Huwezi kusikiliza tena

Shangwe na vigelegele Timbuktu

Wakaazi wa mji wa Timbuktu walioutoroka mji huo baada ya wapiganaji wa kiisilamu wenye siasa kali, kuuvamia mji huo, zaidi ya miezi tisa iliyopita, wamepongeza sana hatua ta majeshi ya Ufaransa na Mali kuweza kuukomboa mji huo.

Wakaazi hawa walipoteza makaazi yao baada ya kulazimika kukimbilia usalama wao katika mji wa Gao.

Hawa ni baadhi ya wale waliokimbiliza usalama wao na wanaelezea matumaini yao kuhusu mustakabali wa Kaskazini mwa Mali.