Huwezi kusikiliza tena

Utalii waathirika Mali

Sekta ya Utalii ni sehemu muhimu ya uchumi wa nchi, lakini mgogoro wa sasa ambao umesababishwa na wapiganaji wa kiisilamu umepelekea kudidimia kwa idadi ya watalii wanaozuru nchi hiyo.

Majeshi ya Ufaransa, sasa yametwaa mji wa Timbuktu, ambao wapiganaji wa kiisilamu wamekuwa wakiudhibiti kwa karibu mwaka mmoja.

Wamiliki wa maduka ya reja reja wanatumai kuwa wageni wataanza kumiminika nchini humo hasa baada ya majeshi ya kigeni kusaidia katika kudhibiti baadhi ya miji

Ripoti hii inaonyesha hali uilivyo katika mji wa Djenne, ulio umbali wa kilomita 500 Kaskazini mwa Bamako