Huwezi kusikiliza tena

Mwanamfalme ashindwa kupata mchumba

Mwana wa mfalme, au Prince Harry kama anavojulikana hivi karibuni alijieleza kwa kirefu kuhusu tatizo linalomkabili la kushindwa kumpata mchumba.

Alisema kua hofu yake ni kwamba wanawake wengi wanahofia shughuli zake katika Familia ya Kifalme' na kusema mara kwa mara hujiwa na fikra labda ingekua bora kama angekua mtu wa kawaida na siyo wa familia ya kifalme.

Licha ya kua mmojapo wa wanaume ambao bado wanaishi maisha ya upweke, Harry aliliambia TV ya Marekani kwamba amekua akijitahidi kumpata mpenzi bila mafanikio na kufikia uwamuzi wa kua tayari kujivua hadhi ya Kifalme labda anaweza kufanikiwa.