Huwezi kusikiliza tena

Muraya Jr azungumza na Sanaa

Image caption Wimbo wake mmoja unawapa shukrani wafanyakazi wa nyumbani wa kike, 'mayaya'.

Katika makala ya Sanaa ya Jumapili, tarehe 18 Machi, mwanamuziki wa Kenya, Patrick Mwangi Muraya, kwa jina la usanii Muraya Junior, atueleza kwa nini, kinyume na wanavyofanya vijana wengi, yeye ameamua mbali na kuimba nyimbo za mapenzi, kutunga wimbo pia kuhusu wafanyakazi wa nyumbani wa kike, wanaojulikana zaidi kama mayaya.

Muraya, ambaye huimba kwa lugha za Kikuyu na Kiingereza, anasema wafanyikazi hawa wana jukumu muhimu katika maisha ya kila siku katika familia nyingi, na wanastahili kupongezwa.

Patrick ni kijana wa marehemu Sam Muraya, aliyekuwa mashuhuri kwa nyimbo zake kwa lugha ya Kikuyu.