Huwezi kusikiliza tena

Damu yamwagika Tana

Polisi na wataalamu wa uchunguzi wa maiti walipigwa na butwaa baada ya kukosa kupata chochote katika kilichodhaniwa kuwa makaburi ya siri katika eneo la Tana River kufuatia wiwki tatu za makabiliano kati ya jamii mbili hasimu.

Mzozo wa kikabila kati ya wapokomo na waorma ambao ulisababisha mauaji ya zaidi ya watu miamoja ndio umeanza kutulia. Maelfu ya watu waliachwa bila makao huku nyumba zikiteketezwa.

Taarifa za awali zilisema kuwa huenda watu wa jamii ya wapokomo iliwaondoa maiti katika makaburi hayo wakati polisi walipokuwa wanasubiri kibali cha mahakama kuweza kuyafukua. Sasa hali ilikuwa vipi katika eneo hilo na nini hasa chanzo za mzozo huu? Taarifa hii inasimulia zaidi.