Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Asante kwa kuwa nasi Kombe la Dunia 2018!

  Pongezi Ufaransa, wewe shabiki pia!

  Imekuwa ni faraja kuwa nawe makala ya 21 Kombe la Dunia, nchini Urusi 2018 hadi mshindi, Ufaransa alipokabidhiwa taji lake ugani Luzhniki.

  Limekuwa ni Shindano lenye mvuto, timu 32, mechi 64 kwa jumla zikipigwa na kushuhudia hisia tofauti.

  Tunashukuru mchango wako kwenye kurasa zetu za Facebook na Twitter.

  Kumalizika kwa Kombe hili ni ishara kuwa sasa ndio mwanzo wa msimu wa ligi za bara ulaya na macho yote sasa yataelekezwa kwa vilabu vya soka.

  Dirisha la uhamisho limefunguliwa, na mastaa wameanza kuingia au kubanduka.

  Tutazidi kukuletea taarifa zaidi kuhusu Kombe lililokamilika kwa kuangazia Ufaransa itakavyokaribishwa nyumbani, taarifa za wakufunzi kupigwa kalamu na wachezaji kustaafu.

  Zidi kuwa nasi kwenye mtandano huu wetu kwa habari zaidi za spoti.

  Shukran na hadi Qatar 2022, panapomajaliwa, kwaheri!

 2. Mshindi wa Kombe la Dunia bila kugusa mpira

  ..........Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.

  Adil Rami, beki wa Ufaransa amepokea medali ya dhahabu kwa kubeba Kombe la Dunia na timu yake licha ya kutoingia uwanjani au hata kugusa mpira!

  Mpenzi wa Pamela Anderson, alikuwa kikosini.......akila starehe tu!

 3. Croatia imeondoka Urusi kwa kuweka rekodi........

  ....................itasalia kwenye kumbukumbu

  • Croatia ni timu ya kwanza kupoteza fainali ikicheza kwa mara yake ya kwanza tangu timu ya Uholanzi 1974 (2-1 v Ujerumani).
  • Mandzukic ni mchezaji wa kwanza kujifunga bao fainali ya Kombe la Dunia.
  • Perisic ni kiungo wa pili historia ya Kombe la Dunia kusababisha penalti na kisha kufunga goli tangu Marco Materazzi wa Italia mnamo 2006.
  • Mandzukic ni mchezaji wa pili katika historia ya Kombe hilo kutinga goli na kujifunga tangu Ernie Brandts wa Uholanzi wakichuana na Italia 1978.
  • Mandzukic ni wa tano kufunga goli fainali ya Kombe la Dunia na ya Champions League tangu Ferenc Puskas, Zoltan Czibor, Gerd Muller na Zinedine Zidane.
 4. Ufaransa: Heri Ubingwa kuliko Burudani bila ufanisi

  Ufaransa imeshinda Kombe la Dunia licha ya kutoburudisha!

  Ufaransa ilizifunga Australia na Peru kabla ya kulazimishwa sare 0-0 na Denmark hatua yamakundi.

  Baadaye kikosi cha Didier Deschamps kilifanikiwa kuiadhibu Argentina mechi iliyoshuhudia mabao 7 hatua ya mchujo kabla ya kuzinyamazisha Uruguay na Ubelgiji mechi za robo fainali na nusu fainali mtawalia.

 5. Croatia: Inauma lakini tunajivunia.

  Wamefungwa 4-2 na Ufaransa

  Croatia ni taifa lenye idadi ndogo ya watu kuwahi kufika fainali ya Kombe la Dunia tangu Uruguay 1950.

  Croatia imefungwa na Ufaransa 4-2 fainali lakini imeimarika kutoka matokeo yake ya awali ya 1998 ilipomaliza nafasi ya 3.

  Naibu kocha wa Croatia Drazen Ladic ameelekeza kidole cha lawama kwa goli la penalti la Antoine Griezmann kwa kuwavunja moyo.

  "Kwanza kabisa ningependa kuipongeza Ufaransa. Tunahisi uchungu lakini pia tunajivunia," alisema. "Tulilenga kubeba Kombe la Dunia lakini ndio soka ilivyo. "Ufaransa haikutushangaza,tuliachia mabao mepsi mno ikiwemo penalti na goli la kujifunga."

 6. Deschamps awazima wakosoaji wake

  Didier Deschamps ajikusanyia sifa kedekede kwa ustadi wake!

  Waliomuamini walikuwa wachache, na hakuwa na kazi rahisi Urusi.

  Akilini aliwaza....na kusema....'Kelele za mlango haziniwasi usingizi'.

  Deschamps ni mtu wa tatu kuwahi kunyanyua taji la Kombe la Dunia akishikilia nyadhifa tofauti: Ameinua akiwa mkufunzi 2018 baada ya kufanya hivyo 1998 akiwa nahodha wa Ufaransa.

  Kwa sasa anaweza kumithilishwa na magwiji Mario Zagallo na Franz Beckenbauer wawili walioandikisha rekodi aina hiyo.

  Zagallo alifanikisha haya akiwa mchezaji Brazil 1958 na 1962 kabla ya kuliongoza taifa lake kuifunga Italia 1970 akiwa Mkufunzi.

  Mjerumani Beckenbauer aliiwezesha Ujerumani Magharibi kubeba Kombe la Dunia 1874 akiwa mchezaji kabla ya kuiletea ufanisi akiwa kocha wake 1990 wakati timu yake iliiadhibu Argentina 1-0.

  Tukubali.....kelele za mwenye nyumba hazimuudhi mgeni kulala.....

  Didier Deschamps
  Image caption: Didier Deschamps
 7. Pogba na Ufaransa wafuta chozi la 2016

  Walipoteza Kombe la Euro kwa Ureno mbele ya mashabiki wa nyumbani.

  Paul Pogba akihuzunika 2016
  Image caption: Paul Pogba akihuzunika 2016

  Ubingwa wa Dunia 2018 nchini Urusi umerudisha tabasamu nyuso za mashabiki wa Ufaransa!

 8. Rais Emanuel Macron wa Ufaransa ajiunga na sherehe

  Kwa nini Rais pia asisherekee?

  Rais wa Ufaransa Emanuel Macron
  Image caption: Rais wa Ufaransa Emanuel Macron
 9. Thibaut Courtois mdakaji bora duniani 2018

  Amefungwa magoli 4 pekee mechi 3 za mchujo.

  Kipa wa Ubelgiji na Klabu ya Chelsea Thibaut Courtois ndiye kipa bora wa Kombe la Dunia 2018.

 10. Kylian Mbappe kinda bora duniani 2018

  Mbappe ametuzwa kwa kuisaidia Ufaransa

  Baada ya kuwa Chipukizi wa kwanza kufunga goli fainali ya Kombe la Dunia tangu Pele 1958, na nyota mwenye umri mdogo kufunga magoli mawili Kombe la Dunia tangu Pele wa Brazil dhidi ya Sweden 1958.

  Mbappe alifunga mabao yake dhidi ya Argentina mechi ya mchujo.

 11. Luka Modric ndiye mchezaji bora 2018

  Nahodha wa timu ya Croatia atunukiwa kwa ustadi wake Urusi

 12. Harry Kane ajinyakulia kiatu cha dhahau

  Amefunga mabao 6 mpaka sasa!

  Nypota huyo wa Uingereza ndiye mfungaji bora Kombe la Dunia 2018

 13. Modric akosa medali, ajizolea sifa Urusi 2018

  Nahodha wa timu ya Croatia iliyofungwa na Ufaransa

  Modric ni mmoja wa nyota waliong'aa Kombe la Dunia 2018.

  Luka Modric
  Image caption: Luka Modric
 14. 2018 ni mwaka wa Ufaransa

  Ufaransa imeshinda Kombe kwa kuizima Croatia 4-2.

  Mabingwa wa Kombe la Dunia 2018
  Image caption: Mabingwa wa Kombe la Dunia 2018

  Ufaransa mabingwa wa dunia kwa mara yao ya pili tangu 1998.

  Mnamo 2006 walimaliza nafasi ya pili baada ya kulazwa na Italia.

  Wamewahi kushika nafasi ya 3 mnamo 1958 na 1986!

 15. Habari za hivi pundeUFARANSA MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2018

  WAMEIFUNGA CROATIA 4-2 LUZHNIKI 2018

 16. Ufaransa ni moto kwenye fainali!

  93' Ufaransa 4-2 Croatia

  Ufaransa ni timu ya kwanza tangu Brazil 1970 kufunga mabao 4 mechi ya fainali Kombe la Dunia.

 17. Pogbaaaaaaa, hatari, amekosa la 5!

  92' Ufaransa 4-2 Croatia

 18. Paul Pogba pia aweka historia

  90' Ufaransa 4-2 Croatia

  Paul Pogba ni mchezaji wa kwanza anayepiga ligi ya Uingereza kufunga goli Kombe la Dunia tangu Emmanuel Petit , 1998.

  Dakika 5 zaidi kuchezwa mechi hii.

 19. Nikola Kalinic: Mchezaji wa Croatia mwenye uchungu

  88' Ufaransa 4-2 Croatia

  Mfungaji wa Croatia Nikola Kalinic alifurushwa kutoka kikosi cha timu hiyo baada ya kukataa kuingia mechi waliyoisambaratisha Nigeria 2-0.

  Alisalia kwenye benchi licha ya kupiga jaramba na kusema kuwa alikuwa na jeraha la bega.

  Kuondoka kwake iliiathiri Croatia ambayo haikuruhusiwa kujaza pengo aliloliacha na kusalia na wachezaji 22.

  Wenzake wameweka historia kwa kusakata mechi muhimu maishani mwao huku akijiunga na mashabiki kufuatilia fainali.

  Amepachika mabao 15 mechi 41 akiiwakilisha taifa lake.

  Ni mshambulizi wa zamani wa Blackburn anayeitumikia AC Milan kwa sasa.

 20. Siku ya Didier Deschamps.........

  86' Ufaransa 4-2 Croatia

  Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps, kuweka historia kwa kuwa mtu wa tatu kubusu Kombe la Dunia akiwa mchezaji na mkufunzi.