Angalia matiti uongeze umri

Angalia matiti uongeze umri
Matiti ya wanawake yanatofautiana kwa ukubwa

Chanzo cha picha, INTERNET

Maelezo ya picha,

Matiti ya wanawake yanatofautiana kwa ukubwa

Tuseme wewe ni mwanamume na watafuta mchumba , kitu gani utakachoangalia kwanza kabisa?. Yaani kivutio cha kwanza ni kipi? Utavutiwa na nini au sehemu gani ya mwanamke?

Pole .Umekosea ,sivyo unavyofikiria?

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kitu cha kwanza kabisa wanaume anachoangalia katika mwanamke ni matiti. Naam Matiti.

Chuo kikuu cha Victoria University of Wellington nchini Uingereza, kimefanya utafiti na kubainisha kwamba kabla ya mwanamume kuangalia tabia, elimu au nasaba ya mwanamke wao hupiga jicho kwanza kabisa kifuani kuangalia kukoje?

Haya,mimi nadhani utafiti huu ulifanyiwa wazungu peke yao, sio waafrika. Lakini ndio utafiti wenyewe huo.

Watafiti hao wamegundua kwamba wanaume wengi huwa hawa kupiga jicho ...pa mara moja tu! Hapana! Wao huangalia kwa muda mrefu kabla ya kufikia uamuzi wa nimwambie au nisimwambie?.

Ni utafiti wa chuo kikuu cha Victoria kilichoko Wellington, mjini London, Uingereza.

......

Jee unafahamu kuwa matiti ya wanawake sio saizi moja? Kwa kawaida moja ni kubwa lengine ni dogo. Wanasayansi wanasema titi la kushoto kawaidi huwa ndilo kubwa kushinda la kulia. Lakini tofauti yao ni ndogo mno kiasi kwamba sio rahisi mtu kugundua utofauti hiyo.

.......

Sijiu kama unafahamu kuwa hata chuchu zenyewe za matiti zina tofautiana kwa ukubwa. Usihadaike ukaziona zote zimechomoka kifuani ukafikiri zinaelekea upande mmoja. La hasha! Chuchu moja inaelekea mbele nyengine upande kidogo

kwa sayansi hiyo ya kimaumbile , tukomee hapo kwa leo, Mungu akipenda tukutane tena wiki ijayo.

Mimi ni Odhiambo Joseph..