Huwezi kusikiliza tena

Nipe nikupe ya Silaha na Komputa

Serikali ya Libya imeanzisha mpango maalum wa kuwataka watu nchini humo kusamilisha silaha. Na sio hilo tu, bali serikali badala yake inawapa wananchi waliorejesha silaha zao tarakilishi aina ya Laptop, wanaweza kushinda magari na hata televisheni kubwa.

Je unadhani mpango huu utawashawishi watu kuachana na silaha wakati Libya ingali inakumbwa na hali mbaya ya usalama? silaha hizo zilizagaa miongoni mwa wananchi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomng'oa mamlakani Muamar Gaddafi.

Taarifa hii inasimulia mpango huo mpya.