Huwezi kusikiliza tena

Waziri hana pesa za nyongeza ya mishahara

Serikali ya Kenya imesema kuwa haiwezi kutimiza matakwa ya walimu wa shule za misingi wanaogoma nchini humo huku mgomo wao ukiingia siku ya pili.

Waziri wa elimu Mutula Kilonzo ameelezea BBC kuwa matakwa ya walimu ya kuongezwa asilimia miatatu ya mishahara yao haiwezekani kwa sababu pesa hizo hazikujuimshwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka huu.

Waziri huyo aliongeza walimu hao walichezewa sherehe miaka kumi na tano iliyopita wakati walikubaliana na serikali wakati huo kwamba mishahara yao ingeweza kuongezwa kwa asilimia miatatu.

Waziri Mutula Kilonzo alizungumza na mwandishi wa BBC Nyambura Wambugu