Huwezi kusikiliza tena

Machafuko siku ya pili Mombasa

Vurugu zimezuka kwa siku ya pili hii leo mjini Mombasa baada ya kifo cha mhubiri tatanishi aliyeuuawa kwa kupigwa risasi.

Aboud Rogo Mohammed alidaiwa kuwasajili wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kuenda kupigana nchini Somalia.

Hata hivyo haijulikani nani aliyemuua muhubri huyo hasa baada ya polisi kukanusha madai kuwa walihusika.