Machungu ya vita vya Syria

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 16:25 GMT

Aleppo kunani?

  • Nyumba ambazo zimeharibiwa kwa makombora na mashambulizi ya angani katika eneo la Sha'ar mjini Aleppo. Mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria, imekuwa eneo muhimu ambako mashambulizi yanafanyika katika mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe ni vita vikali dhidi ya serikali ya Bashar al-Assad na jeshi la Free Syria. ''Ikiwa hutasikia makombora yakirushwa au ndege za kivita basi utasikia vifaru vikirusha mabomu.'' anasema Javier Manzano
  • Raia wanatafuta hifadhi katika duka moja baada ya ndege moja kuonekana ikizunguka katika mtaa mmoja karibu na makao makuu ya jeshi la Syria mjini Aleppo. Hii ni baada ya shambulizi la mabomu kuwaua watu saba karibu na eneo hilo ''katika kipindi cha siku mbili, nimeona idadi kubwa ya raia waliojeruhiwa na wengi ni watoto,'' alisema Manzano.
  • Mtoto mdogo analia kwa uchungu huku madaktari wakijaribu kumtoa marisau ya kombora ama (Shrapnel) baada ya mlipuko kwenye nyumba moja. Javier Manzano alisema kombora lilianguka nyumbani kwao msichana huyo na vipande vya marisau kuingia mwilini mwake,lakini kwa bahati majeraha hayakuwa makubwa na akanusurika. Hospitali mjini Aleppo zimekuwa zikilengwa maksudi na mashambulizi ya kiholela kutoka jeshi la Syria.
  • Mlenga shabaha wa jeshi la waasi, anajiandaa kushambulia wanajeshi wa serikali katika eneo la al-Arqoub mjini Aleppo. " Wakati unapowasili hapa Aleppo kuna njia nyingi za kufika katika msitari wa mbele wa mapigano.'' anasema Manzano . " Kawaida utasaidiwa na kikundi cha waasi hawa. Kwa wanajeshi ni vigumu kuwa pande zote mbili kwa wakati mmoja."
  • Mwanajeshi wa waasi hapa analia sana baada ya kifo cha mwenzake aliyefariki katika shambulizi lilofanywa na jeshi la Syria.''Waasi wanatoka pande zote ''anasema Manzano."Wanahisi kama hawana hasara yoyote katika vita hivi.''
  • Waasi wa Syria wanajaribu kutayarisha silaha zao, ambazo mwishowe wataziweka kwenye pickup. Javier Manzano anasema kuwa wengi wa wapiganaji hapa wanatoka sehemu nyingi za nchi , ni wakulima, seremala na hata wafanyabiashara.
  • Raia mmoja hapa anahojiwa na waasi baada ya kupatikana akiwa anatembea ovyo katika eneo la msitari wa mbele. Waasi hao wametuhumiwa kwa kuwatesa watu na kuna wasiwasi kuhusu kufika hapa kwa wapiganaji wa kigeni.
  • "watu wa Aleppo na kote nchini Syria, ambao nimeongea nao, wanaonekana kuwa na matumaini. Wanajua kitakachotokea baada ya vita hivi lakini nahisi kama wamepuuzwa na jumuiya ya kimataifa,'' anasema Manzano. Barabarani watu wanachukua muda kuongea nami kuniambia hisia zao na wananiheshimu kuwa mimi ni mkristo

Javier Manzano ni mpiga picha rais wa Mexico ingawa ana asili ya Marekani, yeye huishi nchini Afghanistan. Ametembea nchini Syriana hasa katika mji wa pili kwa ukubwa Aleppo. Ni Kitovu cha mapigano nchini humo kati ya serikali ya Rais Assad na waasi wa Free Syrian Army. Anasimulia kwa picha wanyopita watu wa Aleppo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.