Historia ya BBC World Service

Imebadilishwa: 28 Februari, 2012 - Saa 18:59 GMT

Historia ya BBC World Service

 • Kuingia Bush house

  Shirika la BBC World Service linasherehekea miaka themanini ya matangazo yake ya kimataifa. Tafadhali bonyeza hapa uweze kuona hifadhi ya kumbukumbu muhimu za BBC.

 • Mkurugenzi mkuu wa BBC wakati huo John Reith

  Siku ya kwanza ya matangazo ya himaya ya kiingereza

  BBC ilianza rasmi matangazo yake mwezi Disemba mwaka 1932 kwa redio ya masafa mafupi.

 • Mfalme George wa tano.

  Hotuba ya Mfalme

  Siku sita baada ya kufunguliwa rasmi kwa idhaa ya himaya ya kiingereza, ndio ulikuwa mwanzo wa utangazaji, huu ndio ulikuwa ujumbe wa Krismasi wa himaya ya Uingereza. Hotuba ilitolewa na Mfalme George wa tano, moja kwa moja kutoka katika nyumba ya familia ya kifalme ya mapumziko Norfolk mjini Sandringham. Maneno hayo yaliandikwa na mshahiri na mwandishi Rudyard Kipling na hivvi ndivyo hotuba ilivyoanza: " Nazungumza nanyi kutoka nyumbani kwangu maneno haya yakitoka rohoni mwangu." Hivi ndivyo mkurugenzi mkuu wa wa BBC John Reith aliandika katika kitabu chake cha kumbukumbu: " Huu ndio ulikuwa ufanisi mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya BBC. Mfalme alisikika kote duniani.

 • Generali Charles de Gaulle

  Vive le Gerale

  Serikali ya UIfaransa ilisalimu amri kwa utawala wa Nazi wa Ujerumani mwezi Juni mwaka 1940. Kiongozi wa vuguvugu la 'Free French' Generali Charles De Gaulle, alipeperusha matangazo hadi nchini Ufaransa, kutoka chumba cha matangazo cha B2, katika Broadcasting House. Wafanyakazi waliambiwa kuwa generali ambaye hakutajwa, alikuwa anakuja Broadasting House. Hata hivyo hotuba yake haikurekodiwa na ilibidi kurejelewa, kitu kilichomkera generali huyo. Aliendelea kutangaza kwa dakika tano kila usiku kwa miaka minne. Kulingana na mwandishi mmoja wa idhaa ya kifaransa, hakuwahi kusikia generali huyo akikosea hata kidogo katika matangazo yake. Alikuwa mkarimu na kila baada ya matangazo alimshukuru fundi wa mitambo.

 • Mhariri msaidizi wa idhaa ya kiarabu D Stephenson (mkono wa kushoto)

  Mwanzo wa idhaa za lugha.

  Vita vya pili vya dunia vilichochea kubadilishwa kwa jina la idhaa ya himaya ya Kiingereza, na sasa ikajulikana na idhaa ya kimataifa Novemba mwaka 1939 na kueneza matangazo yake kwa luhgha tofauti kama vile Kiarabau, Kihispania, Kijerumani , Kiitaliano, Kifaransa, Kiafrikaan, Kihispania kwa nchi za Uropa na Kireno kwa nchi za Ulaya. Mwishoni mwa mwaka 1940, BBC ilikuwa inatangaza katika lugha thelathini na nne. Kila siku kulikuwa na matangazo sabini na nane ya habari ikiwa ni maneno 250,000 kila siku. Idhaa zingine mpya zilizoanza kupeperusha matangazo yao ni pamoja na idhaa ya Iceland, Albania, Kihindi, Burmese na Lugha inayozungumzwa mjini Luxembourg.

 • Kitengo cha BBC kufuatilia matangazo

  War of words

  Ofisi za BBC ziliweza kupatikana Broadcasting House, Oxford Street na katika Senate House. Idhaa mpya ya kimataifa sasa iliweza kupata nguvu baada ya serikali ya Uingereza kugundua umuhimu wa utangazaji. Mwaka 1941, kulikuwa na zaidi ya wafanyakazi 1400. Mwaka huo mbunge wa eneo bunge la Derby, Phillip Noel_Baker, katika mjadala bungeni, alisema "sidhani waziri atatofautiana nami nikisema kuwa katika njia zote alizonazo za kuwafikia watu barani Ulaya, utangazaji ndio njia bora zaidi."

 • Uharibifu uliosababishwa na mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini dhidi ya jengo la Bush House

  Kuhamia Bush House

  Nafasi ya utangazaji kwa idhaa nyingi za BBC, ilikuwa inapungua kule Broadcasting House. Wakati bomu la kutegwa ardhini lililipuka nje ya Broadcasting House mwaka 1940, ilisababisha moto uliodumu saa kadhaa na kusababisha uharibifu mkubwa. Idhaa za Ulaya zikalazimika kuhamia Maida Vale kaskazini magharibi mwa London ambapo walitangazia kutoka kwa chumba kidogo. Mwaka 1941, idhaa hizo zilihamia Bush House, katika barabara ya Fleet Street kitovu cha viwanda vya kuchapishia magazeti wakati huo ikitozwa kodi ya pauni thelathini kila wiki.

 • Julai 1941: Picha ya mwanamke anayeuza mauwa yakiwa yametengezwa mfano wa herufi 'V'

  Ishara ya uasi

  Mwezi Januari mwaka 1941, mkurugenzi wa idhaa ya kifaransa ya Ubelgiji, Victor de Laveyele, aliwashauri wasikilizaji wa idhaa hiyo kutumia herufi 'V' kama ishara ya ushindi dhidi ya vikosi vya kigeni. Na mara tu herufi hii ikaanza kuchorwa kwenye kuta nchini Ubelgiji, Uholanzi na Ufaransa. 'V' sasa ikaanza kutumiwa kama ishara ya kupiga simu katika idhaa zote za BBC zinazopeperusha matangazo Ulaya. Pia ilikuwa inafanana na mwanzo wa simfoni ya tano ya Beethoven. Baadaye mwaka huo, Churchhill aliitumia ishara hiyo kwa mara ya kwanza, katika hotuba yake ya ushindi tarehe kumi na tisa mwezi Julai mwaka 1941.

 • Baadhi ya wapiganaji wa Ufaransa wakisikiliza matangazo

  Ishara za siri

  Wakati wapiganaji waliokuwa wanapinga vikosi vya kigeni barani Uropa, walipojaribu kukabiliana na vikosi hivyo, idhaa hiyo iliwatangazia ujumbe wa siri. Ujumbe huo haukueleweka mfano ''Le lapin a bu un aperif'' ( kwamba sungura alikunywa kinywaji cha aperitif), au '' mademoiselle caresse le nez de son chien'' ( kwamba mademoiselle anapapasa pua la mbwa wake). Huu ujembe ulikuwa unaawambia wapiganaji kuwa ikiwa oparesheni ilikuwa iendelee au ikiwa imesitishwa au ikiwa watu ama stakabadhi zilikuwa zimefika.

 • CD Adamson, fundi wa mitambo wa BBC

  Utangazaji vitani.

  Waandishi wa BBC kuhusu vita, kama vile CD Adamson, katika picha hii, walituma ripoti zao kutoka msitari wa mbele wa vita katika rekodi. Mwandishi mwingine Godfrey Talbot, alituma ripoti kuhusu ushindi wa kwanza wa washirika, El Alamein, mwaka 1942 akiwa juu ya lori moja ijulikanayo kama Belinda ambayo ilikuwa imebadilishwa na kuwa chumba cha kupeperushia matangazo. Afisaa mmoja wa jeshi alikuwa naye kuweza kubana baadhi ya taarifa hizo na kisha kupeleka habari zake mjini Cairo ili kuweza kupeperushwa hadi London.

 • George Orwell

  Waandishi wa Bush House

  Kutoka mwaka 1941 hadi mwaka 1943, George Orwell alifanya kazi kama mtayarishaji wa kipindi katika idhaa ya mashariki. Hakufurahia kazi yake na ilipofika mwaka 1944, aliandika "huenda nikarejelea maisha yangu, na kuweza kuandika kitu muhimu. kwa sasa mimi ni kama chungwa ambalo limekanyagwa na kiatu kichafu sana" Lakini kazi yake katika BBC ilimsaidia kuweza kuandika kitabu chake, mwaka 1984 ambacho inasemekana alitoa mawazo yake mengi kutoka maisha yake BBC.

 • Idhaa ya kirusi mwaka 1964

  BBC wakati wa vita baridi

  Baada ya vita baridi, uhusiano na utawala wa Strelin ulianza kudorora huku ukuta wa chuma ukiwekwa kati yao. Februari mwaka 1946, wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza, iliitaka BBC kuanzisha idhaa ya kirusi na mwezi mmoja baadaye ikaanza kupeperusha matangazo yake. Mwanzoni wasikilizaji wa Urusi waliweza kusikiliza idhaa hiyo bila wasiwasi lakini punde vita baridi vilipokuwa vinaendelea, serikali ya Urusi ikaanza kudhibiti hali. Matangazo yalianza kuingiliwa, hitilafu za kila mara zikiripotiwa na hivyo BBC ikalazimika kuongeza nguvu za mitambo yake.

 • Waziri mkuu Anthony Eden

  Kuhifadhi uwazi.

  Wakati wa kutangaza mzozo wa Suez mwaka 1956,waziri mkuu wa Uingereza Anthony Eden, aliamini kuwa idhaa ya kiarabu, inapaswa kutangaza kwa kupendelea majeshi ya Uingereza. Idhaa hiyo nayo iliendelea kutangaza bila mapendeleo kwa usaidizi wa mkurugenzi mkuu Ian Jacob licha ya wizara ya mambo ya kigeni kusema kuwa itapunguza mamilioni ya dola ambazo BBC ilikuwa inapokea kama ufadhili. Katika wiki chache zilizofuata, licha ya vitisho vya waziri na wabunge, BBC ilisisitiza msimamo wake ya kutopendelea upande wowote.

 • Mwanaume aliyezingirwa na kikundi cha watu wakichoma picha ya Stalin

  Ujumbe wa binafsi

  Baada ya jeshi la kisovieti kuzima mapinduzi ya kiraia ya Hungary mwaka 1956, idhaa ya BBC ya Hungary, ilitangaza ujumbe wa kibinafsi kutoka kwa wakimbizi waliokuwa wamekimbilia Uingereza. Wakimbizi hao walitumia majina ya siri kuhakikisha maafisa wa Hungary hawatotambua familia zao. Wakati huo baadhi ya vituo vya radio vilitangaza kuwa wakimbizi hao watapokea msaada, BBC ilitangaza kwamba , nchi za Magharibi zitatoa msaada wa kisaikolojia wala sio wa kijeshi.

 • Mmwanmke akitizama transista za redio

  Mageuzi ya Transista

  Miaka ya tisini, ilikuwa miaka ya kueneza umiliki wa redio, hasa baada ya kuzinduliwa kwa betri ambazo zingewezesha transista kufanya kazi. Kati ya mwaka 1955 na 1965, umiliki wa redio ulipanda katika nchi za kikomunisti mashariki mwa Ulaya na kuongezeka hata maradufu mashariki ya kati, China , nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na nchini India. Mwezi Mei mwaka 1965, iligeuzwa na kuwa World Service kuweza kuonyesha umaarufu wake wa maswala ya dunia.

 • Kidude chenye sumu hiyo kali.

  Kuhusu vitabu vya kijasusi mwaka 1978, mwandishi katika idhaa ya Bulgeria, Georgi Markov alipokuwa anaelekea kazini Bush House, akiwa katika eneo la Waterloo Bridge. Alihisi uchungu katika paja lake. Alipogeuka alimwona mtu akiokota

  mwavuli lakini Markov aliendelea na safari yake kwenda Bush House. Baadaye siku hiyo aliugua na kufariki siku tatu baadaye. Uchunguzi uliofanyiwa mwili wake uligundua kidude kidogo katika paja lake. Inaamika kidude hicho kilikuwa na sumu kali. Ilibainika baadaye kuwa polisi wa siri wa Urusi waliunda mwavuli ulioweza kumdunga mwathirika simu hiyo.

 • Vacla Havel mwaka 1978

  Mpinzani kugauka rais

  Matatizo ya kuripoti nyuma ya ukuta wa chuma wakati wa vita baridi, yanaelezewa bayana hasa baada ya kutibiwa kwa Vaclav Havel, raia wa Czechslovakia na mwandsihi wa michezo ya kuigiza,ambaye alikuwa rais wa nchi hiyo baada ya utawala wa kisovieti. Katika juhudi za kumnyamazisha, maafisa wa utawala walimpiga maruku kumiliki simu. Pia alichunguzwa kwa karibu sana na polisi wa kisiri. Lakini BBC iliweza kupata njia ya kuongea naye kupitia simu ya jamii iliyokuwa karibu na alipoishi na kumfanyia mahojiano. Aliweza kupiga simu kupitia Posta ili kuweza kufanya mahojiano hayo.

 • Kijana mdogo anamsaidia mwanjeshi wa Uingereza kubeba vifaa vyake

  Kupiga simu katika Falklands

  Wakati Argentina ilipovamia Falklands mwaka 1982, kipindi cha kila wiki cha BBC "calling the Falklands" ndio iklikuwa njai ya pakee ya watu wa kisiwa hicho kuwasiliana. wansiasa wakuu walialikwa kwenye kipidni hicho, huku mwandishi wa idhaa ya Amerika ya kusini, Harold Briley, akisifika sana kwa sababu ya ripoti zake za kila mara. Kama vile tu wakati wa mzozo wa Suez, BBC ilishutumiwa sana. Waziri mkuu Margaret Thatcher, alisema " kuna wakati ambapo itaoneakana kama sisi na watu wa Argentina tuko sawa. Serikali ya Uingereza ilichukua sehemu ya masafa ya BBC kutangza vita vya kisaikolojia kwa wanajeshi wa Argentina. Hata hivyo idhaa ya Amerika kusini iliendelea kupeperusha matangazo yake bila mapendeleo kwa kutaja vita hivyo kama vya Falkalands au Las Islas Malvina kila wakati walipotaj vita hivyo hewani.

 • Polisi wa Kisovieti mbele ya jengo la KGB

  Mafunzo ya kiingereza

  BBC ilichukua jukumu la kuwafunza maafisa wa KGB. Oleg Gordievsky aliyekuwa jasusi, alielezea kuwa majasusi waliokuwa wanafunzwa kiingereza waanze kwa kusikiliza matangazo ya habari ya BBC, lakini mwanzo lazima kila kilichokuwa kinapinga utawala wa kisovieti kuondolewa kwenye matangazo hayo. Alisema " nasisitiza umuhimu wa BBC katika utawala wa kisovieti. Ilikuwa kama chuo kikuu kwetu"

 • Wanjeshi wa Ujerumani Mashariki wantizama kupitia ukuta wa Beerlin

  Elimumwendo ya Lugha

  Katika historia yake, BBC imepeperusha matangazo yake katika lugha 68. Nyingi ya Lugha hizi zimekuwepo na kwenda ikiwemo, Maltese, Gujarati, Kijapani, na Welsh iliyotumika kwa ajili ya idhaa ya Potagonia. Kuanguka kwa ukuta wa Berlin, ilikuwa ishara ya enzi mpya Ulaya Mashariki na BBC ikawa sio muhimu sana kwa watu wa nchi hizo kama ilivyokuwa mwanzoni. Kwa hivyo nyingi ya idhaa za nchi hizo zikafungwa ili kuweza kufadhili vitengo vingine vya BBC ikizingatiwa bajeti yake ambayo ilikuwa inapungua. idhaa hizo zikafikishwa 28 zikipeperusha matangazo yao kupitia mtandao tu.

 • Wanjeshi wakiwa kwenye Lori

  Habari za uetendeti

  Wakati tawala za Kisovieti zillipoporomoka miaka ya tisini, kulikuwa na eneo jipya lililokuwa linatokota katika Ghuba. Tarehe 2 mwezi Agosti, mwaka 1990, majeshi ya dikteta wa Iraq, Sadam Hussein walivamia Kuwait. Wakati uvamizi ulipoanza, mwezi Januari mwaka 1991, World Service, iliondoa mpangilio wa vipindi ili kuweza kupeperusha habari na kuweza kuzungumzia maswala ya dunia kwa mara ya kwanza.

 • Mjumbe maalum Terry Waite mjini Beirut muida mfupi baada ya kushikwa mateka.

  Mateka wasikiliza

  Redio ya BBC World Service, imekuwa chombo muhimu kwa watu kote duniani kwa walioshikwa mateka nje au ndani ya nyumba zao. Mnamo mwaka 1986, msomi Brian Keenan, mwandishi wa habari wa televisheni, John McCarthy na mjumbe maalum Terry Walikamatwa Lebanon na wapiganaji wa kiisilamu. "nilisikiliza World Service kila wakati" alisema Terry White, nilisikia binamu wangu akitangza katika kipindi cha Outlook, na hicho kilikuwa kitu muhimu sana kwangu. "

 • Mikhail Gorbachev aonekana kwa mara ya kwanza baada ya mapinduzi ya Agosti mwaka 1991

  Sifa kutoka kwa Gorbachev

  Wakati Mikhail Gorbachev aliposhikwa kwa siku tatu nchini Urusi, Agosti mwaka 1991, mawasiliano yake na dunia ilikuwa tu kupitia idhaa za kimataifa za redio. aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa World Service John Tusa, alikumbuka mkutano wa waandishi wa habari ambapo Gorbachev alisema kuwa BBC ilisikika kwa uzuri na ilishinda redio. zengine. Ina maana kuwa sifa zilitolewa kwa BBC kwa ujumla na kwa idhaa ya kirusi.

 • Mlinda amani wa umoja wa mataifa akimbeba mtoto mdogo nchini Rwanda

  Jukumu lisilofaa la Redio

  Redio ilikuwa na jukumu kubwa sana katika matukio nchini Rwanda mwaka 1994. Redio Mille Collines, redio ya Rwanda, ilichochea chuki na uhasama kati ya Watutsi na Wahutu. BBC ilisaidia, kutuliza hali kufuatia ombi la mashirika ya misaada. wasimamizi wa vipindi kutoka idhaa za Kifaransa na kiswahili, walisaidiana na shirika la msalaba mwekundu kuwasidia mamilioni ya watu walioachwa bila makao na vile vile kutoa taarifa kuhusu watu waliopotea. Idhaa hiyo baadaye iliweza kupanuliwa na kuwa idhaa ya maziwa makuu.

 • Mwanaume akiwa amefunikwa na vumbi lililotoka kwenye jumba la World Trade Centre.

  Hatua za haraka

  Tarehe kumi na moja mwaka 2001, wakati mashambulizi yalitekelezwa dhidi ya jumba la World Trade Centre nchini Marekani, waandishi katika Bush House mara moja walipigwa na butwaa hali ikawa ya taharuki. Mhariri msaidizi Rachel Harvey alilazimika kusimama juu ya dawati lake ili kutuliza waandishi na punde kutoa mwelekeo wa namna ya kupeperusha habari hizo kwa siku nzima.

 • Mtangazaji wa televisheni ya kiarabu Tony El-Khoury (Kushoto)

  Televisheni ya kimataifa

  Idhaa ya kiarabu ilianza kupeperusha matangazo yake kupitia televisheni mwezi Machi mwaka 2008, na kufuatiwa na idhaa ya kifarsi mwaka uliofuata. Haikuwa mara ya kwanza World service kutangza kupitia televisheni. Matangazo ya televisheni ya kimataifa ya kiingereza yalianza mwaka 1991kupitia televisheni ambayo baadaye iliitwa World TV mwaka 1996 na kisha sasa inaitwa BBC World News.

 • Alan Johnston

  Kukamatwa kwa mtutu wa bunduki

  Mwandishi wa BBC aliyekuwa Gaza Alan Johnston, alikamatwa kama mateka na wanamgambo mwezi Machi mwaka 2007. Aliachiliwa siku miamoja kumi na nne baadaye. Wakati huo kipindi cha mahojiano cha televisheni, World Have Your Say, kilipeperusha matangazo kuonyesha wasikilizaji wakimtakia kila kheri mwandishi huyo. sio mara ya kwanza mwandiosihi wa BBC emshikwa katika hali hiyo, baadhi wamekatwa na kuteswa na hata familia zao kutishwa. Baadhi wamekufa. Taaluma ya uandishi wa habari inaendelea kuwa hatari.

 • Mtoto akichungulia klupitia kitambaa katika kambi

  Utangazaji wa chanzo kwa watu

  Wakati wa tetemeko la ardhi nchinin Haiti ishaa ya BBC ya visiwa vya Caribbean, ilitangaza kipindi cha dakika ishirini kila siku kwa lugha ya Haiti, kuweza kutoa taarifa muhimu kuwasaidia watu kuweza kupokea maji na chakula pamoja na dawa baada ya tetemeko hilo lililotokea tarahe kumi na mbili Januari mwaka 2010. Kando na kutoa taarifa za usaidizi kwa waathirika wa tetemeko hilo, kipindi kiliwasaidia watu kuweza kuwasiliana na jamaa zao waliokumbwa na tetemeko hilo. Pia kilitoa fursa kwa wanamuziki wa kigeni kuwafikia waathirika wa tetemeko .

 • Mwanume mwenye tabasamu akibeba bango lenye maelezo kuhusu Face Book

  Mtandao wa kijamii.

  Wakati wa mapinduzi ya kiraia katika nchi za kiarabu, mwaka 2011, mitandao ya kijamii uligeuka na kuwa chanzo muhimu cha habari kwa waandsihi wa habari katika eneo hilo. Matukio mawili yalionekana kuwa muhimu sana. Mwanzo mitandao hiyo ilibainika kuwa chanzo kikubwa cha habari kwa waandishi wa habari, pili, kupeperusha habari hizo kulifanya wasikilizaji kuwa sehemu ya habari za BBC World Service na namna ambavyo BBC inakusanya na kupeperusha habari zake.

 • Aung San Suu Kyi

  A Jolly Good Show

  Novemba mwaka 2010, kiongozi anayepigania demokrasia, nchini Syria, ung San Suu Kyi, aliachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Burma. Katika mahojiano baadaye, alisema kuwa alisikiliza BBC World Service, wakati wa kuzuiliwa kwake na kusema kuwa pamoja na vipindi vingine alipenda kusikiliza kipindi cha ombi la muziki cha A Jolly Good Show ambacho huendeshwa na DJ Dave Lee Travis. Alisema kuwa kusikiliza kwake kwa BBC kulimkamilishaia mtukio duniani.

 • Jumba jipya la matangazo ya BBC

  Nyumba mpya

  Mwaka 2012 BBC World Service, inahamia katika jumba la Broadcasting House ila tu wakti huu limefanyiwa ukarabati wa hali ya juu na kuwa jumba la kifahari la matangazo yake baada ya miaka sabini na moja katika Bush House. Waandishi wa habari wotw sasa watakuwa katika jumba moja na wafanyakazi wengine wa BBC mfano waandishi wa mtandao pamoja na wenzao wa Televisheni ili kuweza kuweka habari za kimataifa katika kitovu kimoja.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.