Huwezi kusikiliza tena

Damu yamwagika Tana

Zaidi ya watu 100 wameuawa katika mapigano kati ya wapokomo na waorma (wakulima na wafugaji) wanaozozania ardhi na maji katika eneo la Tana river na kisha baadaye kilichodhaniwa kuwa makaburi ya siri yakafukuliwa ingawa hakuna kilichopatikana ndani ya makaburi hayo mbali na mguu mmoja wa mtuu.

Zaidi ya watu elfu tano wameachwa bila makao baada ya kutoroka mapigano na mashambulizi ya kuvizia kulipiza kisasi kati ya jamii hizo mbili.

Taarifa hii inasimulia mambo yalivyokuwa wakati wa mapigano ya kulipiza kisasi Tana River kwa zaidi ya wiki tatu.