Ajali ya helikopta London kwa picha

Imebadilishwa: 16 Januari, 2013 - Saa 11:57 GMT

Aajali ya helikopta mjini London

  • Helikopta moja hii leo iliangukia mashine ya 'Crane' wakati wa shughuli ya ujenzi katika eneo la Vauxhall Kusini mwa London.
  • Iliarifiwa kuwa helikopta hiyo iligonga magari mawili wakati ilipoanguka ardhini . Polisi walisema baadaye kuwa watu wawili walifariki kwenye ajali hiyo. Mmoja alikuwa hali mahututi wakati wengine wanane wakipata majeraha madogo
  • Wazima moto walikuwa na kibarua kuuzima moto katika picha hii inayoonyesha vifusi vikiteketea
  • Ajali hiyo ilitokea katika barabara yenye shughuli nyingi mjini London kando na mto Thames karibu sana na vituo vya basi na treni vya Vauxhall ambavyo baadaye vilifungwa.
  • Sehemu ya machine ilianguka ardhini karibu na eneo la ujenzi
  • Zaidi ya wazima moto ishirini walifika katika eneo la ajali kuuzima moto
  • Baadaye ilikuja kuthibitika kuwa helikopta hiyo iliangukia mashine ya ujenzi juu ya jumba lenye ghorofa 51. Picha hii inaonyesha uharibifu uliofanyiwa mashine hiyo inayoning'inia kwenye jumba lenyewe
  • Moshi mkubwa ulionekana katika eneo la ajali hiyo
  • Eneo ambalo ajali ilitokea liko karibu na jengo la M16 lilio karibu na ubalozi mpya wa Marekani lakini baadaye hofu ya kuwa huenda ilikuwa shambulizi la kigaidi ilitupiliwa mbali
  • Ajali ilitokea wakati wa msongamano wa magari na kusababisha mtafaruku kwa wale waliokuwa wanatembea barabarani

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.