Picha za matukio Afrika wiki hii

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 13:12 GMT

Afrika wiki hii kwa picha

  • Nchini Nigeria , ''Dambe'' ni mieleka ya kitamaduni ambapo wapinzani hupigana kwa kuvalia glove moja kwa raundi tatu. Hapa Issah Abu (kushoto) anamenyana na Ali Pillow katika shindano hilo siku ya Jumamosi lililoandaliwa kama sehemu ya tamasha la kitamaduni.
  • Mashariki mwa DRC, wanajeshi wa serikali walishiriki kwenye gwaride la jeshi kuonyesha nguvu zao katika mji wa Goma siku ya Jumatatu baada ya waasi kuondoka mjini Goma kufuatia shinikizo za viongozi wa Maziwa makuu.
  • Huku visa vya uwindaji haramu wa vifaru ukifika viwango vya juu nchini Afrika Kusini, walinda pori siku ya Jumanne walikagua ndege hii maalum inayoweza kutambua wawindaji haramu katika mbuga mashuhuri nchini humo ya Kruger. Wawindaji haramu huwaua wanyama hao kwa sababu ya pembe zao ambazo huziuza barani Asia ambako zinatumika kama dawa za kienyeji.
  • Baadhi ya wenyeji wa mji wa Goma, ambao una idadi ya watu wapatao milioni moja walifurahia sana baada ya waasi kuondoka kutoka mji huo na kudhibitiwa na jeshi la DRC. Zaidi ya watu laki saba wameachwa bila makao tangu mwezi Aprili ambpo mgogoro kati ya serikali na waasi wa M23 ulipoanza.
  • Uchagzui wa Ghana ambao una ushindani mkali umekuwa mfano wa tamasha huku ukifika kilele pale kampeini za uchaguzi zilipokamilika siku ya Jumatano siku moja baada ya mpiga kura huyu mjini Accra kuonyesha anavyovutiwa na chama cha rais John Dramani Mahama cha NDC
  • Wakati mwanamke huyu alionyesha uzalendo wake kwa chama cha upinzani kwa kupaka rangi meno yake ..rangi hizo za chama cha New Patriotic Party
  • Mwanajeshi wa Uganda, Namakula Flavia ni mcheza golf ambaye alishiriki katika shindano la wanawake la Omega Dubai Ladies Masters katika milki za kiarabu, siku ya Jumanne. Alitupwa nje ya mashindano hayo baada ya kushindwa.
  • Nchini Libya, wanawake walifanya maandamano mjini Tripoli siku ya Jumatano kudai uhuru zaidi wa kujieleza pamoja na uwazi serikalini. Waandamanaji wanaishutumu serikali kwa kupuuza ahadi zake ilizotoa baada ya kuong'olewa mamlakani kwa hayati Muamar Gaddafi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.