Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

 1. Tottenham yamsaini Giovani Lo Celso

  Tottenham imethibitisha kumsajili kiungo wa kati Giovani Lo Celso kutoka klabu ya Uhispania ya Real Betis kwa mkopo wa muda mrefu kukiwa na uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa kudumu.

  View more on twitter
 2. Habari za hivi pundeMbwana Samatta akosa kujiunga na Klabu ya England

  Mshambuliaji wa klabu ya Genk nchini Ubelgiji na nahodha wa timu ya taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta amekosa kujiunga na klabu ya England baada ya dirisha la uhamisho la taifa hilo kufungwa rasmi.

  Samatta ambaye kulingana na gazeti la The Sun la England ana thamani ya pauni milioni 12 bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

  Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley.

  Samatta
 3. Habari za hivi pundeCaroll arudi Newcastle

  Mshambuliaji wa zamani wa England Andy Carroll amerudi katika klabu yake ya utotoni miaka minane baada ya kuondoka.

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 , aliachiliwa na kuwa mchezaji huru na klabu ya West Ham msimu huu kufuatia kandarasi ya miaka sita iliokumbwa na majereha.

  Ametia kandarasi ya mwaka mmoja.

  Caroll
 4. Dirisha la uhamisho lafungwa

  Dirisha la uhamisho hatimaye limefungwa .

  Hatahivyo haimaanishi kwamba hakutakua na matangazo yoyote.

  Mikataba kadhaa huenda imeidhinishwa na tutaisikia saa moja lijalo.

  Mashabiki wa Arsenal wanasubiri kwa hamu habari kuhusu uhamisho wa David Luiz.

 5. Habari za hivi pundeKieran Tierney ajiunga rasmi na Arsenal

  Sasa ni rasmi beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney atajiunga na Arsenal

  Kieran Tierney
  View more on twitter
 6. Habari za hivi pundeRomelu Lukaku ajiunga na Inter Milan

  Inter Milan wametuma ujumbe wa twitter ulio na kanda ya video ya Lukaku akiwa amevalia jezi ya timu hiyo akisema ''Inter sio ya kila mtu ndio sababu niko hapa''

  Romelu Lukaku ametia kandarasi ya hadi tarehe 30 Juni 2024.

  Lukaku sasa atakuwa mchezaji wa tatu aliye ghali zaidi kusajiliwa na ligi ya Serie A kufuatia uhamisho huo wa dau la £74m move to Inter Milan.

  Wachezaji wengine waliosajiliwa kwa dau la juu zaidi ni Cristiano Ronaldo (£99.2m) aliyejiunga na Juventus na Gonzalo Higuain (£75.3m) .

  View more on twitter
 7. Austin kuelekea West Brom

  West Brom imemsajili mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin kwa dau la £4m.

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaelekea katika ligi hiyo baada ya misimu mitatu na nusu akiichezea St Mary, ambapo aliichezea mara 81 na kufunga magoli 20.

 8. Habari za hivi pundeTottenham yamsajili rasmi Sessegnon

  Tottenhm yamp[atia mkataba aliyekuwa winga wa Fullham
 9. Crystal Palace kutafuta mchezaji atakayechukua mahala pake Zaha

  Crystal Palace imewasilisha ombi la kumsaini mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Jean-Kevin Augustin iwapo mktaba wa siku ya mwisho itaafikiwa kumnunu winga wake Wilfried Zaha, kulingana na Sky Sports.

  Wlfried zaha
 10. Habari za hivi pundeDjibril Sidibe ahamia Everton kutoka Monaco

  Everton imeafikia makubaliano na beki wa Ufaransa Djibril Sidibe kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Monaco.

  Everton ina mbadala ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu huu.

  Sidibe alishinda taji la ligi ya daraja la kwanza na Monaco katika msimu wa 2016-17 na alikua miongoni mwa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe La dunia nchini Urusi mwaka uliopita.

  Amefunga magoli sita katika mechi 114 akiichezea Monaco tangu ajiunge na lille 2016.

  Djibril Sidibe
 11. Herrera apata pigo!

  Ander Herrera atalazimika kusubiri kwa muda zaidi ili kuanza kuichezea PSG.

  Mchezaji hyo wa zamani wa Man Uniuted ametuma ujumbe wa twitter wa picha yake akipokea matibabu ya jeraha la mguu alilopata katika mazoezi siku ya Jumatano, ambalo litamweka nje kwa wiki nne au tatu.

  View more on twitter