Makali ya kimbunga Sandy Marekani

Imebadilishwa: 31 Oktoba, 2012 - Saa 07:41 GMT

Media Player

Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu arobaini, 18 kati yao kutoka mjini New York

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Maelfu ya watu katika eneo la kaskazini mashriki mwa Marekani wamo katika kumbi za shule tofauti kwa usiku wa pili na katika hifadhi nyengine za dharura baada ya makaazi yao kuathirika na mafuriko kutokana na kimbunga kibaya kuwahi kutokea katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu arobaini, miongoni mwao watu kumi na nane kutoka jimbo la New York.

Zaidi ya nyumba milioni nane na maeneo ya kibiashara katika majimbo kumi na saba yamo gizani kwa kukosa huduma ya nguvu za umeme.

Usafiri umetatizika pakubwa na usafiri wa chini ya ardhi wa treni mjini New York huenda usifunguliwe kwa siku kadhaa zijazo.

Rais Obama anatarajiwa kuzuru majimbo yaliyoathirika zaidi kama vile New Jersey,baadaye hii leo.

Kimbunga hicho kimepungua kasi lakini wataalamu wanaonya kuwa shughuli ya kusafisha miji huendna ikachukua muda.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.