 uliwafaa kwani walibadili mchezo.

  Mechi iliingia dakika 30 za ziada huku Croatia ikionyesha kutokuwa na uchovu wowote licha ya kucheza hadi hatua ya penalti mechi zake mbili zilizopita.

  Uchungu wa England uliwasili kipindi Mario Mandzukic alipowaacha walinzi wa England wakizubaa na kufyatua mkwaju wake dakika ya (109)

  Mkosi wa nusu fainali umerudi na kuikwaza England tena na sasa timu hiyo itasubiri Qatar 2022 kujaribu bahati yake.

  Kwa upande wake, Croatia imeweka rekodi kwa kufika fainali kwa mara ya kwanza.

  Itakuwa na nafasi zaidi ya kuandika historia itakapokutana na Ufaransa Jumapili.

  Ubelgiji iliyoondolewa na Ufaransa, itakwaruzana na England katika mechi ya kuwasaka washindi wa tatu na wa nne.

 2. Croatia kucheza fainali kwa mara ya kwanza

  CROATIA 2-1 ENGLAND

  Baada ya kutofanikiwa 1998, Croatia imetua fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia yake.

  Croatia kucheza fainali kwa mara ya kwanza
  Image caption: Croatia kucheza fainali kwa mara ya kwanza
 3. CROATIA KUCHEZA NA UFARANSA FAINALI

  MECHI IMEMALIZIKA; CROATIA 2-1 ENGLAND

 4. Mkwaju wenye thamani England.

  122' Croatia 2-1 England

  Milan Badelj ameunawa mpira. Rashford kuleta krosi.

 5. Croatia imesalia na sekunde chache kutua fainali

  122' Croatia 2-1 England

 6. Dele Alli na Rakitic wakabana koo

  121' Croatia 2-1 England

  Dele Alli na Rakitic wakabana koo
  Image caption: Dele Alli na Rakitic wakabana koo
 7. Dakika 3 zaidi kuchezwa.

  120' Croatia 2-1 England

 8. Kramaric akosa goli.

  119' Croatia 2-1 England

 9. Luka Modric ampisha Milan Badelj

  118' Croatia 2-1 England

  Dakika 2 zimesalia

 10. Mkwaju wa ikabu England, Rashford ainua

  117' Croatia 2-1 England

  England inasaka Kona, refa amekataa.

 11. England inacheza na wachezaji 10 baada ya Trippier kuumia

  116' Croatia 2-1 England

  England inacheza na wachezaji 10 baada ya Trippier kuumia
  Image caption: England inacheza na wachezaji 10 baada ya Trippier kuumia
 12. Vedran Corluka ameingia Croatia, kipa Pickford aiokoa England.

  114' Croatia 2-1 England

 13. Mandzukic alivyovunja nyoyo za England.

  113' Croatia 2-1 England

  Mkwaju wa juu uliletwa naye Perisic hakuzubaa kumpiku Mlinzi wa England Trippier.

  Licha ya kuwa kichwa hafifu, iliwaonyoka mabeki akiwemo John Stones ambaye hakujua Mandzukic alikuwa nyuma yake.

  Bila ya kuchelea, mwindaji Mandzukic aliachilia mkwaju kupitia guu lake la kushoto na kumduwaza Pickford.

  Mandzukic alivyovunja nyoyo za England.
  Image caption: Mandzukic alivyovunja nyoyo za England.
 14. Vardy aingia England

  111' Croatia 2-1 England

  Beki Kyle Walker ametolewa.

 15. Mario Mandzukic ndiye mfungaji wa bao la Croatia dakika 109.

  110' Croatia 2-1 England

 16. Mandzukiiiiiiiiic aiweka Croatia mbele!

  105' Croatia 2-1 England

  Mario Mandzukic afunga
  Image caption: Mario Mandzukic afunga
 17. Zamu ya Croatia?

  106' Croatia 1-1 England

  Isipokuwa tishio la Mario Mandzukic, England ilitamalaki awamu ya kwanza katika dakika 30 za ziada Luzhniki.

  Kwa sasa ni kona Croatia, Brozovic amepiga kichwa hadi nje.

 18. Dakika 15 za mwisho kuchezwa.

  105' Croatia 1-1 England

  Wakikosa kufungana, watajitosa kupiga penalti.

 19. Modric na Mpira, anakwenda Modric, aaaaah, Kipenga kimelia.

  Muda wa mapumziko: Croatia 1-1 England

 20. Simba Pickford aiokoa England!

  105' Croatia 1-1 England

  Mario Mandzukic alikaribia kuiliza England kabla ya Pickford kutumia ujasiri na kumzima.