Viongozi Afrika wameisha?

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 16:04 GMT

Media Player

Kwa mara ya kwanza katika miaka 6 tangu kuanzishwa wakfu wa Mo Ibrahim kuhusu utawala bora barani Afrika, tuzo hiyo imeingia mwaka wa tatu bila mshindi.

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Kwa mara ya kwanza katika miaka sita tangu kuanzishwa wakfu wa Mo Ibrahim kuhusu utawala bora barani Afrika, tuzo hiyo imeingia mwaka wa tatu bila mshindi.

Tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni tano inatakiwa kutolewa kila mwaka kwa kiongozi aliyechaguliwa kwa kuzingatia demokrasia na ambaye ameongoza taifa lake vizuri, kuinua maisha ya wananchi na hatimae kuondoka mamlakani kwa hiari.

Jopo linaloshughulika na suala hilo mwaka huu, sawa na mwaka 2009 na mwaka 2010 haukuwa na mshindi ambaye ameweza kutimiza vigezo vinavyotakiwa.

Solomon Mugera amezunguma na Salim Ahmed Salim ambaye ni mmoja wa wanakamati katika jopo la tuzo hiyo, amemuuliza wakfu huo hausikitiki kuwa azma yake inazidi kugonga mwamba.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.