Huwezi kusikiliza tena

Lubanga watetezi wadai hana hatia

Bosco Ntanganda mtu aliyekuwa naibu wa mbabe wa kivita wa zamani,DRC, Thomas Lubanga, amemtetea vikali aliyekuwa kiongozi wake.

Hii ni baada ya mahakama ya jinai ya ICC kumpata Lubanga na hatia ya uhalifu wa kivita katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Akiongea na BBC, Ntanganda aliyekuwa naibu kamanda mkuu wa jeshi la waasi la Thomas Lubanga (FLPC) eneo la Ituri, amekanusha madai kuwa kundi lao la waasi lilihusika na visa vya mauaji pamoja na kuwatumia watoto kama wanajeshi.

Lubanga aliyekamatwa mwaka 2005 mjini Kinshasa, anatuhumiwa na kuwatumia watoto wa chini ya umri wa miaka 15 kama wanajeshi pamoja na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya watu wa Ituri

Mahakama ya jinai ya ICC, inatarajiwa kutoa hukumu ya adhabu atakayopokea Lubanga baadaye.

Zainab Deen alizungumza na Bosco Ntaganda kufahamu hisia zake kuhusu uamuzi wa mahakama ya ICC dhidi ya bwana Lubanga.