Huwezi kusikiliza tena

TeknoMaarifa

Makala ya TeknoMaarifa, inatathmini simu mpya aina ya iPhone 4 iliyozinduliwa mwezi Juni. Simu hiyo inayogharimu zaidi ya dola 750, imepata kushabikiwa kila inakouzwa kama ilivyokuwa kwa nyingine za iPhone zilizotangulia, lakini imekosolewa vikali kutokana na matatizo ya kupoteza mawasiliano ya mazungumzo, hasa ikishikwa sehemu yenye antena.

Kampuni ya Apple, inayounda simu hiyo, ililazimika kutoa makasha maalum bure kwa wanunuzi wa iPhone 4 kuepusha tatizo hilo la mawasiliano kukatika. Hassan Mhelela anasimulia zaidi katika TeknoMaarifa.