Mikate, Mikono na DRC.

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 16:42 GMT

Afrika picha

 • Mwanaume anasimama nyuma ya lori siku ya Alhamisi Mashariki mwa DRC ambako uasi unaendeshwa na wanajeshi waasi. Uasi huo ulianza mwezi Aprili na hakuna dalili kuwa utaisha hivi karibuni. Ripoti ya Umoja wa Mataifa ulihusisha Rwanda na Uganda na uasi huo kwa kusema wanaunga mkono waasi wa M23....lakini Kigali imekanusha madai hayo
 • Takriban umbali wa kilomita 1,600, mjini Kinshasa DRC, mwanamke anabeba mikate siku ya Ijumaa kando ya uwanja mmoja ambako mkutano wa viongozi wa nchi zinazozungumza kifaransa walikutana mwishoni mwa wiki jana
 • Mke wa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, Patience Jonathan, hapa anawasili katika uwanja wa ndege kutoka nchini Ujerumani. Alikuwa ameenda kwa matibabu kwa hali ambayo haijafichuliwa. Amekuwa nchini humo tangu mwezi Agosti
 • Yeni Kuti, mwanawe gwiji wa mziki wa nchi hiyo marehemu Fela Anikulapo-Kuti, anaonyesha viatu vya babake katika nyumba ya familia yake mjini Lagos ambayo sasa wanataka kuibadilisha kuwa makavazi kuhusu mwanamuziki huyo wa kale.
 • Wasichana wadogo wa Senegal, wakiwa wamevalia nguo za kitamaduni wanashika vibakuli vya mauawa wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Ufaransa Francois Hollande katika kisiwa cha Goree. Kisiwa hicho kinatambulika kama kumbukumbu ya kihistoria ambako kulikafanyika biashara ya watumwa.
 • Mnamo siku ya Jumanne wanajeshi wanashika doria katika soko la Abobo kufuatia vurugu kati ya polisi na vijana.Makabiliano yalianza siku moja kabla ya polisi kuwafurusha wachuuzi waliokuwa wameziba barabara.
 • Nchini Algeria mamilioni ya CD ambazo zilinaswa zikiuzwa kimagendo zinaharibiwa hapa baada ya msako wa polisi dhidi ya wauzaji haramu wa muziki.
 • Katika nchi jirani ya Tunisia waandishi wa habari wanagoma dhidi ya kile wanachosema ni serikali kuwanyima uhuru wa vyombo vya habari. Kufuatia kundolewa mamlakani kwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali mwaka jana, vyombo vya habari viliweza kupumua lakini sasa wanaharakati wanasema kuwa serikali imeanza kuwawekea vikwazo.
 • Katika ziara yake Kusini mwa Gabon, Rais Ali anaweka jiwe la msingi katika kile kitakachokuwa chuo cha uhandisi na kitafunguliwa katika miaka mitatu ijayo.
 • Wasomali wanapiga gumzo kwenye mkahawa ulio kando ya bahari, mjini Mogadishu. Zaidi ya mwaka mmoja tangu Al Shabaab kuondoka mjini humo,mji huo unashuhudia ukarabati mkubwa.
 • Katika jimbo la Somaliland mifugo hawa katika soko la Berbera wanasubiri kupelekwa nchini Saudi Arabia kwa maandalizi ya siku kuu ya Idd wiki ijayo baada ya Hajj.
 • Nchini Zimbabwe,mwanamke anatayarisha mahindi aliyovuna viungani mwa mji mkuu Harare.
 • Hapa nchini Afrika Kusini watoto wanafunzwa namna ya kunawa mikono na umuhimu wa kutumia sabuni kunawa mikono katika mtaa wa Soweto.
 • Maelfu ya wachimba migodi, Afrika Kusini, wakidai nyongeza ya mishahara hapa wanaandamana kuelekea ofisi za kampuni ya madini ya AngloGold Ashanti mjini Carletonville karibu na Johannesburg. Wanaunga mkono kiongozi rasmi wa upinzani Helen Zille

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.