Huwezi kusikiliza tena

Pata shika migodini

Wachimba migodi wa Lonmin Platinum walikubali nyongeza ya asilimia 22 ya mishahara wiki hii na kisha kurejea kazini lakini kabla ya maafikiano ilikuwa vurugu na ghasia ambazo zilisababisha mauaji ya wafanyakazi 44 wa sekta ya madini. Sasa baada ya kuridhia nyongeza hiyo , sekta ya madini inaweza kutabasamu baada ya wachimba migodi kurejea kazini.