Huwezi kusikiliza tena

Nilivyonusurika kifo kutokana na madawa

Uraibu wa madawa ya kulevya ni tatizo sugu nchini Kenya hasa pwani mwa nchi hiyo. Shirika la kupamana na utumiaji huo limekuwa likifanya miradi mingi tu kusadia vijana hasa waliotumbukia kwenye uraibu kuweza kujikwamua.

Fatma Musau ni mmoja wa wale waliaosi uraibu sasa kwa miaka kumi na saba. Alisimulia alivyonusurika kifo na alivyotumia talanta yake ya kuandika kujiliwaza wakati wa uraibu wake.

Aliongea na Zainab Deen kuhuhusu alivyoweza kujikwamua kutokana na uraibu wa madawa ya kulevya na ambavyo anawasaidia wanawake wengine waliokuwa kama yeye miaka kumi na saba iliyopita