Huwezi kusikiliza tena

Mgomo wa madaktari nchini Kenya

Madaktari nchini Kenya leo wanaanza mgomo wao kushinikiza nyongeza ya mishahara huku sekta ya afya ikiwa katika tisho la kuathirika.

Madaktari hao watajiunga na Walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiendelea na migomo kwa wiki ya pili sasa.

Madaktari hao kutoka hospitali za umma wanasema kuwa serikali imepuuza onyo lao la kugoma ikiwa haitatimiza matakwa yao.

Madaktari hao wanasema kuwa serikali iliwahadaa baada ya kukataa kutekeleza makubaliano waliyoafikia mwezi Disemba mwaka jana ya kutimiza matakwa yao ya mishahara bora na mazingira mazuri ya kazi na mafunzo ya kitaaluma.

Mariam Dodo Abdallah amezungumza na Daktari Victor Ng'ani, ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Madaktari hao wanaogoma, na kwanza kumuuliza kilio chao hasa ni kipi ?