Huwezi kusikiliza tena

Uingereza yakiri kudhulumu Mau Mau

Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Serikali ya Uingereza imekiri kwamba uliokua ukoloni wa Uingereza nchini Kenya ulitekeleza dhuluma za kibinadamu dhidi ya raia waliozuiliwa katika kambi zilizotengwa kuwaadhibu wanachama wa vugu vugu la Mau Mau ambalo liliendesha harakati za kudai uhuru wa Kenya. Dhuluma hizi zilifanyika baada ya kutangazwa hali ya hatari nchini Kenya mwaka wa 1952.

Hatua ya sasa inafuatia ombi la mashujaa wa uhuru wa Kenya ambao wanataka mahakama kuu ya Uingereza kuamua ikiwa wana haki ya kufungua kesi dhidi ya serikali kutokana na dhuluma zilizotekelezwa na ukoloni huo.

Ng'endo Angela anafuatilia kesi hio kwa karibu na leo amezungumza na Wakili Paul Muite aliyeanzisha harakati ya kutafuta haki ya mashujaa hawa kwanza ikiwa kuna nafasi ya wao kuishtaki serikali ya Uingereza.