Malawi yalilia AU kuingilia mzozo

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 16:49 GMT

Media Player

Rais Banda alisema Malawi inajiondoa katika mazungumzo ya mpaka na Tanzania na kufikiria kwenda katika mahakama ya kimataifa.

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Rais wa Malawi Joyce Banda ametaka Umoja wa Afrika kuingilia kati mzozo wa mpaka kati ya nchi yake na Tanzania.

Mapema mwaka huu Rais Banda alisema Malawi inajiondoa katika mazungumzo ya mpaka na kufikiria kwenda katika mahakama ya kimataifa.

Nchi hizo mbili zinavutana kuhusu wapi hasa mpaka halisi upo.

Ziwa Malawi, au Nyasa ni moja kati ya maziwa makubwa ya Afrika na ni la nane kwa ukubwa duniani. Ziwa nyasa linapakana na nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda alikuwepo London na amezungumza na Salim Kikeke kuhusu suala hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.