Gesi Tanzania inafaidi nani?

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 16:24 GMT

Media Player

Nchi za Afrika mashariki zimegundua mafuta na gesi hali ambayo katika baadhi ya maeneo imesababisha mvutano wa rasilimali.

Sikilizamp3

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Kwa miaka mingi, Afrika imekuwa ikijulikana kwa sifa ya kuwa na rasilimali nyingi kama vile madini ya dhahabu, almasi, shaba na kuendelea.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za bara hili, zikiwemo zile za Afrika mashariki zimegundua utajiri mkubwa wa mafuta na gesi hali ambayo katika baadhi ya maeneo imesababisha mvutano wa rasilimali.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau kutoka Dar es Salaam amefanya mahojiano na mhandisi Joyce Kisamo ambaye ni mtaalamu mtafiti wa masuala ya gesi asili kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania, na kwanza alimuuliza, iwapo bara la Afrika liko tayari kutumia rasilimali hizi kwa manufaa ya wananchi wake?

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.