Huwezi kusikiliza tena

Hali siku za usoni itakuwa vipi?

“BBC inatafakari siku za usoni, - Je hali ya afya itakuwa vipi? elimu, usafiri na hata mapenzi.

Je hali ya usoni itakuwa vipi kwako? Shiriki dhindano letu na kuchangia mawazo yako kuhusu hali itakavyokuwa miaka ijayo na unaweza kujishindia komputa ya laptop .

Kuweza kukupa mweleko kidogo, tumewaomba wachoraji sita kutoka kote duniani kutupa mawazo yao ya siku za usoni.

Hebu tafakari ikiwa ungekuwa na maono yako ya siku za usoni? Tuambie ingekuwa nini na pia tuchoree picha inayoonyesha maisha yetu ya baadaye duniani.

Tungependa utumie mbinu yoyote itakayoonyesha picha , iwe uchaoraji wa vibonzo au filamu na ututumie picha ya taswira yako kuhusu dunia itakavyokuwa katika siku za usoni.

Jee unadhani dunia ingekuwa unavyoitaka wewe? Unaweza kutafakari hali yako itakuwa vipi katika siku hizo, je tutafanana vipi, tutakula nini na uhusiano wetu utakuwa vipi.

Tungependa mawazo yako, ambayo unadhani ni muhimu kwa watu kuyajua. Tutatangaza majina ya wale watakaokuwa na mawazo bora zaidi, ambayo yanatoa picha nzuri kuliko zote.

Tayari wachoraji sita maarufu , watengeza filamu na wapiga picha watengeza vibonzo, wamechora picha au taswira ya dunia katika siku za usoni na unaweza kujionea picha zao kwenye ukurasa huu. (http://www.bbc.co.uk/swahili/medianuai/2013/02/130207_what_ifswa.shtml)

Shindano hili limewekwa katika vitengo viwili,wenye kutuma picha na wenye kutuma video ya sekunde 50 na kutakuwa tu na mshindi mmoja katika kila kitengo.

Majaji watano wameteuliwa kutoka katika kila bara . Watachagua picha nzuri zaidi katika vitengo hivyo

Unaweza kujua zaidi kuhusu majaji hao kwenye ukurasa huu ([bbc.co.uk/whatif or bbc.com/what if]) Unaweza kutuma tu katika kitengo kimoja. Shindano hili litafungwa rasmi saa saba mchana saa za Afrika Mashariki mwezi Machi 2013.

Washindi wawili mmoja katika kila kitengo ataweza kujishindia Laptop yenye thamani ya dola 3,900.

Miongoni mwa yale majaji watakuwa wanaangalia, ni Ubunifu,Ubora wa picha, Mada na hisia inazoibua picha yako