Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 10:12 GMT

Afrika wiki hii Cup

 • Watu wanawashangilia wendesha baiskeli siku ya Jumamosi. Hapa walikuwa wamefika takriban umbali wa kilomita 147, katika eneo la Tropicale Amissa Bongo, katika mashindano ya wiki moja nchini Gabon.
 • Siku tatu baadaye, mwanaume hapa anaonekana akiwa amebeba vifaa vya kuuza katika soko la baiskeli karibu na eneo la Segou, umbali wa kilomita 240 Kaskazini mwa Bamako, mji mkuu wa Mali.
 • Siku hiyo hiyo, mjini Segou, wavuvi wa Mali wanaonekana hapa wakivua samaki katika mto Niger,huku mwanaume aliye kando ya mto akipakia nguo zake baada ya kuziosha
 • Watoto katika kambi ya wakimbizi ya Goudebou, Kaskazini mwa Mali. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UN, lilisema wiki hii kuwa takriban raia 7,500 wa Mali walivuka na kuingia Mali, tangu kuanza kwa mashambulizi ya angani. Kulingana na UN,tangu mwaka jana takriban wakimbizi 337,000 wametoroka vita nchini Mali.
 • Siku ya Jumanne mfanyakazi katika kinu cha gesi nchini Algeria anaonekana akifanya kazi yake katika kiwanda hiki karibu na kiwanda cha gesi cha Amenas na Tigantourine, ambako mateka na wapiganaji wa kiisilamu waliuawa.
 • Ghasia na vurugu zilizuka mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya baada ya wafuasi wa vyama vya kisiasa kugawanyika kwa mirengo kufuatia uchaguzi wa mchujo uliofanyika mjini humo kusababisha vurugu
 • Mwanamke anayemiliki vibanda vya mboga nchini Sudan Kusini aokota mwavuli wake baada ya kuangushwa kwa upepo mkali
 • Maelfu wajitokeza kuhudhuria mazishi ya makamu wa rais wa Zimbabwe John Nkomo, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 baada ya kupambana na saratani, mjini Harare, siku ya Jumatano
 • Heka heka za mwanzo wa michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika yaliyoandaliwa nchini Afrika Kusini
 • Mashabiki wa soka walijitokeza kwa wingi kushangilia nchi zao nchini Afrika Kusini
 • Kando ya ziwa akina mama hawa wanabeba nyavu za kuvulia samaki huku mtoto mdogo akikimbia kumshika nguo mamake. Ni nchini Benin
 • Siku hiyohiyo, katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,waliweka bango lenye michoro iliyofanywa na wasanii ambao hawakuruhusiwa kufanya wakati kundi la al-Shabab lilipokuwa linadhibiti mji mkuu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.