Huwezi kusikiliza tena

Usalama Kenya watetereka

Wakaazi wa mji wa Kismayo, Somalia wamesema majeshi ya serikali na ya Umoja wa Afrika yameingia katikati mwa mji huo kwa mara ya kwanza tangu Al-Shabaab kuutelekeza mji huo mwishoni mwa juma.

Walioshuhudia wamesema wameona askari wakishika doria kwa miguu katika moja ya barabara kuu. Wamesema kuondoka kwa kundi hilo kumezua wasiwasi mkubwa na viongozi wenye ushawishi katika koo mbalimbali wameuawa.

Bila shaka matukio ya Somalia yanaigusa nchi jirani ya Kenya kwa njia moja ama nyingine. Suala la usalama ndio hasa jambo kuu. Naibu waziri mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi alizungumza na Salim Kikeke mjini London, kuhusu masuala hayo,mwanzo akielezea hatua iliyofikiwa.