Dunia kwa picha hii leo

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 16:40 GMT

Picha za siku

  • Mwanaharakati wa upinzani nchini Syria, anaendesha pikipiki Kaskazini mwa mji wa Aleppo.Waasi wametenga barabara kuu inayounganisha mji huo na Damascus na kukatiza usafiri wa wanajeshi kutoka sehemu moja hadi nyingine.
  • Mjadala wa wagombea wenza katika uchaguzi wa urais nchini Marekani. Joe Biden na Paul Ryan walimenyana vikali katika mdahalo wa wagombea wenza, huku kura za maoni zikionyesha wagombea wanatoana jasho kabla ya uchaguzi tarehe sita mwezi ujao.
  • Maadhimisho ya miaka kumi na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika mjini Bali Indonesia na kusababisja mauaji ya zaidi ya watu miambili. Watu kutoka nchi 21 walifariki katika mashambulizi hayo ambayo kundi la wapiganaji wa Jemaah Islamiah walitekeleza
  • Wanafunzi wakipambana na polisi mjini Santiago, Chile,wakati wa maandamano yao wakitaka serikali kuimarisha mfumo wa elimu mjini humo. Wakati baadhi walikuwa wakicheza densi ,wengine waliwafuata na kuwarushia mawe polisi.
  • Mwimbaji Usher Raymond akiwatumbuiza mashabiki kwa wimbo wa ''We Will Always Love You'' kumkumbuka gwiji wa muziki Whitney Houston mjini Los Angeles, California
  • Mwanamke anajiandaa kupaka rangi sanamu kwa sherehe za Navratri ambazo husherehekewa mara mbili kila mwaka nchini India
  • Wanaharakati wanaopinga kawi ya nuklia, wakipiga mayowe nje ya makao rasmi ya waziri mkuu wa Japan Yoshihiko Noda mjini Tokyo
  • Simone Corsi wa Italia wakati wa mazoezi ya Grand Prix ya Japan
  • Watu hapa wanawatizama walinzi wa rais wakiondoka katika eneo hili ambalo ni la kihistoria mjini Athens, Ugiriki wakikumbuka siku waliyojinyakulia uhuru kutoka kwa watawala wa Nazi

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.