Kipindupindu nchini Sierra Leone

Imebadilishwa: 13 Novemba, 2012 - Saa 08:43 GMT

Sierra Leone Cholera

  • Msimu wa mvua unapokaribia kuisha, mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Siera Leone kwa miaka 15 umeanza kupungua. Mlipuko huo umeonyesha wazi mazingira wanamoishi watu katika mitaa duni mjini Freetown,ambako ndio kitovu cha ugonjwa huo.
  • Mtaa wa Kroo Bay, umesongamana watu waliohamia hapo toka vijijini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na sasa takriban watu 6,000 wako hapa. Kando ya mtaa huu kuna maeneo ya kutupa taka ambayo yanafika katika ufuo wa bahari ya Hindi.
  • Hali ya usafi hapa ni duni sana kukiwa tu na vyoo vichache safi. Watu wengi huenda haja kubwa hadharani hasa kando ya mto ambao unapitia katika mtaa huu wa Kroo Bay.
  • Kila mwaka wakati wa msimu wa mvua, mito hupasua kingo zake na kusababisha mafuriko katika mtaa huu ambao uko nyanda za chini. Chifu Alimammy Kamara, alilalamika kuwa ni hatua ndogo ambazo zimechukulwi kuzuia kufurika kwa eneo hilo. "Tunahitaji kujengewa kuta za simiti kando ya mito,'' alielezea chifu huyo.
  • Nguruwe hutembea ovyo kando ya mto , na kukula masalia ya chakula kwenye taka hizi. Chini kidogo kwenye mto huu, watoto wanacheza na hata kuogelea wakati wengine wakikojoa kando ya mto.
  • Ingawa visima vya maji vimewekwa katika mtaa huu, bado kuna tisho la maji hayo kuchafuliwa na kuwa chanzo cha maradhi. Shirika la Unicef linakadiria kuwa asimilimia 42 ya watu nchini Sierra Leon, hawana maji safi ya kunywa.
  • Katika mazingira kama haya, kipindupindu husambaa kwa kasi kupitia katika mitaa duni. Ingawa inatabiwa kwa urahisi, ikiwa utagunduliwa mapema, ugonjwa huo bado ni hatari hasa ambako vituo vya afya haviko karibu huku uhamasisho ukiwa wa chini mno.
  • Mnamo mwezi Agosti, Rais Bai Earnest Koroma, alitangaza ugonjwa huo kuwa janga la kitaifa wakati vifo vilivyotokana nao vilipoongezeka kufuatia mvua kubwa. Ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 280 mwaka huu.
  • Serikali kwa ushirikiano na mashirika ya misaada , zimejitahidi kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Lakini hadi mazingira safi yatakapoimarishwa hasa katika mitaa duni mjini Freetown na maeneo mengine ya nchi, ugonjwa wa kipindupindu utendelea kuwa tisho kubwa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.