Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Hazard atuzwa mchezaji bora wa mechi.

  Matokeo: Belgium 2-0 England.

  Eden Hazard
  Image caption: Eden Hazard

  Bao, burudani na ubingwa!

 2. Afrika imewakilishwa mechi kati ya Belgium na England?

  Matokeo: Belgium 2-0 England.

  Ndio: Mwamuzi Diedhiou Malang kutoka Senegal amepokea medali kwa kuhudumu kuwa mwamuzi wa nne mechi kati ya Belgium na England kumsaka mshindi wa 3.

 3. Wachezaji wa Belgium kupokea medali kwa kumaliza nafasi ya 3

  Belgium imeifunga England 2-0 kipute cha kuwania nafasi ya 3.

 4. Achia mbali Taji, hata tatu wamekosa England.

  Mechi imekamilika: Belgium 2-0 England

  Ngoma imekatika St. Petersburg na Belgium ndio timu ya 3 Kombe la Dunia 2018.

  Mabao ya Thomas Meunier na Eden Hazard yameilazimu England kujituliza na nafasi ya 4.

  Pole kwa Eric Dier
  Image caption: Pole kwa Eric Dier
 5. Hatari Hazard na Belgium wamaliza wa tatu Kombe la Dunia 2018

  Matokeo: Belgium 2-0 England.

  Eden Hazard: Mechi 25 na maehusika ufungaji wa mabao 25.

  Amefunga 12, na kutoa pasi za usaidizi 13.

 6. Dakika 3 zaidi, zitaitosha England?

  90' Belgium 2-0 England

 7. Hatimaye Hazard aamua hatma ya Harry na England!

  83' Belgium 2-0 England

  Hazard
  Image caption: Hazard

  Ni Rasmi: Bao la pili la Belgium lililopachikwa na Hazard limbadili mambo!

  Ubelgiji kumaliza nafasi ya 3 Kombe la Dunia 2018.

  England kumaliza wa nne.

  ...................iwapo hakutakuwa na miujiza, mambo yatakuwa namna hiyo!

 8. Hazaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaard. Belgium na la Pili!

  Belgium 2-0 England

 9. Kipa Pickford apiga 'save' ya mwaka

  79' Belgium 1-0 England

 10. Post update

  Kieran Trippier
  Image caption: Kieran Trippier

  Kieran Trippier anazidi kupongezwa mechini kwa jinsi anavyochanja krosi zake.

  Ni muda tu kabla ya kusababisha goli mechi hii.

 11. Frikiki England, Maguire apiga nje

  74' Belgium 1-0 England

 12. De Bruyne dawa ya England?

  70' Belgium 1-0 England

  De Bruyne
  Image caption: De Bruyne
 13. Kompany amuangusha Rashford, uhasimu wa Machester huu au?

  70' Belgium 1-0 England

 14. Dier anyimwa goli na Toby!

  69' Belgium 1-0 England

 15. Harry Kane kujilaumu akikosa kiatu cha dhahabu 2018!

  Romelu Lukaku ametoka nje kumaanisha Kane anaandamwa na Mbappe na Griezmann pekee kinyang'anyiro cha kuwania kiatu cha dhahabu.

 16. Hatari Belgium, mawasiliano duni yasababisha mpira kutoka nje

  67' Belgium 1-0 England

  England imeponea.

 17. Kona ya England, Sterling nje.

  65' Belgium 1-0 England

  Rashford apewa muda zaidi mechini kwa kujaza pengo la Sterling safu ya England

 18. Belgium yasaka ushindi wa 6 Kombe la Dunia 2018

  63' Belgium 1-0 England

  Iwapo Belgium itashinda leo, wataondoka Urusi wakiwa na ushindi mechi 6 ikiwa ni rekodi bora kuliko mafanikio yake 2014 nchini Brazil waliposajili ubingwa mechi 4 tu.

 19. Delph azuia pasi nzuri kutoka Hazard

  62' Belgium 1-0 England

 20. Hatari England, Vertonghen aondoa

  50' Belgium 1-0 England