Burundi na Kenya kutoana jasho

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 08:38 GMT

Media Player

Mechi hiyo itakuwa ni ya mkondo wa kwanza, na wa pili utafanyika jijini Nairobi mwakani.

Tazamamp4

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Jumapili hii kuna kivumbi mjini Bujumbura wakati timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itakapochuana na Burundi kwenye mechi ya kufuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani.

Mechi hiyo itakuwa ni ya mkondo wa kwanza, na wa pili utafanyika jijini Nairobi mwakani. Kocha wa Kenya James Nandwa anasema amejumuisha wachezaji watano walioshiriki mashindano ya Cecafa ya kombe la Senior Challenge mjini Kampala. Nandwa ametoa onyo kwa Burundi wajiandae kwa kipigo kwa sababu anasema anajua mbinu zao zote.

''Burundi ni timu nzuri, lakini kwetu hawatuwezi, wanacheza dana dana lakini sisi tutatumia kasi na nguvu kuzima makali yao. Hatujalishwi na mashabiki wao wa nyumbani,'' asema Nandwa ambaye alisaidia Kenya kufuzu kwa fainali ya mechi za kombe la Senior Challenge wakashindwa 2-1 na Uganda Cranes.Timu ya taifa ya Burundi kwa jina utani Intamba Murugamba

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.