Bondia wa Tanzania abwagwa Afghanistan

Imebadilishwa: 31 Oktoba, 2012 - Saa 12:47 GMT

Ndondi Afghanistan vs Tanzania

  • Afghanistan iliaandaa pigano la kwanza la ndondi kuwahi kufanyika nchini humo huku kukiwa na ulinzi mkali sana. Matanzia Said Mbelwa alitoana jasho na muafghani Hamid Rahimi.
  • Hamid Rahimi ndiye bingwa wa ndondi nchini Afghanistan ingawa alitoana jasho na mtanzania Said Mbelwa ambaye ni mwanandondi wa kulipwa wa uzani wa Supper Middle
  • Ndondi zilipigwa marufuku enzi za Taleban lakini leo wawili hawa walipigana mbele ya mamilioni ya watazamaji na wapenzi wa ndoni nchini humo waliotizama mchuano huo moja kwa moja kupitia televisheni
  • Kauli mbiu ya shindano hilo ilikuwa i ''Kupigania amani na usalama'' na waandalizi wanatumai kuwa ujumbe huu umewafikia watu kote nchini humo
  • Wawili hao hawakushindania mkanda wowote bali watalikuwa wanasambaza ujumbe wa amani kwa watu wa Afghanistan
  • Hamid Rahimi alimshinda Said Mbelwa katika mchunao ambao kawaida ungepigwa marufuku chini ya Taleban, lakini usalama uliimarishwa vilivyo

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.